Naomba ushauri wana jamii forum

Wacha watu wakushauri lakini wasikuamulie. Mapenzi huisha yakabaki mazoea kwa hivyo huyu joe anataka mapenzi na maskini hajui kuyalea. Kama huja zaa naye mtoto chunga asikupe ulezi alafu akutimue alafu alete visababu vyakua we ni catholic naye ni muABC
 
Unajua sisi binadamu tunaona yanayoonekana kwa MACHO yetu tu..bali yasiyoonekana hayo ni ya MUNGU!
Kukushauri kuhs hii mada yako..labda niseme tu kuwa..USIKILIZE moyo wako na jaribu kujiwekea vigezo vyako ili umpime kwa hivyo..kama walau kwa asilimia kubwa atafit basi chukuaneni..Lakini hii habari ya kusema..'mbona kamuacha flan na wewe atakuacha'..hizi ni swaga tu!!..mbona kuachana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida tu!!!

Asante kwa ushauri wako Snowball..............
 
dada sugua goti.kila mtu na bahati yake. yawezekana huyo ni wako ndo mana kazunguka kote huko lakin bdo karud kwako! all da best mdada. . . .

yana kama ulikuwa unajua hata mimi ninafikiria hilo, kwanini azunguke kote huko kisha arudi kwangu tu. ukizingatia kuwa yupo mbali mimi nipo Lindi yeye yupo DSM lakini karudi kwangu.. N-way naendelea kuomba huenda ndo akawa ndiye niliyepangiwa.
 
Wacha watu wakushauri lakini wasikuamulie. Mapenzi huisha yakabaki mazoea kwa hivyo huyu joe anataka mapenzi na maskini hajui kuyalea. Kama huja zaa naye mtoto chunga asikupe ulezi alafu akutimue alafu alete visababu vyakua we ni catholic naye ni muABC

asante kwa ushauri
 
wengi wanakushauri rudiana nae,hali kadhalika mimi pia....ila this time kuwa makini sana dada yng.otherwise wishing you all the best ktk mahusiano yenu mapya.
 
Kwa ushauri wangu mkubalie muchunguze ikiwezekana mfunge ndoa mwenzako huenda ameshateseka sana ndo maana ameamua kurud kwako mpe nafasi ya mwisho.
 
Jiandae kusumbuka....
Hapo keshajigundua kabisa kwamba yeye mwenyewe ni mzigo..na ameona wewe ndo unaweza kumbeba (na hapa ndipo inapokuja hiyo mantiki yako kwamba kazunguka kote hatimae amerudi kwako)!!

If I were you..
Ningejipiga stop kudeal na hivyo vitu nikastick kwenye mambo mengine binafsi......hii ingenisaidia kutulia na kuobserve the reality na si kufanya maamuzi kwa kudhani. This is due to the fact that;

1. Mtu mwenyewe haukumfahamu kabla zaidi ya kukutana kwenye basi....so huna uhakika sana na sababu za yeye kuachana na mpenzi wake wa awali waliyezaa mtoto, pengine ni factors zaidi ya kigezo cha dini.
2.Mpaka sasa uzipatazo ni stori kuwa mke waliachana tena ndiye mkorofi. Je, una uhakika gani kama sio matatizo ya huyo mwanaume mwenyewe??

Mwisho nakuonya, usiingie kwenye ndoa kwa matumaini eti kisa tu wamjua na aliwahi kuwa wako.....eti na sasa amerudi tena kwako, itakugharimu!
 
Story nzuri nimeipenda na kwabahati nzuri hujadanganya kama walivyo wengi. Kwaupande wangu nimeona kuwa mapenzi yenu ww na joe ni natural japo kuna modification kathaa maranyingi mapenzi ya namna hii yanadumu kwa muda mrefu kinachoonekana ni kwamba umbali kati yenu ndio chanzo. sasa inabidi uhakikishe kuwa huko tena mbali nae na mkapime ww na yeye na kama hakuna mwenye tatizo basi kwamoyo mkunjufu mkubalie kwani mapenzi ktk dunia ni zawadi ambayo haijirudii kamwe hivyo kama unampenda kweli mpe mkubalie
nawatakia kila la heri kama mtafanikiwa kufunga ndoa basi na idumu miaka mingi na Mungu awachukue mkiwa kitandani(wazee sana)
 
Ilikuwa ni mwaka 2005 nilipokuwa nasafiri toka Mtwara kuja Lindi, (mtwara ndio nyumbani na Lindi ni kituo cha kazi) ndani ya basi nilikaa kiti kimoja na mkaka mtanashati.. tulisalimiana na kila mtu akachukua hamsini zake… safari iliendelea lakini kwa bahati mbaya gari tulilokuwa tumepanda lilipata tatizo tuteremka na kusubiri matengenezo, ndipo nilipoanza kufahamiana na jirani yangu niliyekuwa nimekaa naye. Alijitambulisha kwa jina na Joe, nikajitambulisha naitwa Emecka. Tukaanza kupiga stori za hapa na pale, Lahaula kumbe Joe anaifahamua familia yangu na mimi nilikuwa naifahamu familia yake ila sisi wenyewe hatukuwa tunafahamiana kwani yeye anaishia Dar es salaam na mimi nilitoka Mtwara miaka mingi iliyopita kwa hivyo hatukuwahi kufahamiana ila Joe alisoma na baadhi ya dada zangu (watoto wa baba mdogo).

Alinieleza short history ya maisha yake kwamba aliwahi kuzaa na mwanamke ila kwa vile Yule mwanamke alikuwa muislamu hawakuweza kufunga ndoa kwani wazazi wa Yule mwanamke hawakutaka binti yao abadili dini kwa hivyo aliachana na yule mwanamke ila walikuwa wamezaa mtoto mmoja… Gari lilitengemaa tuaendelea na safari, tukiwa tunapiga story zaidi na zaidi. Tulifika Lindi kwenye saa 02 za usiku, Joe alinisindikiza mpaka kwa dada yangu ambako ndio nilikuwa ninaishi kwa kipindi kile then akarudi kaw mdogo wake alipokuwa amefikia. Tuliandelea kuwasialiana kwa muda wa wiki moja ambapo Joe alikuwa bado yupo Lindi ghafla tulianza kupendana na na baada ya muda tukawa wapenzi. Joe alirudi zake DSM na mimi niliendela na kazi hapa Lindi, kuna wakati nilikuwa nakwenda DSM kumsalimia Joe, nilikuwa nafikia kwake kwani alikuwa anaishi yeye, mwanaye na housegirl.. nilikuwa free kwa chochote kile.. Tulidumu kwa muda wa mwaka 1 hivi baadaye mawasiliano yakapungua na mwishowe yakaisha,”kama mnavyojuwa mapenzi ya mbali” tukajikuta tumeachana automatically na kubaki kuwasialiana mara chache sana mwishowe tukapoteza mawasiliano kabisa..

mwaka 2008 nikakutana na mdogo wake Joe akanieleza kuwa joe kafunga Ndoa na mjukuu kwa kigogo mmoja hivi wa CCM mwenyeji wa Tanga, basi sikutaka kuchukua mawasialiano, nilisema tu hongera zake na kuendelea na misha yangu. Mwaka 2011 mwishoni alikuja mdogo wake na Joe akitaka kuzungumza na mimi, nilikubalia wito wake tulikaa mahali flani tukazungumza mambo mengi, ila kikubwa ni ujumbe kutoka kwa Joe akiomba msamaha kwa kukatisha mawasiliano, na anaomba namba yangu ya simu ili awasiliane na mimi, nikamuuliza kwani si ana mke anataka nini kwangu tena?
Basi ndo mdogo wake Joe akanisimulia visa vya Yule mke.. kuwa ni mkorofi na wameshindwana na ameshaomba talaka na kesi ipo mahakamani… nilimpa namba yangu kwa shingo upande na kwa masharti kwamba mimi nina mchumba (ingawa nilikuwa na mpenzi ila hatukuwa na makubaliano ya kuonana) kama anataka kuwa na mimi tena hiyo nafasi haipo tena. Basi Joe alinipigia kila mara kutaka maendeleo yangu na mchumbaangu…

nilimpiga tarehe ila hakukata tama akasema nitatakata tama siku nikisikia umefunga ndoa ndo utakuwa mwisho wangu wa kukusumbua.
Basi tuliwasiliana na mwisho wa siku Joe alifunga safari kutoka DSM na kuja Lindi kutaka kuzunguma na mimi kuhusu ndoa kati yangu mimi naye. Kwa bahati mbaya au nzuri alifika wakati niliokuwa nimeachana na Yule mpenzi wangu kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Nilijikuta naanza kurudisha upendo kwa Joe. Niliomba ushauri kwa ndugu zangu wakanieleza kama aliweza kuachana na mkewe wa ndoa atawezaje kuishi na mimi bila kuachana? Naomba ushauri jamani nipo njia panda katka kutoa maamuzi ya kukubali kufunga ndoa na Joe.. Samahani sana kwa kuwachosha..
Dhambi za huyu bwana zimeanzia hapo kutokana na ubaguzi.
 
jamaa anaoa then mambo yanatokea badala asolve anatafuta mwingine wa kuoa then matatizo yatokee afu aoe mwingine.....na wew utaolewa,ataona kuna mambo na matatizo yanakuja atakuacha ataoa mwingine...akili zako changanya na za mbayuwayu...

ategemee kombora huyo jamaa hana msimamo,hakuna mtu mkamilifu
 
Jiandae kusumbuka....
Hapo keshajigundua kabisa kwamba yeye mwenyewe ni mzigo..na ameona wewe ndo unaweza kumbeba (na hapa ndipo inapokuja hiyo mantiki yako kwamba kazunguka kote hatimae amerudi kwako)!!

If I were you..
Ningejipiga stop kudeal na hivyo vitu nikastick kwenye mambo mengine binafsi......hii ingenisaidia kutulia na kuobserve the reality na si kufanya maamuzi kwa kudhani. This is due to the fact that;

1. Mtu mwenyewe haukumfahamu kabla zaidi ya kukutana kwenye basi....so huna uhakika sana na sababu za yeye kuachana na mpenzi wake wa awali waliyezaa mtoto, pengine ni factors zaidi ya kigezo cha dini.
2.Mpaka sasa uzipatazo ni stori kuwa mke waliachana tena ndiye mkorofi. Je, una uhakika gani kama sio matatizo ya huyo mwanaume mwenyewe??

Mwisho nakuonya, usiingie kwenye ndoa kwa matumaini eti kisa tu wamjua na aliwahi kuwa wako.....eti na sasa amerudi tena kwako, itakugharimu!

Kipipi hivi Adam na Hawa walifahamiana muda gani kabla ya kuoana? Kwenye mapenzi hakuna formula kama za hisabati. Love can start from nowhere and last for 50+ years!
 
Du kweli ile nadharia ya uhaba wa wanaume wa kuoa kumbe kuna wanawake wanaitumia barabara.mmmmmmmmmmh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom