Nape JF sio sawa na Facebook

BARUA KWA NAPE ..........uliyemuandikia Nape Mosess Nnauye barua hiyo ww naona na mshabiki wa siasa na kundi hilo lilokutuma humu jamiiforum kufanya hivyo waambie wamechemsha ww ni mfuasi tu wa kundi la MAFISADI UKIJIFANYA MPINZANI WA CCM huna lolote kwa jinsi unavyojieleza ww ni CCM NA MFUASI WA KUNDI LA MAFISADI ila aahh..ahhh Nape nyie hamummsumbui yote mnayotaka kumfanyia mtachemsha na mshachemsha.

-Nape ataendelea kuandika anachoona kiko sawa kwake kama kiongozi wa CCM TAIFA katika Mtandao wa FACEBOOK na wewe ukiwa mfuasi wa kundi hilo la MAFISADI endelea tu kusema unachoona kwako sawa DOMO LAKO NDIO MALI YAKO HAKUNA ANAYEKUZUIA maana usiposema watakulipa mshahara wa bure kwani mnalipwa nyie vijana wa mafisadi, sasa endeleeni weee maana huo ndio mwisho wenu wa haya madudu yenu mnayoyafanya katika nchii, malizeni tu miaka yenu hii, ila mjue AWAMU INAYOKUJA MNAKAZI KWELI....nasema mnakazi kweli.....subirini mtaona nchi hii yetu sote, nyie mwaigeuza yenu peke yenu watu msiozidi 100.

-aluta kontinua.
 
Hiyo sifa kwa jamii apoteze mara ngapi?
Nitarudia tena hapa; Ukishaisaliti demokrasia ya Tanzania, hiyo demokrasia nayo itakusaliti kwa njia moja au nyingine.
Dr. Slaa alimtaja kuwa na yeye alifaidika na pesa sa EPA kupitia J. Patel, Nape aliishia kukanusha tu. Yaani siku hizi ukichafuliwa jina kwenye jamii unatakiwa kukanusha tu. Mbona wanaogopa mahakama?
 
wabongo njaa zitawaua, we sema umepewa ngapi uje hapa ulete ukatuni wako.


wewe ukilipwa ili ulete upupu jamvini unafikiri wote,ccm bwana wanafiki,leo ndiyo mmejua Rostam fisadi wakati mlikuwa mkimtetea sana,na bado hata hao mnao watetea leo,kesho mtawakana tena haaa haaaa .
na kwa vile mko likizo za akili zenu mtasahau lakini tutawakumbusha.wenye ccm yao wako kimyaaa! magamba mapya na ya zamani yananyukana safi sana,ila haya mapya naona hayko strategic kama ya zamani ingawa yameshika mpini.
haaaaa! haaaaaa! tuulizeni tuwashauri
 
Nape si wa kiwango cha JF, hata huyo mwenyekiti wake akanyagi mguu wake hapa nae anaishia huko huko facebook.
 
Ndo uwezo wake jaman. Anaweza kusema ila kulinda alichosema ni vigumu. Alianzisha mada ya mishahara kuwa ni ufisadi wajuvi wakamweleza je vp makamba alikuwa anakulaje? Je mkama ?akanywea,akaleta ya watu wa nyamongo na kikatuni, akaikimbia' n.k n.k.hapana uyu mtu cjui kama mzima kule kwenye ngazi za juu/upstairs. Nape namheshimu,lakini akileta utoto hapana sitamuelewa.
 
RACHEL, hawa wamekisaliti vipi CCM? Mimi nadhani hatuwezi kuwaweka hawa sehemu moja na SIMWANA. Nadhani mkubwa wao aliogopeshwa na mlisho nyuma kuwa CHEL walikuwa na muswada kuwa sio lazima Rais akalie kiti cha chama. Hivyo akaanza kutafuta njia ya kuwatoa kabisa lakini kumbe aliyepewa usukani wa kuendesha hilo jahazi hajakomaa vizuri. Na hili litarudi tu kung'ata mkiani!
Tunatumia muda mwingi kwa kuwajadili akina RACHEL badala ya kuangalia matatizo ya wananchi na jinsi serikali inavyoyatatua au inavyoshindwa kuyatatua ili tutoe hukumu ya kweli 2015 badala ya kuwajadili watu wachache ambao kwa mawazo yangu mmoja wao akipewa nchi hii ataipeleka mbali kwa maendeleo kwani ni mtu ambayo anafuatilia mambo na hapendi porojo. Hao wanaoitwa wasafi ni akina nani ndani ya CCM? Hakuna hata mmoja, shida tu ni kwamba ndani mwao wamezidiana uwezo wa kuongoza na kuwa na mali.

Yaani katika sample ya watanzania wote ukaona mmoja kati ya RACHEL akipewa nchi ataipeleka mbali? Pole sana hata wewe mwenyewe hujajiona unaunafuu kuliko hawa scavengers kuisaidia nchi yako? I hope Tanzanians have not reached to that stage na kama wewe siyo extrem bali ni representative ya a group within a normal distribution basi kazi tunayo!
 
