Naomba Ushauri: Nimempa ujauzito mke wa mtu ambaye ameachana na mmewe miaka miwili iliyopita bila talaka

apologize

JF-Expert Member
Jul 22, 2015
710
568
Habari wakuu?

Kuna binti nipo nae kwenye mahusiano kwa miezi sita sasa. Nilikutana nae kwenye mgahawa mmoja nilipokuwa naenda kupata chakula. Mimi bado sijaoa na sina familia maisha yangu mengi nakula kwenye migahawa.

Nilimpenda kiukweli hatimaye nikawa nae. Binti huyu akuniambia mama ameolewa ( tena ndoa ya kanisani) na alinificha mwanzo kama amezaa lakini nilipofanyana nae mapenzi kwa mara ya kwanza nilitambua Hilo nikamuuliza akakubari kuwa amezaa, Swala la ndoa hakusema.

Inshu ya ndoa nilikuja kujua kwa boss wake anapofanyia kazi wakati napiga nae story akanieleza huyu binti ameolewa tena ndoa halali ya kanisani wametengana na Mme wake kama miaka miwili nyuma.

Nilibidi nimuulize kuhusu Hilo swala alikiri kweli lakini wameachana kabisa. Nikamuuliza utaratibu gani mlitumia anasema waliandikishana ofisi za kijiji Tu hakuna alioenda mahakamani kudai talaka. ( Unafahamu mambo ya kijijini wanachukulia vitu rahisi).

Changamoto ninayo kutana nayo ni kuwa binti kamueleza mama yake kuwa Yuko na mimi na huwa namsikia anaongea nae kwenye simu na mama akisema msalimie mwenzako maana huyu binti mara nyingi anakuja kwangu anapika na kulala kwa siku ambazo haiingii kazini. Na kulala analala Kariba Kila siku kwangu.

Shida ninayo kutananayo nikimwambia mjulishe mama yako kuwa wewe ni mjamzito tuone anasemaje. Hawezi kumwambia mpaka mimba iwe kubwa ya almost miezi Saba au mimi niwaambie wazazi wangu kuwa yeye ni mjamzito.

Mimi nitawezaje kuwaeleza wazazi wangu kuwa Nimempa binti mjamzito kumbuka ni mke wa mtu ambaye hana talaka na pia binti anataka kuishi wote rasmi akiwa mjamzito japo maisha yangu ya kujitafuta lakini naishi kwa bajeti ya laki 2 na 50 kwa mwezi.

Naombeni Ushauri juu ya hilo kwa wazoefu na mnisamehe siyo mzuri kwenye kuandika masimulizi.
 
Cha msingi mwambie ukweli amalizane na mwenziwe ki taratibu zote lakini pia wewe hupaswi kuwa nae kimapenzi. Lea mimba mpaka mtoto ww beba msalaba wa kulea mtoto tu achana na mambo ya mahusiono na mwanamke ambae alishaolewa ndoa ya kanisani tena mumewe akiwa bado yupo hutokuja kuwa na amani na furaha huko baadae na je

Hakuna Raha wala mapenzi amani kuoa tena mwanamke aliyeshindwanana na mumewe Hawa huwa huishia kuwa michepuko tu na single mothers usiyanunue matatizo achana nayo.

Wanawake wengi sana wa Kila sampuli kama huwaoni nenda hata hapo kwa mwamposa chagua size Yako achana na laana ya mke wa mtu maanguko yote makubwa kwa wanaume tangu Adam na Eva mpka Samson na Delilah na wote unawajua ww mpka nanii the late siwezi kumtaja chanzo ni mwanamke kimbia mwanaume mwenzangu Hawa ni dada zetu bibi zetu mama zetu na shangazi zetu lakini Hawa watu kwetu ni balaa
 
Miaka miwili hiyo ni automatically ndoa ilishavunjika hakuna haja ya kuuliza talaka, cha kufanya anza taratibu upya kama vipi fika kwao chumbia kama ni mahali ongea na wazazi wake mtolee na ikibidi mfunge ndoa kanisani kabisa.

Usijipe stress bure hakuna ndoa hapo, miaka miwili kweli, yeye huyo jamaa yake huko aliko hajaoaga tu au naye kakaa tu kabweteka huku hajui hata "mkewe" anakula nini anavaa nini, kuwa huru kamilisha taratibu jitwaliie jiko wewe ukiona wa nini kuna wenzio wanajiuliza watampata lini.
 
Inawezekana ww ndio chanzo Cha kuivunja ndoa ya amaa saiv unazunguka hapa tutuziga Cha msingi mwambie ukweli amalizane na mwenziwe ki taratibu zote lakini pia ww hupaswi kuwa nae kimapenzi Lea mimba mpaka mtoto ww beba msalaba wa kulea mtoto tu achana na mambo ya mahusiono na mwanamke ambae alishaolewa ndoa ya kanisani tena mumewe akiwa bado yupo hutokuja kuwa na amani na furaha huko baadae na je
Hivi huwa mnaona Raha Gani kuchukua mke wa mtu na una lala nae na kutembea nae kwa Amani wakati mumewe yupo wanawake single mbona wengi sana..
Huyu binti alitoka mkoa mwengine amekuja kufanya kazi mkoa mwengine. Kwa hiyo nilikuwa sijui chochote si unajua mtu akiamua kuficha taarifa zake. Na yeye hajui huyo mwanaume anaishi wapi ss hivi.
 
Inawezekana ww ndio chanzo Cha kuivunja ndoa ya amaa saiv unazunguka hapa tutuziga Cha msingi mwambie ukweli amalizane na mwenziwe ki taratibu zote lakini pia ww hupaswi kuwa nae kimapenzi Lea mimba mpaka mtoto ww beba msalaba wa kulea mtoto tu achana na mambo ya mahusiono na mwanamke ambae alishaolewa ndoa ya kanisani tena mumewe akiwa bado yupo hutokuja kuwa na amani na furaha huko baadae na je
Hivi huwa mnaona Raha Gani kuchukua mke wa mtu na una lala nae na kutembea nae kwa Amani wakati mumewe yupo wanawake single mbona wengi sana..
Sijavunja ndoa na hata simjui nimekutana nae alipokuja kwenye mkoa ambao mimi nipo. Ndoa yake anasema waliachana miaka miwili iliyopita na mmewe aliambiwa yuko mkoa mwengine kwa hiyo hawajawahi kuwasiliana.
 
Vuta kitu hicho weka ndani muishi kwa amani kipato kitaongezeka mpe mtaji afungue kijiwe Cha chakula huku anaingiza nawe unaingiza jioni mahesabu.

Kuwa mke wa mtu hakuzuii nyie kuoana kama nyota zenu zinaendana mtaishi kwa amani. Maisha ya dunia bila amani bora usizaliwe.

Angalia mtu anaekupa amani
 
Sijavunja ndoa na hata simjui nimekutana nae alipokuja kwenye mkoa ambao mm nipo. Ndoa yake anasema waliachana miaka miwili iliyopita na mmewe aliambiwa Yuko mkoa mwengine kwa hyo hawajawahi kuwasiliana
Hakuna ndoa hapo hata wakienda mahakamani. Kukaa na mwanamke bila kushiriki tendo ndani ya miezi pasipo sababu huku mkiwa mbalimbali na hakuna mawasiliano kisheria hio ndoa imekufa.

We kakamalishe makaratasi upunguze idadi ya masingle mama mjini.
 
Mwanamke huyo sio muaminifu kwako ,kwanza kakudanganya Hana mtoto ,pili kaficha kuwa alishaolewa

Unadhani ukianza kuishi naye vingapi atakuficha? Unadhani Kwa hizo dalili masuala ya kiuchumi atakuwa muwazi kwako ...mapenzi ya kweli huanza na dalili njema za uwazi hasa Kwa vitu muhimu kama hivyo

Kwa kifupi Dunia ina wanawake zaidi ya billion 4 komaa upate mwingine ambaye atakuwa sahihi kwako
Wote ni wadanganyifu ili kupata ndoa hata mkeo baada ya ndoa ndio umejua baadhi ya vitu.
Anataka ndoa ataweka vipi wazi madhaifu.
Uenda mme wake ndie mwenye matatizo
 
Habari wakuu?

Kuna binti nipo nae kwenye mahusiano kwa miezi sita sasa. Nilikutana nae kwenye mgahawa mmoja nilipokuwa naenda kupata chakula. Mimi bado sijaoa na sina familia maisha yangu mengi nakula kwenye migahawa.

Nilimpenda kiukweli hatimaye nikawa nae. Binti huyu akuniambia mama ameolewa ( tena ndoa ya kanisani) na alinificha mwanzo kama amezaa lakini nilipofanyana nae mapenzi kwa mara ya kwanza nilitambua Hilo nikamuuliza akakubari kuwa amezaa, Swala la ndoa hakusema.

Inshu ya ndoa nilikuja kujua kwa boss wake anapofanyia kazi wakati napiga nae story akanieleza huyu binti ameolewa tena ndoa halali ya kanisani wametengana na Mme wake kama miaka miwili nyuma.

Nilibidi nimuulize kuhusu Hilo swala alikiri kweli lakini wameachana kabisa. Nikamuuliza utaratibu gani mlitumia anasema waliandikishana ofisi za kijiji Tu hakuna alioenda mahakamani kudai talaka. ( Unafahamu mambo ya kijijini wanachukulia vitu rahisi).

Changamoto ninayo kutana nayo ni kuwa binti kamueleza mama yake kuwa Yuko na mimi na huwa namsikia anaongea nae kwenye simu na mama akisema msalimie mwenzako maana huyu binti mara nyingi anakuja kwangu anapika na kulala kwa siku ambazo haiingii kazini. Na kulala analala Kariba Kila siku kwangu.

Shida ninayo kutananayo nikimwambia mjulishe mama yako kuwa wewe ni mjamzito tuone anasemaje. Hawezi kumwambia mpaka mimba iwe kubwa ya almost miezi Saba au mimi niwaambie wazazi wangu kuwa yeye ni mjamzito.

Mimi nitawezaje kuwaeleza wazazi wangu kuwa Nimempa binti mjamzito kumbuka ni mke wa mtu ambaye hana talaka na pia binti anataka kuishi wote rasmi akiwa mjamzito japo maisha yangu ya kujitafuta lakini naishi kwa bajeti ya laki 2 na 50 kwa mwezi.

Naombeni Ushauri juu ya hilo kwa wazoefu na mnisamehe siyo mzuri kwenye kuandika masimulizi.

Mkuu ukifanya mapenzi na mwanamke aliyezaa unajua?? Maana sie wengine tunafanya hadi na maajuza lakini tunaona ni vigori.
 
Wewe unataka kula tunda bila majukumu au ni muharibufu tu kama wale wazee wa kataa ndoa ni utumwa ilihali wanataka kuchakata mbususu bila responsibilities. Mkuu, ukitaka kuchakata jua pia kwamba kuna consequences na sasa deal na hizo consequences.

Unatusumbua tu humu JF kwa kutaka mawazo mbadala ili ujue pa kuchomokea... huchomoki ngo, labda atoe mimba, na kwa jinsi ulivyoandika huyo demu hataki habari hizo... Omba Mungu tu mme mtu asikushitaki kwa ku-destabelise ndoa yake halali.
 
Back
Top Bottom