Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Kwa ufahamisho, Dodoma ulitangazwa rasmi kuwa mji mkuu wa Tanzania na rais mwanzilishi Julius Nyerere mwaka 1973.
Uamuzi wa kuhamisha makuu makuu Dodoma ulichukuliwa na Halmashauri ya TANU chini ya Mwenyekiti wake Baba wa Taifa.
Baada ya hapo Mwalimu Nyerere alihamia Dodoma na kuishi huko kwa siku kadhaa akitekeleza majukumu yake akiwa huko.
Pamoja na mpango wa kuhamia Dodoma kutakiwa kukamilika ndani ya miaka mitano sababu za kutofanikisha zilikuwa nyingi...
Kumbukeni pia kwamba Chama cha Mapinduzi, CCM, ilikuwa haijazaliwa...