Mkuu Radio Producer, mbona unajipotezea muda mwingi kushauri Nape? Viongozi wa CCM tangu lini wakajua kutumia mtandao?

Je unaweza kula pipi tamu iliyookotwa kwenye mtaro? Tafakari
 
Nape hawezi siasa za sasa, bahati mbaya sana wenye chama wamemkabidhi madaraka wakati wenyewe yamewashinda, hajui aanzie wapi zaidi sana anajichafua kwa kauli zake mwenyewe.

Kila mkutano, anatoa tafsiri tofauti ya kujivua gamba. Mkama kamtosa na ili tumkamate vizuri tunasubiri siku 90 tuone maajabu yake!
 
Mkuu tatizo wanadhani tunapowapa ushauri sisi nitofauti na ccm, wengi wetu humu ni wale tunaotaka maendeleo ya nchi yetu ufike mda tukajivunia kuwa sisi ni WATANZANIA, mimi naipenda sana nchi yangu ila kwa yanayotokea nchini SIYAPENDI, NAPENDA TANZANIA IWE NA MIPANGO DHABITI YA KUTOKA KWENYE HUU UMASIKINI, nchi hii mpaka leo umeme ni tatizo maji safi na makazi ya watu hakuna, na watu wanazidi kujaa mijini tuu, Nililitegemea mtu kama NAPE aweze kuongelea mambo hayo! Mbona makamba jr huwa tunamuunga mkono baadhi ya mambo yake ( ingawa sometimes anakuwa kama baba yake) Nape tulikuunga mkono uliposema mafisadi watoke ndani ya ccm na siku Tisini tunazisubili, Ulitakiwa pia uongee ulipofikia achapumba kijana! ( mimi nimwanachama wa ccm lakini ile ya Nyerere na si hii ya MAGAMBA)

inahitajika hekima sana ktk ujenzi mpya. Nguvu ya jamii ni nyenzo kuu. Ni lazima wenye dhamana wote tule na kucheza na watoto wa majalalan ili tujue nin mahitaji yao na tuwatoe huko waliko. Naamin inawezekana..tuondoe mipaka iliyopo tuwe wamoja
 
Safi sana mpe ushauri huyu dogo lakini kwa sababu anajiona nae amekuwa anaweza kuupiga teke ushauri wako, jaribu labda magamba yatapungua
 
Kaka umenena tena kwa busara kubwa sana, kazi kwakweli kujiangalia akiwa kavaa viatu vyake mwenyewe. Kama uwezo wake ni mdogo basi aanze kusoma na kunyanyua uwezo wake nadhani pia silazima atumie akili zake maana ameonyesha hana kitu kichwa kabisa, anaweza kutumia wataalam wakulipwa kumpa mambo ya kuongea na nini cha kufanya.

Kinachoniuma katika nchnin yetu na ninacho pigia kelele kila siku ni matumizi mabovu ya rasilimali watu; hapa kwa harahara naona kama wewe ndie ulipaswa kuwa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa CCM na si Nape nimefanya thathimini ya haraka inaonyesha wewe kama rasilimali ambayo ingeweza kuitumikia nchni yako ujapata nafasi yako staili na moja ya nafasi imezibwa na mtu hasiye na uwezo anaitwa Nape.
 
lakini mi si mlaumu anachokifanya ndio mwisho wa uwezo wake wa kufikiri hivyo anatuzihirishia kuwa yeye ni kilaza namna gani na hata cheo alichopewa si kwa uwezo wake wa kiuongozi bali ni muendelezo wa kujuana na kUpozana.

Ni hali halisi kama mwenyekiti ndo yule itawezekana achague watu wanao mzidi yeye?
Kwa ****** huyu ndo bonge la msomi wa chama!
 
BARUA KWA NAPE ..........uliyemuandikia Nape Mosess Nnauye barua hiyo ww naona na mshabiki wa siasa na kundi hilo lilokutuma humu jamiiforum kufanya hivyo waambie wamechemsha ww ni mfuasi tu wa kundi la MAFISADI UKIJIFANYA MPINZANI WA CCM huna lolote kwa jinsi unavyojieleza ww ni CCM NA MFUASI WA KUNDI LA MAFISADI ila aahh..ahhh Nape nyie hamummsumbui yote mnayotaka kumfanyia mtachemsha na mshachemsha.

-Nape ataendelea kuandika anachoona kiko sawa kwake kama kiongozi wa CCM TAIFA katika Mtandao wa FACEBOOK na wewe ukiwa mfuasi wa kundi hilo la MAFISADI endelea tu kusema unachoona kwako sawa DOMO LAKO NDIO MALI YAKO HAKUNA ANAYEKUZUIA maana usiposema watakulipa mshahara wa bure kwani mnalipwa nyie vijana wa mafisadi, sasa endeleeni weee maana huo ndio mwisho wenu wa haya madudu yenu mnayoyafanya katika nchii, malizeni tu miaka yenu hii, ila mjue AWAMU INAYOKUJA MNAKAZI KWELI....nasema mnakazi kweli.....subirini mtaona nchi hii yetu sote, nyie mwaigeuza yenu peke yenu watu msiozidi 100
 
Back
Top Bottom