TabletFellow
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 918
- 272
mkuu hapa watu hawako siriasAaaah, Police marufuku kuishiwa. maana wakiishiwa hawa jamaa raia ndo tutakayekoma. Watakuwa wanaangalia tu nyumba wanayoona ina unafuu wanavamia wanasema unahisiwa jambazi. Unakaa ndani kama siku tatu hivi hadi ukung'ute hela yote uliyonayo. watakuwa wanamkamata yeyote aliyevaa vizuri humo njiani ili awape chochote. Watatuomba lunch kwa sana, halafu tukikataa tutatishiwa kusingiziwa makosa. Watawatuma vibaka wakusanye simu zetu ili hela wagawane. Haya yanafanywa na polisi hivi sasa ambapo wana unafuu wa maisha, je wakiishiwa?
Wanafunzi pia wasipate ziro, manake wakipata ziro hatutafaidika chochote zaidi ya kuwa na kizazi cha wajinga. Walimu waishiwe, ilii wagome lakini watoto wetu tunataka wafaulu. Na ukumbuke kwamba ukiombea watoto wafeli, basi watakaofeli ni watoto wa walala hoi na si watoto wa walala hai. Maana ni watoto wa walala hoi ndio wanaosoma kwenye shule ambazo mwalimu wake analipwa na serikali.
Lakini zaidi ya yote, ninyi ni kuku tu, tangu lini dua lenu likampata mwewe. Endeleeni tu kuomba hizo dua na katu hazitakaa zitokee na wala hayo mapinduzi hayatatokea kwa kutegemea hizo bahati nasibu. Cha msingi kila mmoja mahali pake kama anaona anapunjwa au anaonewa kwa namna yoyote ile basi achukue hatua. Ili mapambano yaanze na si kusubiri eti yatokee mabaya zaidi. Maana nayo yana kero zake.
ni kupunguza presha za maisha tu