Naomba maoni juu ya kilimo biashara na teknolojia katika kilimo

rosewilliam

New Member
Feb 1, 2024
2
0
Habari zenu wakuu.

Ningependa nipate maoni/busara yenu katika hili. Mimi natamani sana hapo baadaye niekeze katika kilimo biashara. Najua kila zao lina changamoto zake ila nahitaji kuelewa kutoka kwa wale ambao wana experience katika hili wanisaidie kunijulisha, ni changamoto gani ziko katika kilimo biashara leo hii in general? Kitu kingine ninachoona ni ukuaji wa teknolojia katika kilimo kama data availability kusaidia katika kufuatilia ukuaji na utunzi wa mazao kuanzia unapolima mpaka unavuna na kuingiza sokoni. Je kuna changamoto zinaweza tatuliwa kwa data? Na je data gani inaweza kuwa na umuhimu sana katika kilimo?

Shukrani sana
 
Kwa upande wa data muhimu kwny kilimo:-
1.Taarifa za bei ya mazao sokoni katika misimu mbalimbali hii itakusaidia kujua upande zao gani katika kipindi kipi(DataSource:- TAHA Tanzania wanatoaga taarifa za kila wiki/mwezi)

2.Taarifa za mwenendo wa hali ya hewa,, Joto,Baridi,Mvua,Upepo etc(DataSource:- Tanzania Meteorological Agency,TMA)

3.Taarifa za uhitaji na upatikanaji wa zao husika ndani na nje ya nchi

Kwa kuanzia na kwa haraka nliyonayo anza na hzo nkitulia ntaleta zngne
 
Shukrani sana!
 
Back
Top Bottom