Naomba connection au ushauri wa mchongo wa kufanya baada ya saa za kazi

Mmanyanigho

Senior Member
May 18, 2018
186
326
Wakuu bila shaka mu wazima wa afya.

Baada ya hustle za hapa na pale, kuandika nyuzi kadhaa humu na reply kedekede nikitafuta kazi hatimae nilipata, japo sio kutoka humu ni connection tu ya jamaa yangu niliesoma nae.

Hii kazi nina miezi nayo 4 mpaka sasa, mshahara wake kiukweli sio mkubwa hasa kwa matumizi ya jiji hili.

Nalipwa 250k kwa mwezi, na kazini natumia muda mrefu kidogo japo speed yangu ndo itaamua nitoke saa ngapi kazini.

Sasa kutokana na hilo, kijana wenu nimekuja kuomba ushauri, nasaha, connection, michongo ambayo ninaweza kuifanya baada ya kazi.

Naomba mnisaidie kimawazo wakuu, kuna muda unawaza mambo mengi akili inastac, unajikuata huwazi kitu sasa upo upo tu unaexist ila huishi.

Natanguliza shukrani.
Kama taarifa haijitoshelizi basi nipo kuwajibu.
 
Ni kweli mkuu ila changamoto yake ipo kwenye marejesho maana ntalua nafanya lazi usiku tu, na afya pia inaweza isiwe nzuri kwa kutolala.

Mimi niliwaza nijidundulize kwa walau mwaka mzima ninunue boda yangu.
Yeah fanya ivo ununue Boda yako
 
Yaani mleta mara sikuekewi Jiji la Dar unatafuta mchongo wa kitu Cha kufanya kweli wewe akili zimo? Jioni mbona waweza fanya biashara kibao kuuzia vyakula , Matunda,chips kuku,mishikaki,kuuzia bidhas Kwa kumtandika chini unaweka gunia unapanga bidhaa zozote unazowaza ,Bodaboda,taxi driver Dereva wa daladala night worker unspokea Dereva wa mchana nk
 
Mkuu kama una ujuzi au uzoefu wa kimojawapo basi nisanue.
Kila siku tunajifunza mkuu, utajiri mkubwa hasa kwa majiji kama dar ni taarifa sahihi.

Unaweza generalize kama wewe hapo lakini ukite mimi sijui kitu kuhusu hayo, ila ukinisanua kua eneo fulani kuna madini ni rahisi mimi kuchimba zaidi.
Shukran
 
Tembea usiku mitaani angalia watu wanafanya biashara gani na wewe angalia waweza fit wapi
 
Back
Top Bottom