Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Mazda Atenza 2015

Nimekaa nalo miezi 10 hadi sasa. Sijakutana na shida yoyote.

1. Ulaji wa mafuta ni subjective. Ila kwa mimi nilietoka BMW 323i cc 2500 Petrol ambapo mjini napiga 6km/L sahivi napiga 13km/L kwenye heavy traffic. Pia iStop inasaidia sana kupunguza ulaji wa mafuta. Highway napiga hadi 25km/L nikiwa natumia Adaptive Cruise Control.

2. Spare hadi sasa sio issue ila nishajua machaka yote ya spare. Oil natumia ya Castrol C3 5W30 kitu lainiii. Oil lita 5.1 ukibadirisha na filter haifiki 200K.

3. Speed imebaniwa ni 180km/L ila inatosha kabisa. Kwasababu natumia sana mjini highway ni weekend na road trips.

4. Last year niliupdate kwenye uzi wa road trip nilitoka Dar to Lushoto kisha Moshi Then Arusha then Manyara kisha Dom kisha Moro then Dar. Kwa wese la roughly Tsh 250k pamoja na misele ya mjini. Usieamini jiue.

5. Kabla hujanunua diesel ya Mazda soma kidogo kuhusu DPF

Baadhi ya picha:
Hii chini Moro. Zingatia Ground clearance ipo low sana.
View attachment 2949444
Hii B'Moyo. Buti kubwa ila Baiskeli haitoshi lazima niitoe tyre la mbele.
View attachment 2949445
Hii Ushoroba zingatia ground clearance.
View attachment 2949454

Challenge so far:
1. Diesel inataka kuendeshwa sana. So kila weekend mbili after misele ya mjini lazima nipeleke Bagamoyo kwaajili ya DPF regeneration. Bagamoyo situmii zaidi ya wese la 20 kwenda na kurudi starting point Ubungo.

2. Ipo chini sana ila nishazoea magari ya chini. Sijainganyua na sina mpango.

3. Mazda issue ya rangi wanapaka rangi nyepesi sana so jiandae kuchubuka kifala sana. Waulize ata CX5.

4. Gari refu sana. Size kama Crown Majesta au katikati ya BMW 7 series na 5 series.

All in all, nikifananisha na 3 series, uyu nampa 7/10 wakati BM nampa 5/10 hivi. Wajerumani wakina PureView zeiss mtanisamehe. Sirudi Uko kamwe.

PS: Kama upo Ubungo siku njoo upige misele kidogo ufanye maamuzi.
Mkuu assante sana natunai umenipa nguvu ya kuchukua hii chuma naona nichukue model ya 2015 assante pia natumai hii kitu itakuwa na comfort nzuri tu
 
Mkuu assante sana natunai umenipa nguvu ya kuchukua hii chuma naona nichukue model ya 2015 assante pia natumai hii kitu itakuwa na comfort nzuri tu
Kwanini unataka uchukue ya 2015? Tuanzie hapo.
Najua inatofauti na ya 2014.

Ya mwaka 2014 hii hapa:
images (6).jpeg

Ya mwaka 2015 hii hapa:
images (7).jpeg

Mi nikichukua 2015 coz napenda Electronic E-Brake, iyo redio ilivokaa hapo juu na iDrive like knob.

Nje zipo sawa kasoro Grille, LED lights na that Fucking Grill Strip kwenye 2015 Model.

Kama una hela chukua ya 2016 ina pedestrian detection sensor. Gimmicky!
 
Kwanini unataka uchukue ya 2015? Tuanzie hapo.
Najua inatofauti na ya 2014.

Ya mwaka 2014 hii hapa:
View attachment 2950171

Ya mwaka 2015 hii hapa:
View attachment 2950172

Mi nikichukua 2015 coz napenda Electronic E-Brake, iyo redio ilivokaa hapo juu na iDrive like knob.

Nje zipo sawa kasoro Grille, LED lights na that Fucking Grill Strip kwenye 2015 Model.

Kama una hela chukua ya 2016 ina pedestrian detection sensor. Gimmicky!
Iyo handbrake ndio sababu kubwa kukimbia 2014 mkuu, kama bei hazitopishana sana ntachuku 2016
 
Mie ni mpenzi sana wa sedans na nilipanga nikibadili gari basi nihamie Mazda Atenza. Changamoto imekuja kwenye makazi ya kudumu. Umbali wa kutoka nyumbani (rough road) ni 7km (return) hadi kufika barabara ya lami. Barabara si rafiki kwa sedans au hatchback/station wagons. Nilibadili uamuzi kinyonge. Nilikuwa napenda sana body ya 2008-2010.
 
All in all, nikifananisha na 3 series, uyu nampa 7/10 wakati BM nampa 5/10 hivi. Wajerumani wakina PureView zeiss mtanisamehe. Sirudi Uko kamwe.

PS: Kama upo Ubungo siku njoo upige misele kidogo ufanye maamuzi.
Kipindi Kile Cha Nyuma Wakati Ndio Ulikuwa Ndio Mjerumani Haswa Adolf Hilter Kabisa Ulikuwa Uambiwi Kitu.

Sasa Avatar Yao Uwarudishie.
 
Mazda 6 nadhani ni kwa soko la marekani na Canada ila kimsingi ni gari hilo hilo. Tofauti ni ndogo ndogo sana kama zipo, labda taa, upholstery n.k ili tu kutofautisha
Assante mkuu maana nimeona zipo za Singapore nyingi ni petrol na za japani nyingi ni diesel pia bei za japan zimechangamka sasa niko kwenye kufanys maamuzi
 
Back
Top Bottom