Naombeni ushauri jaman!mimi na mchumba wangu(hatujafunga ndoa) tumefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume!lakini tangu hapo kumekuwa na malumbano makubwa sana kiasi kwamba hadi sasa hivi mawasiliano ni hafifu.na mara nyingi nikiwa nahitaji pesa ya matumizi,inachukua mda kunipatia na nikisema nimkumbushe ananijibu anakumbuka lakini hajali shida yangu ya haraka.nikiwa namuhitaji anadai anafanya biashara yuko busy na hata akija hawezi akakaa zaidi ya mwezi,nikimtumia sms nzuri za mapenzi mwenzangu anapotezea,mara hajibu!kiukweli napata shida sana kiasi kwamba mimi mwenyewe nashawishika kutafuta mtu wa kuniliwaza ili nisiwe na mawazo zaidi!inshort yani mme wangu yupo busy zaidi na kazi kuliko familia!kwani hatuishi pamoja!mimi nipo kikazi Dodoma yeye yupo Mwanza na nikirudi nalazimika kwenda nyumbani kwetu,mana yeye hataki nikaishi kwake hadi tufunge ndoa!NAOMBENI USHAURI WAPENDWA NIFANYAJE?