Nani yupo nyuma ya Mary Chitanda?

Jina hilo la CHITANDA ni jina la Watanzania wanaoishi pale LINDI kusini mwa taifa letu.

Na huyu Mary Chitanda wa Arusha, kwa CCM ameonekana Mtanzania mmoja hivi mwenye uwezo wa ajabu kiutendaji hata akapewa:

1. Ukatibu Mkuu CCM Mkoa wa Arusha,
2. Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Tanga,
3. Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Dodoma,
4. 'Mjumbe wa Kukodi' kuchagua Meya Mkoa wa Arusha,
5. Na sasa Makamba anatafuta kutuaminisha kwamba baada ya BALAA LA ARUSHA huyu mama sasa ni Diwani pia Arusha.

Jamani Watanzania na Wana-JF sasa unganisheni hizo dots ...
 
Mkulima hujaongea ukweli..japo una uelewa mpana
Hata mfano uliyozungumzia kwa CDM siyo sahihi..

Mkuu,

Tusaidie kwa kueleza wapi sijaongea ukweli. Lengo ni kufundishana na wala sio mabishano.

Nitashukuru ukinionyesha nilipokosea ili nijifunze.

Tukitaka kupambana na katiba mbovu, ni muhimu kuielewa vizuri. Vinginevyo tutatoana ngeu kwa mambo ambayo yanaweza kufafanuliwa kirahisi sana.
 
Kweli nimeamini sasa JF hamna great thinkers bali kuna Great Stinkers kwanza nimesoma post nyingi hapa hakuna hata moja inayosema kuwa Mary Chitanda amekosea nini zaidi ya kumlaumu tu na kumtishia. Pili yeye kama mbunge na Katibu wa CCM Arusha huo ndio ulingo wake aliyoyasema yeye ni sahihi kabisa na namsupport 100% ukitaka mtu mie ni wa kwanza. Pia wote mnalaumu mnashindwa kuwalaumu maaskofu walioingilia kazi zisizowahusu kwa kujifanya wao ndio waamuzi wa wanaArusha. Poleni sana Mary ataendelea kuwa Katibu na Mbunge.
 
Hana hata mvuto wa kutembea na mtu, ANAROPOKA KWA SABABU YA UDHAIFU WA MWENYEKITI WA CCM MKOA AMBAYE NI DARASA LA SABA ALIYEWEKWA NA LOWASA NA PIA UDHAIFU WA CCM TAIFA NA MPARANGANYIKO WAKE...

CCM IS DEAD PEOPLE......
 
wakuu,

Nimefafanua kwenye thread nyingine. Hakuna mbunge viti maalum anayewakilisha mkoa. nafasi kama hiyo haipo kikatiba wala NEC haina wabunge wa namna hiyo.

Kuchaguliwa kupitia mkoa ni utaratibu ndani ya CCM. Kama ambavyo CHADEMA walitumia vigezo vya elimu na ushiriki kwenye chama, CCM wanatumia makundi mbalimbali likiwemo hilo la mikoa, NGO, walemavu, vyuo vikuu nk.

Ikiisha uchaguzi ndani ya CCM hao wote wanapelekwa NEC majina yao na namba walizopewa hakuna cha kwamba huyu kapitia mkoa au NGO au vyuo vikuu.

Wakiteuliwa na NEC wanaitwa wabunge viti maalum CHADEMA au CCM au CUF.

Hilo la kwamba yeye ni mbunge wa viti maalum Tanga ni confusion ambayo imekuja kwasababu tu ndani ya CCM aligombea kundi la mkoa.

Kikawaida ungetegemea halmashauri akashiriki Tanga kwasababu angelikuwa anaishi huko au ana interests zaidi huko. Lakini huyu mama anafanya kazi Arusha, alikuwa anaishi Arusha hata kabla ya uchaguzi. Kweli mnaona ina make sense awe anasafiri kila wiki km zote hizo kwenda Tanga kuhudhuria vikao wakati kisheria anaruhusiwa popote?

(Swali kwanini aliomba Tanga kuwakilisha akina mama wa huko???? na kwanini hakuomba Arusha???)


Kama kuna wabunge viti maalum wanaowakilisha mkoa, nijulishe upande wa CHADEMA ni akina nani hao?

Hii sheria CHADEMA wenyewe wameitumia kule Hai sasa nashangaa kwanini wanaona hili suala la huyu mama ni tofauti?

Hii sheria ilitungwa wakati hakuna upinzani lakini kwa jinsi upinzani ulivyo sasa itabidi irekebishwe au iongezewe definition. (Hatuhitaji clear definition ila tunahitaji sheria hii ibadilishwe kwani haiwatendei haki wananchi waliowachagua)

Mkulima nashukuru kwa ufafanuzi wako, mie nilikuwa si ilewi vizuri hii issue ya Chitanda! Issue hapa sasa ni kuwa Katiba inahitaji mabadiliko makubwa (Major ovahoul) kwani kama ulivyosema kama hicho kifungu kinadefinition ni hiyo then sizani kama kuna haja ya kuwa na WABUNGE WA VITI MAALUM maanake inaonekana kama kuwa hawako accountable kwa wale wanaowawakilisha kisheria!!!! Mimi nilitegemea kama Rita Mlaki anawajibika kwa NGO's kisheria na vilevile NGO's hawajui kama yeye ndie mwakilishi wao na yeye anaona kama hayuko accoutable kwao then hakuna haja ya kuwa na nafasi hizi, it's a wastage of our resources to finance this group at all it should be abolished at all cost!!!!.
 
Mkulima nashukuru kwa ufafanuzi wako, mie nilikuwa si ilewi vizuri hii issue ya Chitanda! Issue hapa sasa ni kuwa Katiba inahitaji mabadiliko makubwa (Major ovahoul) kwani kama ulivyosema kama hicho kifungu kinadefinition ni hiyo then sizani kama kuna haja ya kuwa na WABUNGE WA VITI MAALUM maanake inaonekana kama kuwa hawako accountable kwa wale wanaowawakilisha kisheria!!!! Mimi nilitegemea kama Rita Mlaki anawajibika kwa NGO's kisheria na vilevile NGO's hawajui kama yeye ndie mwakilishi wao na yeye anaona kama hayuko accoutable kwao then hakuna haja ya kuwa na nafasi hizi, it's a wastage of our resources to finance this group at all it should be abolished at all cost!!!!.

Mkuu,

Hayo uliyoyaandika hapo juu ndio tunatakiwa kufanya. Viti maalum ni balaa tupu na sioni sababu ya wao kwenda kwenye halmashauri. Halmashauri zingeongozwa na madiwani wa kuchaguliwa, madiwani wa kuteuliwa na mbunge wa jimbo.

Hili suala linafanana na hilo uliloliandika la mama Mlaki kuwa mwakilishi wa NGO huko chama kinachowakilisha NGO kikiwa hakina habari. Ukweli nako hakufanya makosa maana yeye anawakilisha NGO za wana CCM na sio muungano wa NGO lazima ujue au uwe unaitambua NGO yake. Kama ana NGO ambayo imesajiliwa kisheria na ni mwana CCM basi ana qualify.

Nafikiri CCM wapunguze haya makundi kwani yanawaletea matatizo bure. Walitaka kuwa inclusive lakini inazua matatizo mengine.

Kwanza viti maalum ni vingi mno na vingepunguzwa na nafasi chache zinazokuwepo ziende kwenye yale makundi ambayo kweli yanahitaji kusaidiwa.

Tatizo hili la Arusha kama kungelikuwa na chombo neutral cha kuchambua katiba wala tusingelifika hapa tulipo maana ni kama sheria ziko wazi hata kama ni mbovu bado ni sheria.

Hilo la kugombea Tanga nafikiri ni ukabila ambao unaikumba TZ kwasasa ukiachia maeneo machache ya mjini. Aliona akipambana na akina Sokoine wa Arusha, angebwagwa chini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom