Nape azomewa, Kinana amshusha jukwaani

chaikavu

JF-Expert Member
Apr 18, 2015
760
473
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameanza vibaya ziara yake wilayani Sengrema, Mwanza baada ya wananchi kumzomea.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana alilazimika kumshusha jukwaani na kisha aliwaomba radhi wananchi hao.

Tukio hilo limetokea leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Zeno uliyopo Sengerema mjini, Mwanza.

Katika mkutano huo, Nape alizungumza maneno yaliyowatibuwa wananchi hasa wale wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa UKAWA.

Kwenye kauli zake Nape ambaye yupo katika ziara moja na Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa, baadhi ya vijana wamekuwa wakipewa viroba ili wafanye fujo.

Nape aliwalaumu vijana hao kwamba, wanapewa pombe aina ya viroba na viongozi wa vyama vya upinzania ili kwenda kufanya fujo katika mikutano ya chama hicho tawala.

"Chadema kimechoka sasa hivi lakini nyie vijana bado mmeng'ang'ani tu, mnapewa viroba na vikisha panda mnashikilia bendera ya ‘Peoples Power' bila kufahamu kwamba, chama chenu kimeisha poteza mwelekeo.

"Kuna watu wanasema eti CCM ifungashe vilago vyake katika Wilaya ya Sengerema kwa kuwa Chadema inaingia katika uchaguzi huu, hicho kitu hakitawezekana na wao ndio wataondoka, mtang'ang'ania sana," amesema Nnauye.

Kauli hiyo iliyosababisha baadhi ya wafuasi wa Chadema kuanza kuzomea na hata kusababisha mkutano huo kusimama kwa saa moja.

Hata hivyo, Kinana hakuweza kuvumilia hali hiyo na kuamka kutoka sehemu aliyokuwa amekaa na kumfuata Nape kumwambia ashuke kutoka jukwaani na kutumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wananchi hao.

Katika hatua hiyo, Kinana alitumia nafasi hiyo kuwaweka sawa wananchi hao kuwa CCM ipo imara na haitetereke kwa chochote na kwamba, itatumia kanuni na misingi ya chama hicho katika kuijenga nchi na kuleta maendeleo.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimekuwa na nguvu kubwa.

Mwanahalisi online
 
haaaaaaaaa haaaaa saaaaaaaa fiiiiiiiiiiiiii saaaaaaa aaaaa naaaaaa
 
vikundi vya uzomeaji viimarishwe ukawa hukaa nyuma ya mstari jezi za kijani unapoishia sasa kina zzk na ccm hudhani ni wana ccm wenzao wakianza tu roporopo wanazomewa
 
Hii zomea zomea itazidi maradufu ikiwa ccm watasimamaisha mgombea fisadi au galasa, vile vile zomea zomea hii itapungua ikiwa ccm itasimamisha mgombea anayekubalika kwa wananchi, anayeakisi kile wananchi wanapenda, alietayari kupambana na kile wanachukia

Akipatikana mgombea safi, akauzwa na watu safi, basi atasaidia sana kurudisha imani ya watanzania kwa ccm, na atasaidia sana kuuza wagombea wa udiwani na ubunge wa ccm. Otherwise, hali ni mbaya kwa ccm kuekea October
 
Bado Kinana maana ukiona unashangiliwa sana jiandae kuzomewa ndio wakati wa CCM sasa umefika......
 
Hii zomea zomea itazidi maradufu ikiwa ccm watasimamaisha mgombea fisadi au galasa, vile vile zomea zomea hii itapungua ikiwa ccm itasimamisha mgombea anayekubalika kwa wananchi, anayeakisi kile wananchi wanapenda, alietayari kupambana na kile wanachukia

Akipatikana mgombea safi, akauzwa na watu safi, basi atasaidia sana kurudisha imani ya watanzania kwa ccm, na atasaidia sana kuuza wagombea wa udiwani na ubunge wa ccm. Otherwise, hali ni mbaya kwa ccm kuekea October

mkuu, pilau hata ikiwa tamu vipi ikiwekwa kwenye sahani iliyo ndani ya choo cha stendi haiwezi kulika!
 
sio kweli Kuwa watu wapanga kuzomea ila ukiongea pumba wakufanyeji, sawa na lowasa katavi watu wanamsikiliza yeye amekalia haijawai tokea,watu wakazomea
 
Back
Top Bottom