Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 19
Nauliza.....nani zaidi?
- Hayati Mwl. Nyerere alipigania uhuru na kujaribu kutekeleza siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kuna wanaodai alijitahidi kwa kiasi kikubwa kuinua pato la mwananchi wa kawaida na kupunguza tofauti ya kipato kati ya aliye nacho na asiye nacho. Aidha, alifanikiwa kutokomeza ukabila, udini na kuhakikisha taifa kwa kiasi kikubwa linaunganishwa kwa lugha moja. Pamoja na mafanikio, wapo wanaodai kuwa sera zake zimewafanya watanzania kubweteka na kutokuwa na uwezo wa kupigania haki zao. Aidha, kuna wanaodai kuwa aliingiza nchi katika vita na nchi jirani kwa lengo la kumrejesha swahiba yake aliyepinduliwa katika nchi hiyo. Mwishoni mwa utawala wake, sera zake hazikuendana na hali halisi na zimebakia katika maandiko bila utekelezaji. Alipachikwa majina mengi mfano "Mchonga", "Musa", "Haambiliki" n.k.
- Alhaj Ali Hassan Mwinyi aliruhusu soko huria - ilikuwa kama sandakalawe - mwenye kupata alipata, wengine hawakuambulia. Kuna wanaodai kuwa sera zake kwa kiasi fulani zilichangia kuporomoka kwa uchumi. Aidha, kuna wanaodai kuwa aliwekwa makusudi na Rais wa kwanza ili atumike kama "remote control". Amebaki na jina la "Mzee Ruksa" kwa "kufungua" milango ya uchumi.
- Bw. Benjamin William Mkapa: Anasifika kwa kuimarisha uchumi na serikali kupata mapato zaidi yatokanayo na kodi.Inadaiwa alifanikiwa kuboresha miundo mbinu (hasa barabara). Hata hivyo anatuhumiwa kuendesha biashara Ikulu na kujiuzia baadhi ya rasilimali za taifa. Aidha wakati wa utawala wake nchi illingia katika mikataba ya uchimbaji madini ambayo kuna madai kuwa inawanufaisha zaidi wawekezaji wa kigeni kuliko taifa. Aliwahi kuitwa "Mr. Clean" ingawa jina hilo limefifia haraka.
- Luteni-Kanali mstaafu Jakaya Kikwete: Anakaribia kumaliza ngwe ya kwanza kwa mujibu wa "utaratibu wa CCM", na anatarajiwa kupewa kipindi kingine cha miaka mitano. Inasemekana amewezesha nchi kunufaika na misaada mingi kutokana na ziara zake nchi za nje. Kuna wanaomtuhumu kwa kutoshughulikia masuala yanayolididimiza taifa kama ufisadi, mikataba mibovu na uwajibikaji. Pia anatuhumiwa kudidimiza juhudi za kumchukulia hatua Rais mstaafu Mkapa na wahujumu uchumi. Majina aliyowahi kupachikwa ni pamoja na "handsome boy" na mwanzoni mwa utawala wake yeye na aliyekuwa Waziri Mkuu (Edward Lowassa) walibatizwa jina la "Boyz to Men".