Naombeni mnipe ushauri kuhusu Viwanja nya Kigamboni

subz3r0

Member
Dec 7, 2011
13
0
Habari zenu, nilikuwa nawaombeni mnisaidie kunipa ushauri kuhusu viwanja vya kigamboni (Mjimwema) nataka kununua kiwanja huko. Lakini nafikiria hiyo kigamboni new city project ipo kwenye mjimwema. sio ninunue halafu nije kuambiwa hapo wanavunja vunja sasa hameni nendeni sehemu nyingine.

Je hapo mtanisaidia je? kwa yoyote yule aliye naejua kuhusu hilo naomba atoe maoni yake, itanisaidia sana mie.
 
wala hamna shida maeneo karibia yote ya kigamboni yamepimwa na yana offer kwa iyo nunua kiwanja chenye offer au title deed!!! kwa iyo huwez uziwa kanyanga maana serikali haito offer au title kwa maeneo yaliyoandaliwa kwa shuhuli zisizo za makazi
 
Mhh mjimwema hapajapimwa.sehemu zilizopimwa ni kibada ya kushoto na kulia ni kule mbele kama unaelekea mikwambe hadi toangoma, zaidi ni geza, ungindoni na ukitaka maeneo ya kijaka, mwasonga unaweza nunua na ukapimiwa sa ruhusa imetoka na watu wanapimiwa ila uwe makini maana unaweza uziwa eneo la mtu ama jeshi. mjimwema kuja feri ni kibada ya kulia kuanzia stendi haina muamala labda kama watapima wakishawalipa fidia wanaotoka.
Zaidi nenda ardhi wizarani au manispaa ya temeke wakujuze vema
 
Back
Top Bottom