Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?

duh!katika wanamuziki wa zamani nawazimia sana M.mwishehe,Marijani,Bitchuka,TxMoshi,fresh jumbe,Dede ,Bushoke na Maneti lakini Marijani ni zaidi ya wote..
 
Mpaka mtu upewe jina la JABALI mana watu wamekubali mchango wako..Tungo za marijani zilikuwa nzuri na zenye maudhui..ndo mana baadhi ya nyimbo zilitumika kufundishia mashuleni.
 
Kwangu mie MARIJANI ni zaidi!! Tungo zake hadi tumefanyia mitihani ya kidato cha nne (MWANAMEKA)......Ukisikiliza nyimbo zake zimechangia sana katika kukuza matumizi fasaha ya kiswahili!! Hakuna wimbo wa Marijani usiokuwa na METHALI; NAHAU na MISEMO kadhaaa.....Kweli tungo zake zilikuwa SPECIAL.....RIP JABALI LA MUZIKI MARIJANI RAJABU (aka Bozza)
 
Mpaka mtu upewe jina la JABALI mana watu wamekubali mchango wako..Tungo za marijani zilikuwa nzuri na zenye maudhUi..ndo mana baadhi ya nyimbo zilitumika kufundishia mashuleni.

Mwanameka!
 
Mbaraka is the best musician ever. Wakuu, to me, huyu mtu alikuwa na sifa zote za mwanamuziki na hakuwa na wakumfananisha. nyimbo zake zote, mbali na uzuri wa melodies alizotumia, zilikuwa na mafundisho mazuri sana katika maisha ya kawaida na ungeweza na unaweza kuzisikiliza na watoto waka/ wazazi wako/ wakwe zako n.k bila kutafuta sehemu ya kujificha ama kuwa na remote mkononi.

Last edited by a moderator:
Kwangu MARIJANI ni zaidi! Napenda kusikiliza mara kwa mara nyimbo Bwana Mashaka Tamaa Mbele, Dunia Uwanja Wa Fujo, Masudi, Namsaka Mbaya Wangu, Ndoa Ya Mateso, Pombe Si Chai, Rufaa Ya Kifo, Sikitiko, Talaka Kampa Nani, Tuishi Kwa Furaha, Ukatili Ni Unyama, Uke Wenza, Usia Wa Baba na Walimwengu
 
Hapo kwenye pombe si chai katoa elimu kwa wanaoanza pombe, wasije kuishia pabaya.
 
Binafsi na mkubali sana Marijani, nyimbo zake zilikuwa na ujumbe mzuri zaidi Mfano Zuwena, Ukewenza, Masudi, wosia, Mwanameka, Vicky, Pondamali nk. Sina maana kuwa Mubaraka hakuwa na tungo nzuri bali ni ushabiki wangu tu.
Kati ya hawa miamba wawili, ni yupi alikuwa na tungo nzuri zaidi ya mwenzie? Pia sauti ya nani ilikuwa na mvuto zaidi?
 
Last edited by a moderator:
Ingawa sikuwepo lakini namsikiliza sana Marijani.
Jamaa alikua jembe sana,pia na Ndala Kasheba-Marashi ya pemba bado inakimbiza.
 
Ingawa sikuwepo lakini namsikiliza sana Marijani.
Jamaa alikua jembe sana,pia na Ndala Kasheba-Marashi ya pemba bado inakimbiza.

Mkuu Marijani amefariki mwaka 1995 bado tu ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa hujajitambua bado?
 
kinachomfanya marijani kuwa juu ya Mbaraka Mwinshehe ni aina ya tungo zake.. Tungo za marijani ni sawa na hadithi.. Mara nyingi tungo zake zilianza na A na kwisha na Z.. Kama mnaufahamu wimbo wake wa ndoa ya mateso ndo mtaelewa ninamaanisha nini.. Pia alikuwa anaingiza sana nahau na methali kwenye nyimbo zake.. Kitendo cha mashairi ya wimbo wake wa mwanameka kutumiwa kwenye mtihani wa kitaifa wa form 4 mwishoni mwa miaka ya 80 (au mwanzoni mwa 90) ni kielelezo tosha kwamba Marijani ni nguli aliesimama pekee juu..
Maneti hakustahili kuwepo kwenye hili kundi..
 
Mkuu Marijani amefariki mwaka 1995 bado tu ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa hujajitambua bado?

Mkuu wakati anakumbana na umauti Marijani alikuwa ameacha kupiga dansi.. Alikuwa na duka lake ambalo alikuwa anauza nyimbo zake pamoja na nyimbo toka kwa wasanii wengine tofauti.. Kama ninakumbuka sawasawa competitive musik aliachana nao kwenye mwaka 1987 hivi (I stand to corrected)..
 
kinachomfanya marijani kuwa juu ya Mbaraka Mwinshehe ni aina ya tungo zake.. Tungo za marijani ni sawa na hadithi.. Mara nyingi tungo zake zilianza na A na kwisha na Z.. Kama mnaufahamu wimbo wake wa ndoa ya mateso ndo mtaelewa ninamaanisha nini.. Pia alikuwa anaingiza sana nahau na methali kwenye nyimbo zake.. Kitendo cha mashairi ya wimbo wake wa mwanameka kutumiwa kwenye mtihani wa kitaifa wa form 4 mwishoni mwa miaka ya 80 (au mwanzoni mwa 90) ni kielelezo tosha kwamba Marijani ni nguli aliesimama pekee juu..
Maneti hakustahili kuwepo kwenye hili kundi..

Mkuu unachosema ni sahihi kabisa, nyimbo za Marijani sio burudani tu ni darasa kabisa, halafu pia zina mtiririko fulani ambao unaleta ladha wakati wa kusikiliza. Hiyo Mwanameka nadhani ilitoka NECTA form four 1993.
 
Back
Top Bottom