Nape acharuka uhamishaji wa kiwanda cha tumbaku Songea

Mar 23, 2012
64
13

Na Stephano Mango, Songea
KATIBU wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameitaka Serikali kurudisha Kiwanda cha kusindika tumbaku cha Songea Tobacco Processing Industry(SanTop) ambacho kimepelekwa mkoani Morogoro na kuwaacha wakazi wa Ruvuma wakilalamika kutokana na msaada mkubwa uliokuwepo wakati kiwanda hicho kikifanya kazi Songea
Wito huo ameutoa jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi,wanachama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) waliokusanyika kumpokea Kata ya Shule ya Tanga Wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako yupo katika ziara ya siku mbili
Nnauye alisema kuwa kiwanda hicho kilijengwa miaka mingi iliyopita na kiliwezesha kutoa ajira za muda mfupi na mrefu kwa wakazi wa mkoani humo na kusababisha kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa fedha na kukua kwa uchumi wa Ruvuma na wananchi wake.
Alisema kuwa wakulima wa zao hilo kwa muda wote huo walikuwa wakijivunia kuwepo kwa kiwanda hicho, hali iliyowafanya kuongeza juhudi katika uzalishaji wa tumbaku na kujipatia maisha bora kutokana na shughuli yao ya kilimo
“ Inasikitisha kusikia wajanja wachache kwa kushirikiana na wawekezaji, bila aibu waliamua kukihamisha kiwanda hicho na kupeleka Morogoro, ambapo hakuna hata mche mmoja wa tumbaku unaozalishwa huko,” alisema Nnauye
Alisema tangu kiwanda hicho kilipohamishwa kutoka mjini humo, uchumi wa mkoa na watu wake umeshuka na kusababisha mateso makali kwa wananchi kutokana na kunyang’anywa fursa yao ya kujipatia kipato na kupelekea majengo ya kiwanda hicho kuwa mahame ambayo popo wanajihifadhi na wadudu wengine katika umasikini
Aliwataka viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma kushirikiana kikamilifu na Serikali ili kuweza kukirudisha haraka iwezekanavyo kiwanda hicho ambacho kilikuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma
Katibu huyo ameanza ziara ya siku mbili mkoani Ruvuma ambako atafanya mikutano ya hadhara na wananchi, vikao vya ndani,kufungua mashina na matawi ya chama hicho pamoja na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya chama
MWISHO

Nape aache unafiki katika ni vema angeanza na kutimiza ahadi za chama tawala ya upatikanaji umeme wa uhakika kwa watu wa songea wanaoendelea kutaabika na mgao wa umeme uliokubuhu.
 
Nape hongera kwa hili ijapokuwa unakumbuka shuka wakati pameshakucha,
lakini kwa hili Nape nakupa Big up kwani hii ndio kazi ya chama tawala ni kusimamia serkali yake ambayo chama ndo imeiweka na kuhakikisha serkali mlioiweka inatekeleza ahadi na sio nyie kama chama tawala kuanza kupiga propaganda za kipumbavu kwa vyama vya upinzani eti za udini ukabila na kuzuia mikutano ya CDM na kuwatumia polisi kuwakamata wafuasi wa upinzani.
 
Kesi ya nyani unampelekea ngedere haaaa Nape anaigiza hapo anawaingiza mkenge wakazi wa songea kwani hilo la kuamishwa kwa kiwanda ndio anajua jana?
 
lazima atoe sapoti kwenye tumbaku....!

mteja wao mzurI sana....!
 
Speaking of kurudisha assets, CCM isharudisha uwanja wa Kirumba serikalini?
 
Apa ndo naposhindwa kuielewa hii serikali, nape anasema aya kama nani?? Kwani si ni ccm hii hii ndo iliyafanya aya madudu ya kuwaona wanasongea hawana umuhimu na kiwanda icho??
Nape acha usanii wako, halafu tumbaku zinazokuwa processed morogoro wazifanyeje?? Acha kuwadanganya watu wa songea, watanzania wameamka there is no cheep popularity ndugu yangu ata wa vijijini wameshajitambua na wameamka.
Msaada kwa watu wa songea jitahidi kuishauri serikali yako fisadi kuwaepusha na migawo wa umeme isoisha kila kukicha, o/w kiandae chama chako kuwa chama cha upinzani 2015
 
speaking of kurudisha assets, ccm isharudisha uwanja wa kirumba serikalini?

si kirumba tu, rudisheni uwanja wa kambarage wa shinyanga, kaitaba, ali h mwinyi, sheikh amri abedi wa arusha na vingine vingi tulishiriki kuvijenga kwa shinikizo na ubabe kwa odi za wote wakati hatukuwa wafuasi wa ccm, mjiandae kuvirudisha serikalini kwa lazima through process ya mahakama ivyo ni mali ya wote
 
Na Stephano Mango, Songea
KATIBU wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameitaka Serikali kurudisha Kiwanda cha kusindika tumbaku cha Songea Tobacco Processing Industry(SanTop) ambacho kimepelekwa mkoani Morogoro na kuwaacha wakazi wa Ruvuma wakilalamika kutokana na msaada mkubwa uliokuwepo wakati kiwanda hicho kikifanya kazi Songea
Wito huo ameutoa jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi,wanachama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) waliokusanyika kumpokea Kata ya Shule ya Tanga Wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako yupo katika ziara ya siku mbili
Nnauye alisema kuwa kiwanda hicho kilijengwa miaka mingi iliyopita na kiliwezesha kutoa ajira za muda mfupi na mrefu kwa wakazi wa mkoani humo na kusababisha kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa fedha na kukua kwa uchumi wa Ruvuma na wananchi wake.
Alisema kuwa wakulima wa zao hilo kwa muda wote huo walikuwa wakijivunia kuwepo kwa kiwanda hicho, hali iliyowafanya kuongeza juhudi katika uzalishaji wa tumbaku na kujipatia maisha bora kutokana na shughuli yao ya kilimo
" Inasikitisha kusikia wajanja wachache kwa kushirikiana na wawekezaji, bila aibu waliamua kukihamisha kiwanda hicho na kupeleka Morogoro, ambapo hakuna hata mche mmoja wa tumbaku unaozalishwa huko," alisema Nnauye
Alisema tangu kiwanda hicho kilipohamishwa kutoka mjini humo, uchumi wa mkoa na watu wake umeshuka na kusababisha mateso makali kwa wananchi kutokana na kunyang'anywa fursa yao ya kujipatia kipato na kupelekea majengo ya kiwanda hicho kuwa mahame ambayo popo wanajihifadhi na wadudu wengine katika umasikini
Aliwataka viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma kushirikiana kikamilifu na Serikali ili kuweza kukirudisha haraka iwezekanavyo kiwanda hicho ambacho kilikuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma
Katibu huyo ameanza ziara ya siku mbili mkoani Ruvuma ambako atafanya mikutano ya hadhara na wananchi, vikao vya ndani,kufungua mashina na matawi ya chama hicho pamoja na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya chama
MWISHO

In short anamwambia mwenyekiti wake arudishe kiwanda!! Last time i checked chama chake ndio kinaunda serikali
 
Hatimaye nape nnauye ajipandisha cheo na kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum
 
Back
Top Bottom