Nani yupo sahihi kati ya hawa?

Dungulee

Member
Oct 23, 2008
17
1
Habari wana JF.
Mimi napenda kufahamishwa kuhusiana na hili neno SHELI.
Maranyingi huwa nasikia watu wakisema "Tukutane pale Sheli Bamaga"ama wengine kama makonda husema "Buguruni Sheli mwisho" na vinginevyo.Inamaana hivi vituo vya mafuta vyote kama BP,Oryx,OilCom na vinginevyo kwa neno moja ni SHELI?
hata waandishi wa habari maranyingi huwa nakuta kwenye magazeti wanatumia neno SHELI katika baadhi ya matukio wanayozungumzia wakati sijawahi ona mahali pa kituo cha mafuta kumeandikwa SHELI.nahitaji kuelimishwa kuhusiana na hilo.NAWAKILISHA
 
Kuna kampuni ya usambazaji mafuta ilikuwa ikiitwa SHELL, sina hakika kama bado ipo ulimwenguni lakini ilikuwepo hapa nchini na kwa mazoea watz mpaka leo kila kwenye kituo cha mafuta/gasi hupaita SHELL
 
bRAVO MKUU!

Azikiwe we ni Mkongwe mwenzangu nini, maana wengi wa hawa vijana wa kisasa hawakuwahi kuiona kampuni hii ikiwa hai!
Na hiyo uliyoweka ndo nembo yake haswaa!
Hii ni moja kati ya kampuni za kwanza hapa nchini, ndo maana jina hilo limekuwa linatumiwa kuwakilisha kituo cha mafuta(japo ni makosa)!
 
Hii ni sawa tu kama vile pikipiki za matairi matatu zote zinaitwa Bajaj. Na baada ya muda ilo jina litang'ang'ania hapo hapo. Huenda BAKITA wakayatohoa hayo manaeno kama yalivyo. Bisha!!!!!!!!!!
 
kwa sasa kuna vituo vingi vya mafuta lakini hapo mwanzo (zamani), palikuwa na AGIP, TOTAL, BP na SHELL, kwa upande wa dar SHELL ilikuwa ni dominannt sana, sasa ikafikia point kila kituo cha mafuta watu wanakiita shell, na hiyo ndio iliyosababisha mpaka leo vituo vya mafuta kubaki na jina hilo la shell
 
Swadakta mkubwa !! Kijana hayo majibu uliyopewa uya bold, zamani wakati wa majina haya yanatamba tulikuwa tunasema pigia msitari, pale ambapo unakuwa umepewa majibu mazuri kama hayo.
 
Ni kama mnyamwezi (old school wengi) anavyoweza kusema "I am going to Xerox this" akimaanisha anaenda ku photocopy.

Au kusema I like that walkman, while walkman is a Sony brand and not every "walkman" is a Walkman.

Not to advocate imprecision, lakini haya mambo yapo the world over.
 
Kuna kampuni ya usambazaji mafuta ilikuwa ikiitwa SHELL, sina hakika kama bado ipo ulimwenguni lakini ilikuwepo hapa nchini na kwa mazoea watz mpaka leo kila kwenye kituo cha mafuta/gasi hupaita SHELL

Duh! unanikumbusha enzi za "jamaa kanunua mobitel" akimaanisha jamaa kanunua simu ya mkononi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom