Naomba ushauri wako nasaha juu ya kufikia malengo ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka mmoja na miezi sita

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
3,590
8,476
Mimi binafsi nahitaji nianze ufugaji wa kuku chotara, ambao wanataga na kuatamia, pamoja na kuku wakienyeji. Ingawa Kuna Comment ya mkuu Kalamu niliwahi isoma hapa jukwaani akiisema kuku wakienyeji hawalipi na wafugaji wengi wanafuga ufugaji wa bila faida hasa wa mazoea.

Sasa siku za hivi karibuni naona wafugaji wengine wanafakiwa kuuza kuku mmoja bei ya elfu 30 Jogoo, na jike wanauza elfu 25. Baada yakufanya utafiti kidogo nimeamua ni fanye ufugaji na target yangu ni kuku 5000, kufikia December 2025. Mpaka Sasa nakuku wanane tu, wawili wa kienyeji, sasso 5 na kroila 1. Nimeanza kuku wachache Hawa nikiwa nikiwa naandaa mabanda yakamilike ndio niongenze kuku wengine.

Je Kwa maono yenu wazoefu wa ufugaji kuku, kufuga kuku mchanganyiko wa kienyeji pure, sasso, kuchi, kroila pamoja na Mbegu nyinginezo inaleta tija?.

Je ushauri wenu ni nini juu ya Mimi kufikia target ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka 1 na miez 6?.

Sina uzoefu wowote katika ufugaji, lakini nategemea kuwaweka vijana wakike wawili ambao wao niwazoefu katika uangalizi wakuku na ntakua nawalipa kiasi Cha pesa kulingana na makubaliano yangu na wao.

Mabanda yapo mawili Kila Moja nalijenga sehemu tofautina yako mwishoni ili niweze kujua yupi anafanya kazi nzuri ili niongenze nguvu Kwa muangalizi mzuri zaidi.

Budget yangu ni 462,000/= Tzsh. Kwa Kila mwezi ndani ya miezi sita yakwanza, hii nipamoja nakunnua chakula pamoja na kuku wakubwa, vifaranga na chakula bila kusahu dawa na chanjo zake.

Hii 462,000 Tzsh, ninje na makubaliano ya mishahara yao.

Mpango wangu nikuku watakatakapofika 1500/2000 nisinunue kuku yeyote bali wazaliane wao Kwa wao tu.

Nimepanga kuwalipa Kila muangalizi shilling elfu 70 Kila baada ya week 2, nikiwa namaana tare 16 ntawalipa elfu 70 Kila mmoja na tare 2 ntawalipa elfu 70 Kila mmoja, hii iweze kuwasaidia wao katika suala la matumizi binafsi madogo madogo. Pia Kila mtu atakua anakaa mahala hapo kwenye Banda husika, ingawa Mimi Niko mbali kidogo na Banda husika lakini nikihitaji kufika naweza kufika ndani muda mchache usiozidi nusu saa.

Nilikua naomba ushauri wenu juu ya mradi wangu huu, kuhusu masoko ya kuwauza nimepanga hapo baadae kufungua butcha za kuuza nyama za kuku , hizi butcha nimepanga kuzifungulia Dar es Salaam Kwa hapo baadae hasa 2026 kwahio ntaweza kuuza jumla na reja reja, pia ntahitaji kununua kuku wengine kutoka Kwa wafugaji wenzangu kadri soko la wanunuzi wa jumla wakuku litakavyoongezeka.

Mradi wangu naufanyia Tanga mjini wa ufugaji, maana ndipo nimeona aridhi inanunulika Kwa bei rahisi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam.

Nimeambatanisha Banda langu mojawapo nalolimalizia pamoja na picha kuku za kuku wangu 3.

Naamini haitokua rahisi kufikia kuku elfu 5, lakini naamini pia haishindikani kufikia malengo.

Asante wakuuu wangu na karibu niweze pata mchango na mawazo yenu kama hamtojali.
 
Attachments

  • IMG_20230423_170804_050.jpg
    IMG_20230423_170804_050.jpg
    1.4 MB · Views: 93
  • IMG_20230423_091836_881.jpg
    IMG_20230423_091836_881.jpg
    2 MB · Views: 81
  • IMG_20230423_170942_261.jpg
    IMG_20230423_170942_261.jpg
    2.4 MB · Views: 71
We jamaa,una ndoto nzuri,ila nikuambie huwezi kufuga kuku chotara na kienyeji kwa idadi hiyo unayotaka bila kuwa na eneo kubwa kwa kifupi Shamba.Tena lisipungue heka 3.

Kufuga kuku Chotara na kienyeji utegemee kuwalisha kwa chakula cha dukani kwa muda wote ni hasara.Ni hasara kwa sababu hawakui kwa haraka kama broiler,

Na kwa vile unataka kuwafugia kwenye mabanda maana yake lazima uwanunulie chakula cha dukani kila mara

Shamba ni la nini?

Shamba hilo litakusaidia wewe kupunguza gharama za ulishaji kwa wewe kulima mazao ya kuwalisha kuku wako,.Mazao kama Mahindi,mtama uwele na Alizeti.Na pia utapanda majani na kutengeneza Azola pia Funza kwa ajili ya protein,

Pia Shamba hilo hilo litatumika kuwaachia kuku wako free waokote chakula mashambani kuliko kuwafungia ndani muda wote.

Kumbuka kuwa kwa idadi hiyo ya hao kuku maana yake utahitaji eneo la kutupia mbolea.So ukiwa na Shamba maana yake hutapata shida kwa kuhifadhi mbolea,na utalima bustani.

Cha mwisho hakikisha unaajiri Daktari wako kwa ajili ya kuwaangalia hao kuku kila siku
 
ufugaji kwa 100% unakuhitaji wewe mwekezaji uwe sehemu ya mradi. tofauti na hapo jiandae kulilia chooni
Mkuu nashukuru Kwa mawazo yako, Mimi bahati mbaya au nzuri kazi yangu nafanya masaa 16 nayo ni kusimamia watu nakufatilia mahesabu nakufatilia mahesabu kadha wa kadha, lakini uwepo wangu eneo la mradi nikama vile nipo na muda wowote naweza nikafika, jambo lingine hakuna mtu anaweza kufanya Kila jambo yeye mwenyewe Kwa 100% na ukisema ufanye hivyo basi tegemea kutopiga hatua kubwa .

Mpaka Sasa nabiashara 3 najitahid niongenze ya 4 ambayo niufugaji je ntaweza jigawa vipi kuwepo Kila eneo Kwa muda wote?.

Jambo kubwa ambalo nalitumia nikufanya ukaguzi Kila baada ya miezi 4 nahili ndio limenisaidia.
 
Kila la kheri boss kijana hakika utafika mbali.....

Hapo la muhimu sana kuliko yote ni kupata watu smart na sahihi wa kusimamia huo mradi full time...........
Yeah mkuu wangu, nahawa mabinti niliowachgua walikua wanafanya kazi mahala Kila mmoja alikua analipwa elfu 80 Kwa mwezi, lakini Mimi nawapa makazi,pamoja na umeme na maji then nawalipa laki Moja na 40 Kwa mwezi. Pia nahitaji niwe nawapeleka kwenye semina mbali mbali, mradi utakapokua mkubwa nao ntakua nawaboreshea maslahi.
 
We jamaa,una ndoto nzuri,ila nikuambie huwezi kufuga kuku chotara na kienyeji kwa idadi hiyo unayotaka bila kuwa na eneo kubwa kwa kifupi Shamba.Tena lisipungue heka 3.

Kufuga kuku Chotara na kienyeji utegemee kuwalisha kwa chakula cha dukani kwa muda wote ni hasara.Ni hasara kwa sababu hawakui kwa haraka kama broiler,

Na kwa vile unataka kuwafugia kwenye mabanda maana yake lazima uwanunulie chakula cha dukani kila mara

Shamba ni la nini?

Shamba hilo litakusaidia wewe kupunguza gharama za ulishaji kwa wewe kulima mazao ya kuwalisha kuku wako,.Mazao kama Mahindi,mtama uwele na Alizeti.Na pia utapanda majani na kutengeneza Azola pia Funza kwa ajili ya protein,

Pia Shamba hilo hilo litatumika kuwaachia kuku wako free waokote chakula mashambani kuliko kuwafungia ndani muda wote.

Kumbuka kuwa kwa idadi hiyo ya hao kuku maana yake utahitaji eneo la kutupia mbolea.So ukiwa na Shamba maana yake hutapata shida kwa kuhifadhi mbolea,na utalima bustani.

Cha mwisho hakikisha unaajiri Daktari wako kwa ajili ya kuwaangalia hao kuku kila siku
Mkuu nashukuru Kwa mawazo yako na u abarikiwe Sana, ntajitahid mradi utakapokua unakua mkubwa nitafute eneo kubwa zaidi. Lakini hawa kuku elfu 5 Kwa malengo yangu nahitaji wawe sehemu mbili tofauti, yaani sehemu Moja kuku 2500, na sehemu nyingine kuku 2500. Nimejaribu kimtembelea nfugaji mmoja yeye anakuku kama 200 lakini pia ana mabanda kama 5 madogomadogo nae anafuga chotara, kwamantiki hio nilihitaji namna kuku wanavyoongezeka na Mimi niwe naboresha miundombinu yao.

Pia kama watakua wengi kufikia kuku elfu 2 basi ntanunua mashamba MUHEZA Kwa ajili ya kukuza mradi zaidi. Lakini mabanda nayojenga Sasa nataka yatumike kuangalia changamoto zilizopo nantakapoona mradi unakua Kwa matarajio yangu na mimi niongenze nguvu zaidi.

Kuhusu kulima bado sijaamua kulima, lakini mbolea mahala pakuipeleka tayali nimeshapapata na nikwawakulima wa mbohamboga Kuna baadhi ya makubaliano nimeingia nao baadhi.

Kuhusu kumuajiri daktari niwazo zuri lakini mtaji Kwa Sasa haujaruhusu, lakini mbeleni kama mambo yataenda Kwa namna navyotaka basi ntamtafuta.

Pia kuhusu kuwanunulia chakula Cha dukani ntanunulia vifaranga tu, watakapotimiza miezi 2 watakula chakula ambacho ntakuwa nachanganya mwenyewe.

Asante mkuu wangu Kwa mchango wako Muhimu na bora, ubarikiwe kiongozi.
 
Kabla hujaendelea kuwaza hicho ulichopanga, hebu anza kuraise kuku wa kienyeji 300 tu, baada ya miezi sita utafuta ndoto yako.
Mkuu kuku wakienyeji nafahamu changamoto zao kiasi ndio maana nimesema nimchanganyiko wa kuku wakienyeji pamoja na chotara. Nafahamu ningumu lakini haishindani mkuu wangu kufikia ijumanne ntakua nimemaliza Banda lakwanza, Kisha kadri muda utakavyoenda ntakua naleta mrejesho.
 
Heshima yenu wakuu
Umri wangu ni miaka 28/32, Sina mtoto wala mke na biashara kadhaa kama 3 tofauti na pia najilipa mshahara wa Mil 1.8 per month kama Gross huu nikwaajili ya matumizi yangu binafsi nakufanya saving Kwa ajili ya kuanzishia biashara mpya Sasa nimeamua niingie katika ufugaji wa kuku.

Mimi binafsi nahitaji nianze ufugaji wa kuku chotara, ambao wanataga na kuatamia, pamoja na kuku wakienyeji. Ingawa Kuna Comment ya mkuu Kalamu niliwahi isoma hapa jukwaani akiisema kuku wakienyeji hawalipi na wafugaji wengi wanafuga ufugaji wa bila faida hasa wa mazoea.

Sasa siku za hivi karibuni naona wafugaji wengine wanafakiwa kuuza kuku mmoja bei ya elfu 30 Jogoo, na jike wanauza elfu 25. Baada yakufanya utafiti kidogo nimeamua ni fanye ufugaji na target yangu ni kuku 5000, kufikia December 2025. Mpaka Sasa nakuku wanane tu, wawili wa kienyeji, sasso 5 na kroila 1. Nimeanza kuku wachache Hawa nikiwa nikiwa naandaa mabanda yakamilike ndio niongenze kuku wengine.

Je Kwa maono yenu wazoefu wa ufugaji kuku, kufuga kuku mchanganyiko wa kienyeji pure, sasso, kuchi, kroila pamoja na Mbegu nyinginezo inaleta tija?.

Je ushauri wenu ni nini juu ya Mimi kufikia target ya kuku elfu 5 ndani ya mwaka 1 na miez 6?.

Sina uzoefu wowote katika ufugaji, lakini nategemea kuwaweka vijana wakike wawili ambao wao niwazoefu katika uangalizi wakuku na ntakua nawalipa kiasi Cha pesa kulingana na makubaliano yangu na wao.

Mabanda yapo mawili Kila Moja nalijenga sehemu tofautina yako mwishoni ili niweze kujua yupi anafanya kazi nzuri ili niongenze nguvu Kwa muangalizi mzuri zaidi.

Budget yangu ni 462,000/= Tzsh. Kwa Kila mwezi ndani ya miezi sita yakwanza, hii nipamoja nakunnua chakula pamoja na kuku wakubwa, vifaranga na chakula bila kusahu dawa na chanjo zake.

Hii 462,000 Tzsh, ninje na makubaliano ya mishahara yao.

Mpango wangu nikuku watakatakapofika 1500/2000 nisinunue kuku yeyote bali wazaliane wao Kwa wao tu.

Nimepanga kuwalipa Kila muangalizi shilling elfu 70 Kila baada ya week 2, nikiwa namaana tare 16 ntawalipa elfu 70 Kila mmoja na tare 2 ntawalipa elfu 70 Kila mmoja, hii iweze kuwasaidia wao katika suala la matumizi binafsi madogo madogo. Pia Kila mtu atakua anakaa mahala hapo kwenye Banda husika, ingawa Mimi Niko mbali kidogo na Banda husika lakini nikihitaji kufika naweza kufika ndani muda mchache usiozidi nusu saa.

Nilikua naomba ushauri wenu juu ya mradi wangu huu, kuhusu masoko ya kuwauza nimepanga hapo baadae kufungua butcha za kuuza nyama za kuku , hizi butcha nimepanga kuzifungulia Dar es Salaam Kwa hapo baadae hasa 2026 kwahio ntaweza kuuza jumla na reja reja, pia ntahitaji kununua kuku wengine kutoka Kwa wafugaji wenzangu kadri soko la wanunuzi wa jumla wakuku litakavyoongezeka.

Mradi wangu naufanyia Tanga mjini wa ufugaji, maana ndipo nimeona aridhi inanunulika Kwa bei rahisi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam.

Nimeambatanisha Banda langu mojawapo nalolimalizia pamoja na picha kuku za kuku wangu 3.

Naamini haitokua rahisi kufikia kuku elfu 5, lakini naamini pia haishindikani kufikia malengo.

Asante wakuuu wangu na karibu niweze pata mchango na mawazo yenu kama hamtojali.
Hongera sana kwa udhubutu .
Ni wazo zuri sana maana utatoa ajira kwa vijana wenzio pia .

Ila jitahidi kuwa muangalifu sana kwa hao utakaowaajiri , ikipendeza wachukue watu wenye elimu ndogo sana ila wape ujuzi na jitahidi kuzingatia maslahi yao kwa moyo wote pasina kuwazungusha hakika utafika mbali .

Vijana wenye ujuzi na uhitaji wa kujituma kwenye miradi ya aina hiyo wapo ukiwahitaji karibu ikiwa utawiwa .

Hongera sana kijana .
 
Mkuu watu ninao tayari, na elimu yao ni form four tu, nimeishi nawahindi baadhi naelewa Kwa nini ndani ya kiwanda chenye wafanyakazi miatano utakukuta waliona degree hawazidi 20, wengine utakuta Wana elimu ya Veta na wengi wao unakuta niform four na wengine nilasaba wanaojua kusoma na kuandika.
 
Sawa hongera sana , nafurahi kwakuwa umenielewa vyema kwenye watu husika , basi kila la kheri ipambanie ndoto yako hakika utaiona .

Nakusubiri kukuona kwenye vipindi kama Kazi ni kazi _ UTV , Ijue siri ya mafanikio _ Tumaini Tv na kila jema lipo kwako _ ZBC

Hongera sana .
 
Nikuambie tu kitu; hao kuku elfu 5 unaweza kuwafimisha ndani ya mwaka Moja tu.

Fanya hivi nunua vifaranga 600 chotara Kwa hiyo bajeti yako vilishe chakuka Cha dukani Kwa mwezi Moja baada ya hapo Anza kuchanganya chakuka chako.

Baada ya miezi 4 hao kuku wataanza kujihudumia kama ifuatavyo

Kama utawatunza vizuri lazima utakuwa na kuku 500+ tuseme jogoo 200 na jike 300.

1. Baada ya miezi mitatu utauza hao jogoo Kwa 20,000 x 200= 4,000,000

2. Baada ya miezi 4 utaanza kuokota mayai utaweza kuokota mayai 4500 Kwa mwezi sawa na trei 150 ukiuza Kwa bei ya chini utapata 1.5

Ukichukua 4+1.5 utakuwa umeingiza 5.5M

Sasa itabidi utumie hizo pesa kukuza mradi Kwa kufanya yafuatayo:-

A. Nunua incubator yenye uwezo wa kubeba mayai 1000; hii unaweza kuipata Kwa 2M.

B. 2M Jenga Banda then totolesha vifaranga ambapo kati ya mayai 1000, yakitoka vizuri utapata vifaranga 800

Vikuze baada ya miezi 4 mingine utakuwa na kuku jike kama 700 na jogoo 400 kama Kawa uza jogoo wako 300 ili update 6M

Huku utakuwa kila mwezi unazakisha mayai 10,500 sawa na trei 350 ambazo zitakuingizia 3.5M.

Baada ya hapo kama utakuwa umeendelea na utotoleshaji wa vifaranga utakuwa na kuku kama 4000 ndani ya mwaka Moja.

NB. Jenga mabanda simple yanayichukua nafasi ndogo ila yanabeba kuku wengi.
 
Asante mkuu wangu Kwa ushauri Bora kabisa, nimeuchukua naufanyia kazi. Kuna wahuni wanauza vifaranga ambao hawakui nahawa ndio nawahofia, pia nahitaji kupata Mbegu nzuri ndio maana nahitaji ninunue vifaranga hasa Kwa watu naowafaham na ambao nimewatembelea. Kuna mfugaji mmoja nimeingia nae makubaliano yakua ananiuzia chotara wa miezi 2 Kwa bei nafuu ndio nataka nimtumie huyu maana kwanza nimtu ambae namfaham na pia anapofanya kazi boss wake nirafiki wa Jamaa yangu.

Pia nahitaji niweze kuona progress kidogo kidogo na changamoto zao l na atleast Kila kuku 100 wawe wanatofautiana mwezi mpaka miezi miwili, hii Kuna namna itanisaidia.

Nashukuru Kwa mawazo yako mkuu wangu.
 
Umeniita, nami nipo hapa.

Kwanza nitoe dukuduku. Huwa sipendi ubabaishaji katika mambo muhimu kama hili unalozungumzia hapa.

Stori yako haikunyooka sana, pamoja na kuwepo kwa mambo yanayoonekana kuwa ya maana.

Nitoe mfano: Umesema umri wako ni miaka mingapi?

Umesema unazo biashara nyingine zinazokuingizia pato la kukulipa mshahara wa Tsh. ngapi? Hizi biashara zinaendeleaje, na itakuwa vipi utakapojitumbukiza kwenye ufugaji wa holela usiokuwa na mpangilio kama huu ulioeleza hapa!

Sasa ukitaka nishiriki kwenye kutoa ushauri katika ufugaji, nyoosha stori yako ieleweke vizuri. Habari yako ina michongo mingi isiyo eleweka.
Ukilazimisha kufuga kwa kutegemea mpangilio huu ulioweka hapa nikwambie bila kusita, kwamba hufiki popote.

Kwa sasa nitakuacha na hayo machache.

N.B. Naona hapo mkuu 'Fursa Kibao' kakutia mori!
Kama unategemea kufuga kwa namna hiyo aliyoeleza hapo, utafuga kwa kusadikika tu!

Kumbuka, usinilaumu. Si nia yangu kukukatisha tamaa, lakini andiko lako kama ulivyoliwasilisha, lina maswali mengi yasiyoeleweka. Kwa kifupi ni kwamba siamini kuwa wewe uko tayari kufuga kuku.
 
Umeniita, nami nipo hapa.

Kwanza nitoe dukuduku. Huwa sipendi ubabaishaji katika mambo muhimu kama hili unalozungumzia hapa.

Stori yako haikunyooka sana, pamoja na kuwepo kwa mambo yanayoonekana kuwa ya maana.

Nitoe mfano: Umesema umri wako ni miaka mingapi?

Umesema unazo biashara nyingine zinazokuingizia pato la kukulipa mshahara wa Tsh. ngapi? Hizi biashara zinaendeleaje, na itakuwa vipi utakapojitumbukiza kwenye ufugaji wa holela usiokuwa na mpangilio kama huu ulioeleza hapa!

Sasa ukitaka nishiriki kwenye kutoa ushauri katika ufugaji, nyoosha stori yako ieleweke vizuri. Habari yako ina michongo mingi isiyo eleweka.
Ukilazimisha kufuga kwa kutegemea mpangilio huu ulioweka hapa nikwambie bila kusita, kwamba hufiki popote.

Kwa sasa nitakuacha na hayo machache.

Kumbuka, usinilaumu. Si nia yangu kukukatisha tamaa, lakini andiko lako kama ulivyoliwasilisha, lina maswali mengi yasiyoeleweka. Kwa kifupi ni kwamba siamini kuwa wewe uko tayari kufuga kuku.
Mkuu Kalamu heshima kwako, lengo lakutaja umri range nikuonyesha kua bado nipo kwenye umri wa kufanya,kushindwa kufanya Tena na Tena nikiwa Sina majukumu yakua na pressure ya familia inayonitegemea kama mke na watoto. Kwahio kipato ambacho nachokipata Kwa Sasa kinaingia katika uwekezaji .

Mkuu @ Kalamu hizo biashara nyingine namaana zinajiendesha pamoja na mimi kunilpa mshahara wa million 1.8 kama sehemu ya mfanyakazi. Napotoa huduma juu ya biashara yangu inahitajika inilipe mshahara , hii nimefanya hivyo ili bishara zijiendeshe zenyewe. Na hiki kiasi nachopata ndicho nachotumia Kwa matumizi binafsi kama Kodi ya yanapoishi pamoja na bill nyinginezo ambazo hazihusiani na biashara Moja kwa Moja. Hii pia nikuonyesha sihitaji biashara Moja iisukume biashara nyingine Bali Kila biashara ijisamamie yenyewe Kwa mapato yake na Kila baada ya miezi 2/4 nafanya ukaguzi juu ya biashara husika kuangalia namna gani inavyoendelea hii inanisaidia kujua uelekekeo wa biashara zangu kama zinakua au ziko palepale au zinashuka nasababu nizipi.

Napohitaji niingie katika ufugaji naingia kama sehemu ya ufunguzi wa biashara nyingine , nikiwanamaana ntaisimamia mwenyewe siku nne mpaka Tano zawiki Kwa muda usiopungua masaa 9 Kwa siku na wasaidizi wangu wawili Kila mmoja atakua hapo kwenye Banda masaa yote maana ndio mahala watakapokua wanaishi.

Pia nimeingia makubaliano yakununua kuku aina ya SASSO ambao wanaweza kuatamia , vifaranga wenye miezi 2, Kila baada ya week 2 vifaranga mia Moja.

Naomba uwe specific wapi nimekwama wapi panachea ,wapi unahitaji maelezo ya ziada Kwa ufafanuzi wako zaidi mkuu wangu Kalamu .

Asantee Boss.
 
Mkuu kuku wakienyeji nafahamu changamoto zao kiasi ndio maana nimesema nimchanganyiko wa kuku wakienyeji pamoja na chotara. Nafahamu ningumu lakini haishindani mkuu wangu kufikia ijumanne ntakua nimemaliza Banda lakwanza, Kisha kadri muda utakavyoenda ntakua naleta mrejesho.
Hukumsikiliza (kumsoma) vizuri huyo uliyemjibu hapo.
Jibu lako hili halitatui tatizo aliloligusia.
Hilo tayari ni kosa lako namba moja katika kazi unayotaka kuifanya.

Mchanganyiko wa chotara na kienyeji halifuti tatizo la ufugaji wa hao kuku.

Nadhani inabidi nimalizane nawe hapa kwa sasa.
Ushauriwangu ni: Nenda kajipange upya.
 
Back
Top Bottom