Nape amtaka Mnyika kujitokeza mbele ya Wananchi kuweka wazi Kiwango cha Elimu yake

Status
Not open for further replies.
Nape does not think....kinachorudisha nyuma maendeleo ya Tanzania ni kupima uwezo wa watu kwa kuangalia vyeti/kujuana........Hata kama Mnyika bado angekuwa darasa la saba yet he is outstanding and bright minded figure..ana uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo kujenga hoja na kuwapigania maskini wa nchi hiii...Hebu Nape tujibu...tumefaidika nini na maprofesa na madaktari wa CCM?wakina maghembe,muhongo na Nchimbi? we dont need certificates we need a bright mind........
 
Mnyika kajidhalilisha sana kwa kudanganya kiwango chake cha elimu. Angesema kaishia form six (6) asingechaguliwa? Katudanganya mangapi?

Kwa nchi za watu makini, Mnyika angetakiwa ajiuzulu kwa kuudanganya umma.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Shame on you mzee, hata kama ni open university,tayar ni elimu ya chuo,unachotaka zaidi ni nini gamba wewe?
 
kama hujaelewa nilichokisema , basi wewe ni mfano wa watu wenye tuzo nzuri ila kichwani ni povu tupu kama hili ulilotapika hapa.
Mwalimu anaweza akawa anacheti kizuri kwa sababu alisoma kwa ajili ya kufaulu mtihani, pia mwalimu uyo anaweza kufundisha ila akawa na uwezo mdogo wa kueleweka na wanafunzi kwa sababu yeye alikariri tu ili afaulu mtihani.
Mfano mzuri ni wewe mwenyewe, Maghembe pamoja na JK.

Ni hiari na utashi wako kuniweka katika kundi lolote unalopenda lakini ukwelu utabaki kuwa ukweli.

Sijui uko dunia gani. Naomba ujue kuwa, Kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya kiwango cha hali ya juu hakuna hiki kitu unachokisema kusoma kwa ajili ya kufaulu. HAKUNA.

Huyo mtu unayesema amesoma ili kufaulu na akafaulu. Kiuhalisia, kama angekuwa katika vyuo vinavyotoa elimu ya kiwango cha hali ya juu wala asingefaulu na kutunikiwa tuzo ya kitaaluma. HUU NDIYO UKWELI. Kwa maana kuwa, kuna watu wako na taaluma ambazo kiuhalisia hawakupaswa kupata na kwa sababu hiyo, hata hawakupaswa kupata hiyo kazi.

Kwako wewe huoni mankiti na tofauti ya mtu kuwa na tuzo ya taaluma aliyoipata kwa rushwa au kiujanja ujanja na yule aliyeipata kutoka chuo ambacho ni makini( standard) kwa merit. Kwa mawazo yako. Hawa wote unawapima katika itendaji ule ule. YOU MUST BE JOKING.

Bora niendelee kuwa na kichwa chenye povu kuliko kuwa na mawazo yako haya yenye kichwa kisichokuwa na povu.
 
Nape does not think....kinachorudisha nyuma maendeleo ya Tanzania ni kupima uwezo wa watu kwa kuangalia vyeti/kujuana........Hata kama Mnyika bado angekuwa darasa la saba yet he is outstanding and bright minded figure..ana uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo kujenga hoja na kuwapigania maskini wa nchi hiii...Hebu Nape tujibu...tumefaidika nini na maprofesa na madaktari wa CCM?wakina maghembe,muhongo na Nchimbi? we dont need certificates we need a bright mind........
Nape haja linganisha uwezo wa mtu na Elimu wala hilo lisikupe shida, Shida ya Nape kaja na hoja kua Mnyika kadanganya Elimu yake, Tumewaauliza hapa wapi Mnyika kadanganya hakuna alileta ushahidi kwa hiyo madai ya Nape yakua discolified hapa ndo hoja hakuna ishu nyingine
 
Unachofanya hapa ni kujenga hoja isiyojengeka ili kuharalisha hoja. Ukisema mitihani ya form 1V na form Six haivuji wakati huo huo ya darasa la saba na elimu ya vyuo vya juu inavuja ni kichekesho kama siyo mshangao. Kuna watu tulikuwa nao JKT ambao wao paper ya form six waliipata wiki moja kabla ya mtihani kitaifa na siyo wao tu, shuhuda zilikuwa ni nyingi na Kwa sasa hivi wako makazini baada ya kumaliza university. Usiniulize walimaliza vipi university. Kuna watu walikamatwa wakiwa na majibu kwenye mtihani wa form four na wakafutiwa matokeo. Point ninayotengeza ni kuwa, matatizo ya elimu ya kimagumashi haiko immune kwa O- level and A-level. Kwa hiyo hii point yako ni muflisi.

Sijabeza uwezo wa Mh. Mnyika hata kidogo. Hatuwezi kuanza kuhoji alipataje A's wakati sababu ya kufanya hivyo hatuna. Nimebeza analogy yako kwa sababu imeileta kisiasa kwa kubeza elimu inayotolewa under CCM bila kujua kwa kufanya hivyo unabeza hata uwezo wa Mh. Mnyika kupata A's.

Uwezo wa Mh Mnyika unajieleza wenyewe na ndio maana alisoma shule za vijapi maalum. Nabeza mtu aliyepata elimu kwa magumashi kama Nape, au hata mimi au hata wewe na wanafunzi wengi tuliosoma vyuo vya bongo, kumnyooshea mtu mwingine kidole kwa aeleze kiwango cha elimu wakati merit ya huyo mtu iko wazi kabisa. Thats all. Wako watu wa kumnyooshea Mh Mnyika vidole kuhusu elimu yake lakini Nape hayupo kwenye hilo kundi, yeye ni mmoja wa craps ambao wamepata masters kwa njia ambazo zina mashaka makubwa. Only kwa kuwa kuna mfumo CCM hakuna nafasi ya kuhoji ile masters yake ya mzumbe lakini ukiisha huu mfumo CCM sisi wengine tutaanzisha ubishi kwa baadhi ya watu kuwataka warudishe digrii ambazo hawakuzifanyia kazi bali walifanyiwa kazi na watu wengine na kupewa kama sadaka
 
Gazeti lenyewe ni la ''UHURU'' wa Wapuuzi. Jambo la muhimu alilotakiwa kusema NAPE a.k.a ''MWANAHARAMU'' ni km amempata babayake ua la!, kabla ya MNYIKA kutaja kiwango chake cha Elimu na
 
Ikiwa kweli Mh Mnyika ana elimu ya Form 6 kama anavyodai huyo, na siyo ya Chuo Kikuu; basi anastahili heshima ya kipekee kuliko angekuwa na elimu ya Chuo Kikuu, kutokana na kazi zake zilivyo mahiri!

Go go Mnyika!
Ishu hapa ni kweli Mnyika kadanganya au la? mpaka sasa hakuna aliyethibitisha hili, hayo mengine ya uwezo wala yasikupe shida hayapo kwenye hoja hii!
 
Elimu ni kilichobaki kwa head after kusahau ulichojifunza shuleni,baada ya kusema hayo naomba nipite speed nisijepewa ban kwa kuandika ninayofikiria kuhusu Nepi
 
Kuzaliwa Dar ni form six tayari, Kuweza kuishi dar ktk midle class level ni masters tayari, kuweza kushawishi watu wasiopungua 32,000 wakupigie kura ni doctrate tayari kushinda kiti cha ubunge chama cha upinzani jimbo muhimu katikati ya jiji hapa unakuwa prof. So bwana nape kwakuwa mnyika aliweza ulichoshindwa hata kupenya kwenye chama chako tu ujue dogo mnyika ni Prof kwako ! teh tehh
 
Elimu ni kilichobaki kwa head after kusahau ulichojifunza shuleni,baada ya kusema hayo naomba nipite speed nisijepewa ban kwa kuandika ninayofikiria kuhusu Nepi
..aaaaah ! rudi bhana, hamna ban kwenye kweli bana,tupe vitu vya nap e si kalianzisha mwenyewe si kazi yetu ndogo tu,kumalizaaa
 
Mnyika kajidhalilisha sana kwa kudanganya kiwango chake cha elimu. Angesema kaishia form six (6) asingechaguliwa? Katudanganya mangapi?

Kwa nchi za watu makini, Mnyika angetakiwa ajiuzulu kwa kuudanganya umma.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

wewe ukisema hvyo mbona kina mwigulu wenye kusomea majina ya wa2 wataacha weng sana akina mulugo na wengne weng tu,
 
Nape ndugu yangu kila siku nakwambia jivunze kupitia vya vya nje vyenye majina makubwa kama CCM,unakidhalilisha chama wewe unajua wadhifa ulio nao ni mkubwa sana wewe siyo wa kufanya siasa hizo,siasa hizo waachie akina Juliana Shonza na wengine,msemaji wa chama unaongea utumbo????Elimu ya Mnyika itatuletea maji sisi wana ubungo????njoo n point siyo kinyesi ulichojaza kichwani Foolish!!!!
 
Jamani mbona huyu Nape kazi yake kubwa ni kujadili na kupakaza mambo ya watu, alianza na Dr Slaa sasa amehamia kwa Nyika, kwani kazi yake ni kufuatilia watu, au kusaidia katika ujenzi wa taifa hili???? Wabunge wangapi hasa wa CCM eilmu yao ni ya chini, mbona CHADEMA hawatumii huo mtaji kuchafua watu, hiyo ina faida gani katika ujenzi wa taifa letu Tanzania?????


kwake yeye itikadi na uenezi = UDAKU
ndicho anachokijua vizuri na ndio elimu yake inachomfanya achanganue mambo ya namna hiyo tu. sio kutafakari kwa upeo wa hali ya juu kabisa juu ya changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku na suluhu zake.
 
yeye huyo huyo nape asisubiri mnyika akanushe au la kama kweli yeye anaushahidi na anayoyasema aweke hadharani sio kumchafua mwenzake kwa siasa zake za maji taka.
 
Mnyika kajidhalilisha sana kwa kudanganya kiwango chake cha elimu. Angesema kaishia form six (6) asingechaguliwa? Katudanganya mangapi?

Kwa nchi za watu makini, Mnyika angetakiwa ajiuzulu kwa kuudanganya umma.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Hujakosea Mkuu.. Kwa mwendo huo huo nae Katibu mkuu wa ccm angetakiwa ajiuzulu kwa kukiri kwake kuhucika kwa kampuni yake kusafirisha meno ya tembo.. Au..?
 
Kwanini Nape anataka kujua elimu ya mbunge mmoja tu na sio wote? Why only Mnyika?
 
Kweli Mnyika kiboko ya Nnape,kaka yangu mbona unamnanga hivyo mdogo wako?Hebu muache ale maisha yake kwa raha zake.ELimu yake inahusu yeye na familia yake,wewe wala mimi hainihusu.Kinachonihusu ni je ame-deliver?Perfomance yake ipo sawa?Mengineyo ni mamabo ya binafsi ya ndani ya nguo za mtu.Acheni siasa za kuvuana nguo.
 
Dr. Mkumbo,
Tutakushangaa kama na wewe unaingia kwenye ulingo wa spinning. Utamtunuku vipi mtu tuzo ya kitaaluma wakati uwezo wake wa kifikra ni mdogo. Unataka kutuaminisha kama tuzo za kitaaluma hazina maana yeyote. REALLY?. Mbona hii kitu siielewi.

Zina maana sana, tena sana na wala mimi sisemi watu wasisome. Mimi nathamini sana elimu na ninapenda viongozi wawe na elimu ya kutosha. Nitachopinga ni kusema Mnyika ameficha kiwango shake cha elimu. Mnyika hajawahi hata siku moja kujipachika madigrii ambayo hana. Sasa hii habari ya kusema aweke elimu yake wazi inatoka wapi?
 
This proves wrong those who like to say Nape is not effective at his job. Well, Nape can change the national debate from religious tremors set to demolish the country to "Mnyika atoe vyeti vyake vya kuzaliwa."

Sasa unaweza kusema huyo sio effective leader, kwa saab anatutoa kwenye ya msingi, lakini huwezi kusema sio effective propagandist of his party, kazi yake by definition ni ofisa propaganda wa chama, he is an effective opinion leader who can broach a vigorous debate in the country. He is serving the party well and deserve every penny of his salary.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom