Nani Zaidi: Mwanakijiji Vs John Mashaka

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji hata ujumbe wa nyumba kumi kuupata itakuwa matatizo.

Hivi ulivyoandika hii habari ulikuwa umeshakunywa chai ya asubuhi? au ulikuwa kwenye swaum. Tusikuhukumu kumbe ulikuwa na njaa!
 
<font size="3"><font color="#0000ff">Ndugu Wadau, Nadhani muda unavyokwenda, nchi yetu inazidi kudidimia katika wimbi la ufukara. Nchi imekwisha na hali inazidi kutisha, hasa tukizingatia hali ya kisiasa na ya kiuchumi.</font></font>
<br />
<br />
Mkuu sio kudidimia tu maisha kwa ujumla ni magumu sana hasa kwa watu tunaoishi chini ya dola moja kwa siku
 
Wakulu JF, salaam mbele sana

- Look here huu unafiki utatuua wa-Tanzania, tujifunze kuwa part of the solution badala ya kila siku kukazania kuwa part of the problem kwa sababu hatuwezi ku-make any progress needed as a nation na this kind of negative thinking,

- I mean kila siku tunalia hapa kwamba viongozi wengi tulionao hawafai, sasa here comes a suggestion kutoka kwa mwananchi mwenye uchungu na taifa lake, kwamba kwa maoni yake hao aliowataja anaamini kwamba wanaweza kulisaidia taifa letu kiuongozi, wakipewa nafasi na hasa za juu kwa uongozi wa taifa letu, huyu anajaribu kuwa part of the solution,

- Wanatokea the usuals, no progress no positive thinking, no nothing ila kubeza beza tu bila hoja, sometimes JF tunajishusha hadhi wenyewe, one day Mkulu Mwanakijiji ni semi-God, the next day hawezi kuwa kiongozi ni mchangiaji wa internent tu!, just nonesense at best. JF inapaswa kuwa ni taasisi ya ushauri wa bure kwa taifa letu, na sio siri we are very good at it sasa iweje tena members wa hii taasisi tusiwe na huo uwezo wa kuongoza hili taifa ambalo we are very good at analysing its core problems?

- Kuna mijitu inashauri eti weka CV zao hapa, hivi mna maana kwamba CV ya Kikwete na wenzake hazifahamiki? Sasa kama CV ni the naswer then kwa nini tumekwama as a nation? Kama CV ni the answer kwa nini tunalia hapa JF na viongozi wetu kila kukicha? Wakuu stop this madness, heshimu wanaokuzidi vipaji, heshimu wanaoukuzidi maarifa, wanaokuzidi uwezo wa kufikiri ndio the only way tunaweza kupata viongozi wanaotufaa kwa taifa letu!

- Sijui Cv za Mkulu Mwanakijiji na John Mashaka, lakini kwa maoni yao niliyowahi kuyasoma sehemu nyingi sana internent na magazetini, ninaamini they could do better to our nation than viongozi kama Kingunge, Mzindakaya, Lowassa, Karamagi, Mbowe, Lipumba, Mwakipesile, na wengineo wengi maviongozi magoi goi tuliojaza kwenye serikali yetu!

Go Mwanakijiji na John Mashaka!

Ahsante!

Ni Kutoka Kwangu:- William Malecela.

Kama kweli wewe ndiye William Malecela.....Big up! na kuanzia sasa nimeamini sasa watanzania tunatumia vichwa vyetu kuliko upambe wa 'system' na hasa u-CCM wa kizamani uliowalemaza wengi na kudhani nje ya CCM hakuna viongozi. Ni kweli mwanakijiji na hao wengine wana uwezo wa kutuletea mawazo chanya ya kujenga nchi...japo mimi pia naamini uongozi wa nchi unahitaji mtu mwingine aliyeiva kisiasa kuliko hawa. Tukutane 2015 naamini tutampata kiongozi mwenye mwelekeo wa kusikiliza wananchi hasa waliomasikini kuliko ilivyo sasa.
 
Hawa vijana wawili ni tishio katika siasa za Tanzania iwapo watajikita kuwania nafasi za uongozi.Majina yao siyo geni. Ni majina ambayo tumeyazoea na uwezo wao unafahamika. Mwankijiji ni moyo wa JamiiFourms. Anaibua mijadala mizito na kuweza kuyatetea. Niseme tu kwa kifupi kwamba MMwanakijiji ni mwiba wa Mafisadi na adui mkubwa wa ufisadi. Anaipenda nchi yake. Mwanakijiji na Mashaka ni tishio kwa viongozi wa juu CCM, hasa wana CCM wanajiona kwamba ni "Estabslishment"

Ingawa wengi hawamjui Mzee Mwanakijiji kwa sura, ila kutokana na uzalendo wake, watanzania ndani na je ya nchi wanamkubali. Ni jembe la uhakika. John Mashaka ni kijana na jasiri ambaye wengi wanamfahamu. He is gifted and very articulate. 2009, nilimuona Kinondoni-Biafara, nilimkubali. Ana kipaji. Ni kichwa na hilo halina swali wala ubishi. He is "intelligent" na ana uzoefu mkubwa kitaaluma kiasi cha kuweza kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya nchi

Ni kijana mwenye bidii na machungu na Tanzania. Kama alivyo mwanakijiji. Bila shaka uwezo wake kuchambua maswala ya kiuchumi na kisiasa utauwezesha upinzani kukua kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Kuwepo kwa Mwanakijiji na Mashaka kutawaletea hamasa na changamoto nyingi watanzania wanaopoteza matumaini na uongozi wa serikali dhalimu ya CCM.

Kwa lugha nyepesi, kwa sasa hivi, mwana siasa nje ya Dr. Slaa, ambaye yuko kwenye level ya Mwanakijiji na Mashaka ni Tundu Lissu. Tundu Lissu ndiye Jembe ambaye anaweza kujenga hoja na kukabiliana na hao magwiji wawili. Itakuwa vyama chama chochote pinzani makini ikawakamata hawa vijana wawili mapema. CUF au CDM inabidi iweke jitihada kuwavuta hawa vijana wawili kwa maana ni dhaabu kwa taifa letu. CCM haitawafaa kwani wana mawazo mbadala ambayo haitakiwi ndani ya CCM. CCM ni chama cha Mazingaombwe ufisadi kulindana na kurithiana vyeo
 
Hawa vijana wawili ni tishio katika siasa za Tanzania iwapo watajikita kuwania nafasi za uongozi.Siyo kwamba ni majina geni, ni majina ambayo tumeyazoea na uwezo wao unafahamika. Mwankijiji ni moyo wa JamiiFourms. Anaibua mijadala mizito na kuweza kuyatetea. Niseme tu kwa kifupi kwamba MMwanakijiji ni mwiba wa Mafisadi na audi mkubwa wa ufisadi. Anaipenda nchi yake. Haya majina mawili ni tishio hata kwa viongozi wa juu serikalini, hasa wana CCM wanajiona kwamba ni "Estabslishment" wao ni threat kubwa sana

Ingawa wengi hawamjui Mzee Mwanakijiji kwa sura, ila kutokana na uzalendo wake, watanzania ndani na je ya nchi wanamkubali. Ni jembe la uhakika. John Mashaka ni kijana mstaarabu na jasiri ambaye wengi wanamfahamu. Ni kichwa na hilo halina swali wala ubishi. He is “intelligent” na ana uzoefu mkubwa kitaaluma kiasi cha kuweza kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya nchi

Ni kijana mwenye bidii na machungu na Tanzania. Kama alivyo mwanakijiji. Bila shaka uwezo wake kuchambua maswala ya kiuchumi na kisiasa utauwezesha upinzani kukua kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Kuwepo kwa Mwanakijiji na Mashaka kutawaletea hamasa na changamoto nyingi watanzania wanaopoteza matumaini na uongozi wa serikali dhalimu ya CCM.

Kwa lugha nyepesi, kwa sasa hivi, mwana siasa kijana ambaye yuko kwenye level ya Mwanakijiji na Mashaka ni Tundu Lissu. Tundu Lissu ndiye Jembe ambaye anaweza kujenga hoja na kukabiliana na hao magwiji wawili. Itakuwa vyama chama chochote pinzani makini ikawakamata hawa vijana wawili mapema. CUF au CDM inabidi iweke jitihada kuwavuta hawa vijana wawili kwa maana ni dhaabu kwa taifa letu. CCM haitawafaa kwani wana mawazo mbadala ambayo haitakiwi ndani ya CCM. CCM ni chama cha Mazingaombwe ufisadi kulindana na kurithiana vyeo


Kwani lazima wawe wanasiasa ndio watumikie taifa lao?
 
Hao ni wapinzani by nature wapenda mabadiriko wataenda chama watakacho wakati ukifika ni kweli mada zao huwa zinaleta mjadala wa kitaifa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom