Naomba ushauri na Msaada wenu kuhusu Scholarships Application Vyuo vya nje

smiler705

Member
Jul 27, 2023
26
11
Hello guys, habari za humu ndani wana JF.

Mi ni binti, nimemaliza form 6 mwaka huu na namshukuru Mungu nimefauru vizuri, nimepata dv 1 ya point 7 HGL, na niliapply vyuo baadhi na nimechaguliwa vyote including Udsm

Lakini napenda nipate scholarship nisome vyuo vyo nnje hasa nchi za ulaya, Canada au US, sababu ni ndoto yangu kubwa, na hua namuomba Mungu sana, nimefanya application baadhi, lakini kuna vitu nashindwa, naomba mwenye ujuzi wa kunisaidia jinsi kuapply scholerships please help me, naomben mnisaidie tafadhari, ushauri wenu baba, mama, kaka na dada zangu help me please, najua humu ndani watu wanafahamu nambo mengi, thats why naamini sana JF members. Karibunii na natanguliza shukurani.
 
Hongera sana kwa ufaulu na upambanaji katika kutimiza ndoto zako ila samahani jitahidi kurekebisha muandiko wako .

Ufauru× = Ufaulu✓
Scholership × = Scholarship ✓
 
Hongera sana kwa ufaulu na upambanaji katika kutimiza ndoto zako ila samahani jitahidi kurekebisha muandiko wako .

Ufauru× = Ufaulu✓
Scholership × = Scholarship ✓
Shukurani mkuu, ngoja nirekebishe, thanks again
 
Pia uwe makini maana Kuna matapeli kibao saiv wapo kwenye vivuli vya kujifanya wana waunganisha watu na scholarship za nje, kupigwa nje nje.
Chukulia makini huu ushauri ,matapeli nao wapo vile vile.
 
Hongera kwa hatua hiyo!
Ushauri wangu, soma kwanza upate shahada ya kwanza kutoka vyuo vyetu vya ndani, halafu shahada ya Uzamili sasa uombe vyuo vya nje. Samahani kwa mawazo yangu, ila kama hutanielewa leo, utanielewa siku nyingine. Kila la kheri!
 
Nikiwa kwenye websites nyingine nataka ku apply zinaleta Soo many datas, nashindwa kujua nifanyaje, maybe nakoa procedures au vipi, Ili simalizi , znakua snajirudia, help me wana JF
 
Hongera kwa hatua hiyo!
Ushauri wangu, soma kwanza upate shahada ya kwanza kutoka vyuo vyetu vya ndani, halafu shahada ya Uzamili sasa uombe vyuo vya nje. Samahani kwa mawazo yangu, ila kama hutanielewa leo, utanielewa siku nyingine. Kila la kheri!
Nimeyapokea mkuu na ni mawazo mazuri pia, Asante sana,nitayafanyia kazi pia
 
Back
Top Bottom