Naomba msaada, kanusha sentensi hii "ameshiba sana"

mwachisabwe kibona

Senior Member
Aug 5, 2014
116
27
Naomba msaada jaman kuna watu tunabishana nao hapa wengine wanadai ''hakushiba sana''kwa madai Kwamba sarufi ya kiswahili haina dhima ya ''Ja''
Na wengine wanadai 'hajashiba sana' lakini wanashidwa kutoa dhima ya 'ja' na 'ku' inaonesha wakati uliopita Kwa wanaounga hajashiba sna
 
hajashiba sana ndio dahihi.....maana inakanusha tendo lililopo la Ameshiba sana.
ukisema hakushiba sana.....ni wakati ulishapita.......kwakuongezea tu ila mkuu hapo juu ameshakujibu.
 
Dah, nyie sasa naona mnanichanganya sasa.

Kukanusha ni, siyo mimi niliyesema nimeshiba sana, mmeninukuu vibaya.

Mkuu kukanusha kiufupi ni kama kukataa au kupinga kwa maana ya kuweka "negative" ya nyambo (negate) na kinyume ni kuweka kilicho tofauti haswa na jambo husika (opposite). Yani kama mtu hakushiba sana kanusho lake si lazima awe na njaa sana. Anaweza kuwa hakushiba sana na wala hana njaa sana pia. Lakini ingekua kinyume chake basi ni sawa yani "shibe" kinyume chake ingekua "njaa".
 
Mkuu hii yako inasound very logical.
 
Mkuu kinachofanyika hapa ni kitu cha kitaaluma , yaani sarufi maana ( semantikia) kama hujui afadhali upite tu!
katika neno "hajashiba " mofu ( kwa mujibu wa Chomsky et el ) "-ja-" inafanya kazi gani?

ha- hiki no kiambishi awali kinachoonesha nafsi ya tatu umoja, lakini pia huonesha ukaunushi wa tendon yaani kushiba.

-ja- ni wazi kwamba lugha ya kiswahili ina njeo ambazo zinafahamika kama vile -li-, -na-,-me- na -ta- lakini pia tukumbuke pia lugha ina sifa ya kughairi sifa na taratibu ya lugha yenyewe.

Hivyo basi, mofu - ja- inaingia katika njeo ya wakati uliopo hali timirifu..
lakini pia ni kighairi cha lugha.

Hii ni kwasababu nikitaka kuonesha wakati uliopita nitasema "hakushiba"

kana utakubali kuwa "Ku" ni njeo basis hata "ja" itakuwa njeo kwa sababu zina uwezo wa kubadilushana nafasi.

Akhsante.
 
Mkuu shukran kwa darasa; ingawa jibu langu hapo juu halikulenga kwenye nyakati za eidha ame-, ali-, haja-shiba n.k, bali ilikuwa tofauti ya kukanusha na kinyume tu. Kwa sababu mleta mada alitaka msaada wa "kukanusha" sentensi husika na mdau nilyemjibu nahisi aliandka "kinyume" cha sentensi hiyo na si kukanusha kama alivyotaka mleta mada.
 
Back
Top Bottom