Nape na January, wanasiasa wenye Historia zilizopinda

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Mara nyingi, vijana wengi wamekuwa wakiwalaumu wazee kuwa ndio wamekuwa chanzo cha maendeleo duni ya nchi yetu, upendeleo na ubaguzi, rushwa na uduni wa fikra mpya za kuweza kuistawisha nchi.

Lakini kiuhalisia, hata kwa upande wa viongozi waliokuwa vijana walipopewa madaraka ikawa ni laana tupu, huku baadhi ya wazee kama Mzee Warioba na Mzee Butiku waking'ara kwa uadilifu, ukweli, ujasiri na weledi.

Jambo la kujiuliza, ni kitu gani kimewafanya viongozi vijana kuwa hovyo kabisa hata wakilinganishwa na baadhi ya viongozi wazee ambao wameendelea kung'ara kwa hekima?

Ni hakika kuwa uzee, ujana au jinsia siyo sifa hata kidogo ya mtu kuwa kiongozi mzuri. Historia ya mtu inaeleza pia mtu huyo ni mtu wa namna gani, hata atakapokuwa mzee.

Fikiria mtu kama January Makamba, ambaye kuna ushahidi wa kutosha kuwa tangu akiwa mwanafunzi, alishiriki kuiba mtihani ili afaulu masomo yake wakati akisoma sekondari. Huyu, anaweza akaelewa kama kuna mafanikio kwa kufuata uadilifu, sheria na kanuni? Lakini na yeye licha ya kuandamwa na makandokando mengi, anaota kuwa anaweza kuwa Rais.

Ukimtazama Nape, alidiriki kudanganya hata umri wake ili awe kiongozi wa UVCCM. Yeye na mwenzie January ndio waliojitapa kuwa CCM ikikosa kura za wananchi, itashinda kwa goli la mkono. Hawa wawili ndio wakawa vinara wa uovu wa kutengeneza matokeo ya uchaguzi wakiiishi dhamira yao ya goli la mkono. Nape hata jina la pili analolitumia, wanaokoo wanajua siyo lake, lakini kwake haimpi shida kwa sababu kwa kutumia jina la Nnauye anaona anaweza kuungwa mkono na jamii ya Wamwera ambao jina la Nnauye lilikuwa kubwa.

Hawa watu wawili, kwa maamuzi ya mahakama, kuwa hakuna mbunge anayepatikana kwa kupita bila kupingwa, ni wabunge batili. Na Rais Samia, akawateua hawa wabunge batili kuwa mawaziri.

Wafikirie akina Mwigulu, Makonda, Sabaya, Gambo na Chalamila, eti hao ndio viongozi wa kizazi baada ya wazee. Kuna mwanga wowote kwa Tanzania ya kesho kupitia hawa watu? Nani mwenye busara, weledi, maono na hekima miongoni mwao?

Lakini wazee pia hawawezi kukwepa lawama, maana hawa vijana waliojaa makandokando na uchafu mwingi, wamefikishwa hapo na wazazi wao, akina Makamba, Kinana, Kikwete na Samia. Wanawajua watoto wao vizuri na mapungufu na uchafu wao, lakini yaelekea hawaumizwi na Taifa kutokuwa na uongozi usio na maono, wanachozingatia ni kuendeleza himaya ya majina yao. Lakini hawajui mapungufu ya hawa wana wao yanaondoa hata kile kidogo walichokijenga.

Mwalimu Nyerere alitawala muda mrefu kuliko Rais mwingine yeyote, lakini alitoka madarakani akiwa hajaacha hata mtoto wake mmoja akiwa Waziri au RC, kwa sababu aliujua uwezo wa watoto wake. Viongozi wa namna hiyo kwa sasa tumewakosa.
 
Tatizo linaanza na mfumo Mzima wa kuchakata wakapatikana wenye uwezo wa kuongoza vijana wapo chungu Mzima!

Tumejisahau Kidogo kwenye mfumo wa kuwatambua wanaoweza kuongoza

Bahati mbaya siasa za Tanzania wanao kuwa na access ya vipesa wakawalipa vijana ndo wanashadadiwa kuliko uwezo kamili wa mtu

Britanicca
 
Kin

Kinachowabeba hawa jamaa ni chama vinginevyo hapo upstairs ni vumbi tuuu ndio lipo jingi
 
Mbona Kuna tetesi hata CEO wa kampuni yetu ni form four failure,Lakini alipata degree na masters na sasa ni Honorable causa.hivyo michezo hii ipo muda mrefu sana

Tanzania ndio tuna waziri mkuu ambaye hakuchaguliwa na wananchi,kwa mujibu wa katiba waziri mkuu lazima apigiwe Kura na wananchi.
 
wote 2 wana uwezo mdogo sana kiakili!
Ndio maana hata wizara zao hawana ubunifu wowote zaidi usanii.
Inshort; hawana msaada wowote kwa mteule wao
 
Tatizo linaanza na mfumo Mzima wa kuchakata wakapatikana wenye uwezo wa kuongoza vijana wapo chungu Mzima!

Tumejisahau Kidogo kwenye mfumo wa kuwatambua wanaoweza kuongoza

Bahati mbaya siasa za Tanzania wanao kuwa na access ya vipesa wakawalipa vijana ndo wanashadadiwa kuliko uwezo kamili wa mtu

Britanicca
Upo sahihi. Ndiyo maana hata vijana wakipata nafasi yoyote, wanachofikiria ni kufanya ufisadi wa hali ya juu ili kuwa na pesa nyingi ya kuwahonga watu mbalimbali.

Nilishangaa nilipoambiwa utaratibu wa naibu PM kuwagawia milioni 10 kila mara wale wanaofanya vetting ili daima jina lake liwe zuri mbele ya mteuzi wake na PM. Na inaonekana inalipa, leo amepewa hata cheo ambacho hakipo kwenye katiba.
 
Hao wote vilaza
Vilaza wasioujua hata uwezo wao. Wazazi wamewaaminisha kuwa wana uwezo mkubwa kuwazidi wanaCCM wote.

Kwa sababu walifanikisha kusimamia zoezi la kupora kura zilizopigwa na wananchi, basi wanaamini wao wana akili za kutosha, angalao za kuwezesha wizi.
 
Kabisa naunga mkono hoja 👍👍
 
Back
Top Bottom