Naomba msaada jinsi ya kujua Laptop ya bei ndogo chini ya 500,000 yenye uwezo mzuri

Digital base

Senior Member
Jul 19, 2020
126
189
Habari ya leo wakuu, samahani

Nahitaji kununua Laptop kwa ajili ya matumizi Katika shughuli zangu

Kazi nnazo hitaji kuzifanya zaidi ni kuandika vitabu, kutengeneza matangazo, posters n.k

Napenda nitumie laptop kufanya kazi hiyo kutokana na mazingira yangu kibiashara kuwa ya kusafiri mara nyingi

Naomba msaada kwa anaye jua vitu gani vya kuzingatia zaidi nikitaka kujua Laptop yenye uwezo wa kufanya kazi hizo bila usumbufu

Bajeti yangu ni chini ya 500,000 nahitaji kwenda dukani kununua pia naomba kujua warrant kawaida ni muda gani?

Samahani kwa usumbufu nimeamua kuja hapa kwakuwa sijui chochote kuhusu uwezo wa laptop naogopa kununua kopo

Maana nnayo moja nilinunua kwa watu wa mnada niliambiwa haina adapter niende kununua nikipata nijaribu na iko vizuri kwa mujibu wa maneno yao

Lakini mpaka leo sijapata adapter yake na nilipeleka kwa fundi akaniambia imekufa mother board pia tulijaribisha kwa kutumia adapter yenye kama ile japo si yake fundi akaniambia inarudisha moto na alipoichunguza zaidi

Ilikuwa haina betri na imetolewa vitu vingi sana kwahiyo hapa nimenunua kopo tu

Naomba msaada wenu maelekezo kidogo kwa aliye na utaalam na hizi machine

Maana nilitaka kununua kwa mtu tena naogopa kuongeza hasara zaidi pesa ikapotea tena

Asante sana kwa muda wako
 
Hiyo bei utata uliyonayo! Naomba kujua program utakazotumia kwenye shughuli zako

Kama utatumia product za microsoft kwenye shughuli zako nadhani pc yenye RAM 4gb itakuwa mpango kulingana na bei

Kikubwa hapa sema app ambazo utazitumia kwenye shughuli zako nione kama naweza kuwa wa msaada
 
Hiyo bei utata uliyonayo! naomba kujua program utakazotumia kwenye shughuli zako

Kama utatumia product za microsoft kwenye shughuli zako nadhani pc yenye RAM 4gb itakuwa mpango kulingana na bei

Kikubwa hapa sema app ambazo utazitumia kwenye shughuli zako nione kama naweza kuwa wa msaada
Hapa mkuu sana sana ni apps zenye uwezo wa kufanya kazi hiyo maana ndo najiandaa na hiyo program

Ila kuhusu matangazo zaidi natumia Google Chrome na Fire Fox
 
Hapa mkuu sana sana ni apps zenye uwezo wa kufanya kazi hiyo
Kikubwa hapa kwa bajeti yako angalia pc isiwe chini ya RAM gb 4 kwa maana kuna program ni pasua kichwa. Ukiwa na RAM ndogo ugumu utakuja pale kwenye kufanya task nyingi kwa wakati mmoja na pia kuna program zinahitaji uwe na PC yenye RAM iliyochangamka

Specifications nyingine hazina umuhimu kwako kwa maana bajeti kidogo sio rafiki.
 
Kikubwa hapa kwa bajeti yako angalia pc isiwe chini ya RAM gb 4 kwa maana kuna program ni pasua kichwa.Ukiwa na RAM ndogo ugumu utakuja pale kwenye kufanya task nyingi kwa wakati mmoja na pia kuna program zinahitaji uwe na PC yenye RAM iliyochangamka

Specifications nyingine hazina umuhimu kwako kwa maana bajeti kidogo sio rafiki.
Sawa sawa mkuu nashukuru sana kwa ushauri huu ubarikiwe
 
Bajeti yako changamoto kwa mpya, nenda Kariakoo maduka ya barabara ya Uhuru kanunue refurbished mkuu
 
Habari ya leo wakuu, samahani

Nahitaji kununua Laptop kwa ajili ya matumizi Katika shughuli zangu

Kazi nnazo hitaji kuzifanya zaidi ni kuandika vitabu, kutengeneza matangazo, posters n.k

Napenda nitumie laptop kufanya kazi hiyo kutokana na mazingira yangu kibiashara kuwa ya kusafiri mara nyingi

Naomba msaada kwa anaye jua vitu gani vya kuzingatia zaidi nikitaka kujua Laptop yenye uwezo wa kufanya kazi hizo bila usumbufu

Bajeti yangu ni chini ya 500,000 nahitaji kwenda dukani kununua pia naomba kujua warrant kawaida ni muda gani?

Samahani kwa usumbufu nimeamua kuja hapa kwakuwa sijui chochote kuhusu uwezo wa laptop naogopa kununua kopo

Maana nnayo moja nilinunua kwa watu wa mnada niliambiwa haina adapter niende kununua nikipata nijaribu na iko vizuri kwa mujibu wa maneno yao

Lakini mpaka leo sijapata adapter yake na nilipeleka kwa fundi akaniambia imekufa mother board pia tulijaribisha kwa kutumia adapter yenye kama ile japo si yake fundi akaniambia inarudisha moto na alipoichunguza zaidi

Ilikuwa haina betri na imetolewa vitu vingi sana kwahiyo hapa nimenunua kopo tu

Naomba msaada wenu maelekezo kidogo kwa aliye na utaalam na hizi machine

Maana nilitaka kununua kwa mtu tena naogopa kuongeza hasara zaidi pesa ikapotea tena

Asante sana kwa muda wako
Nacheka kama mazuri,anyway pole sana jamaa..ujinga always ni wakati wa kwenda..ila kwa hiyo bajeti unataka kurudia same mistake..kitu ukitakacho hakiendani na bajeti yako..utapata majanga tena,trust me!
tafuta hela kwanza..upate atleast laki 7 ununue mashine ya uhakika..kuwa mvumilivu!
 
AKienda discount kubwa kariakoo Anapata acha kumtisha ww
 
Kazi unazotaka kufanya ni basic sana nenda madukani upate used nzuri hata kwa laki nne; mambo ya kuuliza
RAM Kiasi gani 4gb au zaidi
HDD (hard Drive) anything zaidi ya 250gb
Processor; Core i3; i5 au i7
Battery; ulizia inakaa na chaji muda gani
Graphics card; Kama unafanya designing kubwa kubwa au kucheza games hii pesa huenda isitoshe ila kama ni basic kama ulivyosema basi inatosha (graphics cards za maana kina nvidia n.k. graphic peke yake tu inaweza ikakutoa dollar zaidi ya 1000; ila kama hauchezi games au kufanya Computer aided design huitaji hii

Mwisho kabisa cosmetics..., yaani muonekano wa nje kulingana na mapenzi yako....

400K ni tosha kabisa
 
Back
Top Bottom