Napata utata kuielewa ibara 54(5) ya Katiba ya Tanzania.

Nenetwa

Member
Jan 16, 2011
14
0
Ndugu zangu naomba msome ibara hii niliyoinukuu kutoka kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Angalieni ibara ya 54(5) na mnisaidie kuielewa,hainiingii akilini.

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
Baraza la Mawaziri na Serikali
Baraza la
Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
Sheria Na.4
ya 1992 ib…
Sheria Na.34
ya 1994 ibara
12
54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe
wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye
atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi
mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili
Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya
Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha
kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji
wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na
litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote
litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo
maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.
(4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote
ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa
mikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika
mikutano hiyo.
(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa
na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.”


Utata unakuja hapa:-
Je,Mkataba wa Dowans-Richmond ulijadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri?
Kama jibu ni Ndiyo, Je ulikuwa ni ushauri wa Baraza la Mawaziri kwa Rais?
Kama jibu ni Ndiyo, Je Rais alikubali kwa hiari yake kwa mujibu wa masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama jibu ni ndiyo, Je Mkataba huu ni halali?
Kama jibu ni hapana, Je tutashitaki kwa nani ili hali imeandikwa katika ibara ya 54(5) kuwa ''Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa
na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.”

Jamani hiki si kiini macho? Au yawezekana hawa Richmond-Dowans walishazisoma sheria zetu wakaona udhaifu na sasa wanatuadhibu kwa kutunyonya bara-bara kwa kujua hatuna pa kushtaki? na kwamba hata tukishtaki, jambo hilo halitachunguzwa katika mahakama yoyote?
Au yawezekana tunamtafuta mbaya wetu ili hali mbaya wetu ni Sheria zetu wenyewe?
Kweli napata utata, naombeni ufafanuzi!
Maoni yangu: KAMA NA NINYI NDUGU ZANGU MTAPATA UTATA, BASI MABADILIKO YA KUPATA KATIBA MPYA NI YA LAZIMA!

Chanzo:KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977
(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977,
limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba
ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000).
 
Naona kila sehemu wanaogopwa kuchunguzwa... kama hawana chochote cha kuficha...yaani ni watu wa kweli katika kuyafanya yote kwa ajiri ya mustakabali wa Tanzania.. Kwanini wanaogopwa kuchunguzwa?

Ina maana hata wakimpa illegal advise yeye atauchukua tu na hakuna wa kuwauliza... hii inamaanisha kwamba wote walioshiriki au wanaoshiriki kumshauri raisi ni vihiyo wanaogopa uchunguzi wa uozo wao na kama hawaogopi wasimame mmoja baada ye mwingine wahesabiwe kwa maovu yao tuonane nani aliye msafi kama sio wote waliovunda...
 
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.

Naona jibu liko kwenye ibara ndogo ya tatu, suala la Dowans haliangukii katika mambo ya utekelezaji wa madaraka ya rais kwa mujibu wa katiba.

Suala la Dowans halijawahi kwenda kwenye baraza la mawaziri hivyo kifungu kidogo cha tano hakiwezi kutumika hata kidogo.
 
Ndio maana wanataka kulileta kwenye baraza la mawaziri kwa sababu kwanza.. mawaziri walikula kiapo cha ziada kinachosema "na sitatoa siri za baraza la mawaziri". Ndio maana kina Mwakyembe na Sitta wamewahi kutoa maoni yao kuhusu Dowans kabla suala hilo halijaletwa kwenye baraza hilo kwani likiletwa na wao wanafungwa.

Sasa uzuri ni kuwa mtu halazimishi kuishi na siri ya ufisadi. Baraza la Mawaziri likihalalisha uvunjaji wa sheria na ikajulikana wamefanay hivyo kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inaweza kupigwa na waziri mkuu akajiuzulu na baraza kuvunjika au kama ni suala nyeti sana (siamini kama Dowans ni nyeti kihivyo) basi Bunge linaanzisha mchakato wa kumshtaki Rais ambapo akishashtakiwa atatakiwa akae pembeni hadi hukumu itakapotolewa.

Lakini kwa wale ambao hawakubaliani na mashauri au maamuzi ya baraza la Mawaziri watatakiwa kujiuzulu. Mrema alifanya hivyo baada ya kutokubaliana na maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuficha ufisadi uliotokea na malipo ya bilioni 900???
 
Katiba hii haikuwa kwa ajili ya wananchi, ilikuwa kwa ajili yao, so kwa hali iliyopo ni kuwa bare witness tu kama Martin Luther alivyowahi sema. Cha msingi ni kudai katiba itakayokuwa kwa ajili ya wananchi na itakayotokana na maelekazo yao.
 
Sasa uzuri ni kuwa mtu halazimishi kuishi na siri ya ufisadi. Baraza la Mawaziri likihalalisha uvunjaji wa sheria na ikajulikana wamefanay hivyo kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inaweza kupigwa na waziri mkuu akajiuzulu na baraza kuvunjika au kama ni suala nyeti sana (siamini kama Dowans ni nyeti kihivyo) basi Bunge linaanzisha mchakato wa kumshtaki Rais ambapo akishashtakiwa atatakiwa akae pembeni hadi hukumu itakapotolewa.

..mzee Mwanakijiji uko serious!!!!!??? Au ndio wamemuweka mama Makinda na upande wa MAHAKAMA KUU jaji mkuu Chande????!!!!!
 
Hii ndiyo katiba iliyotufikisha tulipo..ndivyo ilivyomaanisha! Hiki na vifungu vingine ndivyo tunataka viangaliwe kwa umakini kwenye katiba mpya(km wenye nchi wataridhia) maana wamewekeza hisa zao katika taifa hili kwa hiyo kuhoji katiba mpya ni kuingilia ulaji wa wakubwa!...ni maono tu!
 
Mchakato wa katiba mpya uanze mara moja, ili tuondokane na huu uozo, hata shetani hauelewi kabisa, ni wachumia tumbo wetu tu ndo wanaufagilia.
 
Sio katiba mpya tu...mchakato mzima uwe huru na wazi ikiwa ni pamoja na kuhusisha wanasheria na wadau tofauti tofauti kutoka kwenye maeneo tofauti kijamii ili kuepuka vifungu/vipengele vinavyompa kiongozi wa umma mamlaka makubwa yanayopelekea kutoa maamuzi ya hovyo hovyo...baada ya kutengeneza draft ya kwanza iwekwe wazi,tuwaambie hiki ondoa,pale tunataka hivi...wakaadraft tena na tena kabla ya kuwaambia hiki ndicho tunachotaka..ndicho tulichowatuma!
 
Back
Top Bottom