Naomba msaada wenu mdogo wangu anasumbuliwa ovarian cyst

helena mgomu

Member
Sep 19, 2022
17
14
Habari Wana jf,

Naomba msaada wenu mdogo wangu anasumbuliwa ovarian cyst, Sasa mwezi wa saba alipimwa utrasound ukawa na cm 3.5 hakupewa dawa yoyoye, walisema utaisha wenyewe.

Sasa juzi maumivu yakawa upande wa kulia akatumia azuma na fragile Leo kaenda kupima hosp wamekuta ana uvimbe upande wa kulia na siyo kushoto na uko na cm 7.30 ×5, kilichotushitua ni kuwa maumivi amekuwa akiyasikia kushoto siku zote na hata vipimo vya awali vinaonesha ni kushoto hiyo cyst ipo

Swali langu no kwamba

imekuaje Tena uvimbe umeenda kulia halafu isionekane kushoto na still maumivu ya upande wa kushoto yanaendelea ikiwa maumivu ya upande wa kulia yameacha baada ya dawa kunywa!

2. Hataua za uvimbe kukua zikoje maana mwezi wa Saba ulikuwa 3.5 cm upande wa kushoto Leo kapima utrasound msomaji kasema ni cm 7.30 uko uapnde wa kulia lkn mgonjwa maumivu yapo kushoto!

3. Naomba kujua utrasound pia huwa zinakosea maana ni wazi jambo haliko SAWA hapo, either Kwa msomaji, mashine, au sisi ndiyo hatuelewi mambo ya kitaalam.
 
Mie udaktari sina, hapa nitachangia kumuombea dua tu, mungu amponye, awape nguvu na pesa nyie wauguzaji.
 
1. Ovarian cyst inatibiwa kwa operation ndogo, au kuchomwa sindano.

2. Kuwa na mkanganyiko wa majibu, inategemeana na mpimaji, ndo maana inashauriwa, kipimo cha USS pima angalau hospital mbili Tofauti alafu linganisha majibu kama yata endana au laa.

3. Ushauri mwingine, vipimo vya figo, moyo, uzazi, mara nyingi huwa yanatokea makosa ya kibanadam ambayo yanaweza kukupelekea ulemavu au hata kupoteza maisha 😢. NASHAURI, PIMA ZAIDI YA MARA MBILI KABLA HAUJAFANYIWA MAREKEBISHO YEYOTE MWILINI MWAKO. 🤝🤝🤝
 
Habari Wana jf,

Naomba msaada wenu mdogo wangu anasumbuliwa ovarian cyst, Sasa mwez was Saba alipimwa utrasound ukawa na cm 3.5 hakupews dawa yoyoye, walisema utaisha wenyewe.

Sasa juzi maumivu yakawa upnde wa kulia alatumia azuma na fragile Leo kaenda kupima hosp wamekuta ana uvimbe upnde was kulia na cyo kushoto na uko na cm 7.30 ×5, kilichotushitua ni kuwa maumivi amekua akiyasikia kushoto siku zote na hats vipimo vya awal vinaonyesha ni kushoto hyo cyst ipo

Swali langu no kwamba

imekuaje Tena uvimbe umeenda kulia afu isionekane kushoto na still maumivu ya upnde wa kushoto yanaendelea!ikiwa maumivu ya upande wa kulia yameacha baada ya dawa kunywa!

2. Hataua za uvimbe kukua zikoje jmn maana mwez wa Saba ulikua 3.5 cm upande wa kushoto Leo kapima itraspund msomaj kasema n cm 7.30 uko upnde was kulia lkn mgonjwa maumivu ypo kushoto!

3. Naomba kujua utrasound piah hua zinakosea maana ni Waz jambo haliko SAWA hapo,either Kwa msomaj , mashine ,au sisi ndy hatuelewi mambo ya kitaalamu!!!

1: Ovarian cyst chini ya cm 5 na mwonekano wa kawaida nyingi huwa ni functional cyst/mabaki ya mfuko uliotoa yai. Ndio maana uliambiwa itaisha yenyewe. Mara nyingi tiba ni dawa ya maumivu tu.

2: Upatikanaji wa cyst upande mmoja, hauzuii kutokea upande mwingine. Hivyo, hii inayoonekana kwa sasa si kwamba imehama bali ni uwezekano wa cyst mpya. Kama majibu yote yako sawa

Hivyo, hakuna maajabu yoyote hapo. Mgonjwa atatibiwa kwa kadri ya kinachoonekana.

Kuhusu maumivu: si kila maumivu chanzo ni uvimbe, kuna sababu nyingine kama viungo tofauti kulata shida au maambukizi na kuna maumivu tunaita referred pain, mfano: tatizo la moyo lakini mau.ivu unasikia kwenye meno au maumivu ya figo unasika kwenye paja nk.

3: Ni kweli, majibu ya altrasound yanaweza kutofautiana kutoka msomaji mmoja mpaka mwingine. Mashine huwa inakuonyesha picha na mpigaji anatakiwa kutafsiri hiyo picha.
Hii hutokana na:

1: Uwezo wa uelewa/maarifa (knowledge) wa mteknolojia kufanya altrasound na kutoa tafsiri.

2: Aina ya mashine/teknolojia anayoitumia mhusika. Uwezo wa kutoa picha inavyotakiwa.

NB: Panapokuwa na mkanganyiko ni vyema kupata kipimo kingine toka sehemu tofautishe. Mara zote mhusishe mtaalamu wa afya, kuchukua historia, ukaguzi na mwisho kipimo usiende kufanya tu kipimo.
 
Asnte umeeleza vzr sana,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom