Mkuu kilindi kuko poa lkn bei ya chakula ipo juu sana pale wilayani Songe. Usafiri wa dar to kilindi upo ni Tsh.17,000/= maji ni ya kisima yana chumvi,umeme upo wilayani na miji iliyopo kando ya barabara itokayo Handeni to Songe, guest zipo nyingi hata za buku 2. Wenyeji ni Wazigua, Wanguu, Wamasai na Wakaguru. Uchawi hasa "tego" ni kitu cha kawaida. Kuna ardhi nzuri sana kwa kilimo, madini ya aina mbalimbali na misitu ya miti ya asili. Vipi dili lenyewe ni hapo wilayani songe au ni vijijini?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.