Naombeni ushauri kuhusu kozi ya Mining Engineering

Engager

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
1,273
2,648
Ndugu zangu wana JF, hebu tushauriane. Hivi ukiwa Mining engineer tofauti na mgodini kunasehem gani tena unaweza kuajiliwa? Coz kuna mdogo wangu amehtm Form 6 mwaka jana (PCM, matokeo mazuri ila hakuaply na anafanya hvyo mwaka huu). Anaonekana kupendele ksoma mining engineering. Mi nataka nimshauri aachane nayo maana naona kma hailipi kwa sasa. Nyinyi mnanishauri vipi? Tusaidiane jamani
 
Kama kweli ni kazi anayoipenda muache akasome tu...ukweli wa mambo ni kwamba mining industry, worldwide ina uhaba mkubwa sana wa qualified/skillled worked force. Na kwa bara letu la Africa, mining is set to grow further as a result of minerals demand, in particularly Tanzania. Kama issue ni kazi tu sioni kama hilo ni wazo zuri...kwa mtazamo wangu, pengine umsaidie toka mapema kuweza kufanya link ya kitu anachotaka kusomea na namna ya kufanya biashara yeye mwenyewe katika eneo hilo. Tujiulize, ni kwanini mining contractors karibu wote wanatoka nje ya Tanzania?? Can't we do it?
 
Unachosema kaka ni kweli kabisa. Lakn inasemekana eti mining engineers wamekuwa wengi sana kias employment oppotunities zinakua haba kwa wenye profesion hiyo kadri miaka inavyo enda ukiachilia mbali Geology. How do you comment on
 
Kipenda roho, nashukuru wachangiaji hapo juu wametoa mawazo sahihi, ajira zipo kwa wenye uwezo, na nina hakika kama ndo fani anayo ipenda ataiweza na atapata furaha maishani mwake.
 
Mkuu hiyo Mining aiache kabisa sahv ajira zake zinasumbua sana maana watu mtaani ni wengi kulinganisha na migodi iliyopo na mara nyingi kazi ni migodini tu,
nakushauri kama anataka engineering achukue Mechanical,electrical, civil au chemical hizi kujiajiri ni rahisi pia ajira ni nyingi
 
du! Mi ndo kwanza naingia mwaka wa pili sijui itakuwaje mbeleni
 
Mwache asome hiyo hiyo mining engineer. Ni pana kuliko unavyoichukulia wewe. Inainclude peer construction industry. Anaweza kuja kuanzisha mgodi hata wa kuchimba madini ya viwandani kama kokoto za granite. Hivi unajua sasa hivi kiwanda cha Dangote Mtwara wanatoa kokoto hapo junction ya kwenda Tanga? Mwache asome anachopenda na atakuwa mbunifu huko.
 
asante kwa ushauri!
 
Tanzania yazindua Mgodi
rasmi wa madini

Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mgodi wake
wa kwanza utakaowaajiri wafanyakazi wazawa tu
kuanzia ngazi za uongozi hadi chini.
Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi
za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira
miongoni mwa watanzania.Aidha waziri wa nishati
na madini nchini humo Sospeter Muhongo
amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo
utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia
nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza
Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni
wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo .
Saumu Mwasimba amezungumza nae mchana huu
na kutupa maelezo kamili kuhusu mgodi huo na
hatua hiyo ya serikali. Kuskiliza mazungumzo hayo
bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Saumu Yusuf
 
Hiyo taarifa nimeisikia na ni nzuri ktk kutatua tatizo la ajira nchini, ila tuombe mambo ya kujuana yasichukue nafasi kwenye hiyo migodi
 
Back
Top Bottom