Naomba ushauri kuhusu kurejesha mkopo

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Sep 20, 2020
1,636
3,806
Habari wanaJF.
Mimi nimenufaika na mkopo kutoka benki fulani...sasa marejesho yako ni 16000/= kwa siku ni kwa muda wa miezi 18.

Ila biashara nayofanya kwa siku ninaweza kupata 20000/= ambayo nikilipa yote muda wa mkopo utapungua na kufikia miezi 13.

Sasa swali langu kuna haja ya kuweka kipato cha juu zaidi kuliko yale marejesho ya bank?

Au nirudishe kutokana na mahitaji ya bank na pesa ingine iliozidi nifanye mambo mengine?

Naombeni ushauri aisee
 
Siku hazilingani. Endelea kulipa 16k, hiyo 4K weka akiba...kuna siku utakosa 16k itatumia hiyo akiba kulipa. Lakini pia uta tumia akiba kukuza mtaji kidogo kidogo.
 
Anhaa kwaiyo hakuna haja ya kuweka kiasi kikubwa ambacho ni juu ya marejesho kwa lengo la kufanyia mambo mengine muhimu?
 
Back
Top Bottom