Siri nyuma ya sura nzuri

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,107
52,832
KISA CHA MUUAJI MJANJA
Uchunguzi wa kimaabara na matukio ya uhalifu.

Siku moja wakati wa ibada ya jioni, mtu mmoja aliyeitwa Steve A. Robards mwenye umri wa miaka 38 alianza kuhisi dosari mwilini mwake. Baadaye usiku alifariki kwa‘shambulio la moyo’ au kwa lugha nyingine ‘Heart Attack.

Iweje mwanaume wa miaka 38 afariki ghafla kwa shambulio la moyo?

Mwaka mmoja baadaye, mtoto wa kike wa Steve Robards aitwae Dorothy Mary robards alikuwa darasani akisoma kitabu kinachoitwa ‘Hamlet’ kilichoandikwa na William Shakespear.

Hamlet ni neno la kiingereza lenye maana ya kijiji kidogo, kisichokuwa na nyumba ya ibada. Ndani ya kitabu hicho, binti huyo alikuta mstari wa maneno yaliyotamkwa na

Mfalme Claudius kuhusu Kifo, Chuki, Hatia na Visasi. Mfalme Claudius alisema;
“My words fly up; my thoughts remain below. Words without thoughts, never to heaven go”. Maana yake, “Maneno yangu hupaa angani, Fikra zangu hubaki chini, Maneno bila kuambatana na fikra, hayatupeleki mbinguni”
Ndani ya maneno hayo, binti alianza kufikiria upya kifo cha baba yake.

Dallas ndio mji mkubwa zaidi katika jimbo la Texas nchini Marekani. Ni mji maarufu kwa mauaji ya Rais John F Kennedy yaliyofanyika mwaka 1963 katika eneo la Dealey Plaza. Steven Robards (38) alikuwa mkazi wa Texas aliyekuwa ameachana na mkewe siku chache zilizopita na wakati huo akiishi na mpenzi wake mpya Sandra Hudgins. Steve alifanya kazi katika shirika la Posta na aliipenda sana kazi yake. Binti yake, Marie, hakuwa na wakati mzuri na rafiki mpya wa kike wa baba yake kwa kuwa waliishi katika nyumba yenye chumba kimoja tu cha kulala. Akiwa na umri wa miaka 16, Marie alijiunga na shule ya sekondari ya Eastern Hills, baada ya kufaulu kwa alama za juu. Uhusiano wa Marie na baba yake ulikuwa mzuri sana, lakini mnamo Februari 17,1993 uhusiano huo ulibadilika.

Siku hiyo, Bw. Steve Robards, alimaliza kula chakula cha jioni na kuamua kwenda kufanya ibada ya jioni. Aliporudi nyumbani aliwaambia mpenzi wake na binti yake kwamba hajisikii vizuri. Baada ya muda alianza kusikia tumbo likikata na kuuma kwa nguvu. Maumivu yaliongezeka kadiri muda ulivyokwenda. Hali ilivyozidi kuwa mbaya, Sandra na Marie waliamua kupiga simu kwa namba 911 ili kupata huduma ya dharura. Gari la wagonjwa lilifika nyumbani kwa Steven Robards akiwa amekwisha fariki dunia.

Uchunguzi wa kitabibu kwa mwili wa Steven ulitoa sababu ya kifo kuwa ni Shambulio la Moyo, sababu ambayo Maafisa wa Polisi hawakuiamini sana kulingana na maelezo kwamba Steven alivyokuwa akilalamika maumivu ya tumbo na zaidi alikuwa kijana wa miaka 38.

Baada ya kifo cha Steven Robards, Marie alikwenda kuishi na babu na bibi yake na hivyo kuamua kuhama shule. Baada ya kumaliza shule, Marie alitumia kiasi cha dola 60,000 kujiunga na chuo kikuu cha Texas, fedha alizopata kama urithi kutoka kwenye mfuko wa bima ambao baba yake alijiunga. Alichukua masomo ya udaktari wa mwanzo (Pre Med) kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuwa mtaalamu wa magonjwa (Pathologist). Akiwa mwaka wa kwanza, aligundua kuwa maafisa wa Polisi walikuwa wakichunguza kifo cha baba yake. Maafisa wa polisi walijiuliza iweje mtu mwenye miaka 38 afariki kwa maradhi ya Shambulio la moyo?

Stacey High, rafiki wa Marie katika shule aliyohamia baada ya kifo cha Baba yake, anasema Marie alikuwa na akili sana, alikuwa anajiamini, nadhifu, mchangamfu na mwenye haiba ya kupendeza. Lakini Stacey alidhani kwamba, sifa hizo za Marie zilikuwa kama ni namna ya kuficha jambo fulani katika maisha yake. Walipokuwa shuleni, Stacey na Marie walitakiwa kusoma kwa sauti kitabu kilichoitwa Hamlet, mbele ya darasa wakati wa kipindi cha somo la kiingereza. Wakati wakisoma kitabu hicho, Stacey alianza kwa kusoma kipengele ambacho kilielezea namna mfalme Claudius alipokuwa akitubu kwa kosa la kumuua kaka yake aliyeitwa Mfalme Hamlet. Claudius alimuua kaka yeka ili autwae ufalme, na sasa akiwa mfalme anajaribu kutubu dhambi ya kumuua kaka yake. Lakini baadaye Claudius anagundua kuwa toba yake haina maana kwa sababu bado anafurahia ufalme ambao ni matunda ya kumuua kaka yake. Kivipi atubu wakati bado anamiliki na kuufurahia ufalme ulitokana na kosa la kuua? Baadaye mfalme Claudius anamuomba Mungu radhi kwa kuwa hawezi kutubu, kwa sababu dhambi aliyotenda bado inaendelea kumnufaisha. Baada ya Stacey kusoma kipengele hicho, ilifika zamu ya Marie, ambaye alisita, akabaki na mawazo kisha akaanza kulia.

Baada ya kipindi, Stacey alimuuliza Marie, “una tatizo gani rafiki? Kuna jambo lolote linalokusibu?” Marie akajibu – ‘Ndiyo’.
-Una ujauzito?
-Hapana.
Kadiri muda ulivyopita Marie aliendelea kukosa raha kwa siri aliyotunza moyoni. Siku moja aliamua kumwambia rafiki yake kuwa alimuua baba yake mzazi. Marie alimuomba Stacey atunze siri hiyo.

Enzi hizo akiishi na baba yake, Marie aliiba sumu kutoka katika maabara ya somo la kemia ya shule alipokuwa akisoma. Kemikali hiyo inapotumiwa huleta dalili za shambulio la moyo. Wiki mbili baada ya kuiba sumu shuleni, Marie alimuandalia chakula cha ki-Mexico baba yake na kumuwekea sumu ile. Chakula hicho cha ki-Mexico kina ladha inayoficha ladha ya sumu ile. Baada ya kula, baba yake Marie, Steven aliaga dunia masaa machache baadaye kwa sababu iliyoonekana kuwa ni ‘Shambulio la Moyo’

Siri hiyo iliyomkosesha amani Marie, ilianza kumkosesha amani Stacey aliyeapa kuitunza. Stacey alijua endapo atafichua siri hiyo, basi rafiki yake atahukumiwa kifo au kuishi gerezani kwa muda wote wa maisha yake. Mawazo na doto za ajabu zilimwandama Stacey. Siku moja akiwa ndotoni alisikia sauti ya baba yake Marie ikitoka kaburini. Katika ndoto nyingine, Stacey aliota akikimbizwa na Marie usiku kucha. Ndoto hizo za mara kwa mara zilimfaya Stacey apoteze muelekeo shuleni na zaidi ilimbidi Stacey aamue kumuona daktari wa afya na maradhi ya akili. Baada ya miezi nane ya kutunza siri, Stacey High alishindwa, akamsimulia mama yake, mlezi wake wa shuleni, na baadaye maafisa wa polisi.

Mara tu baada ya kupewa siri hiyo maafisa wa polisi waliamua kwenda kufanya upekuzi katika maabara ya shule aliyokuwa akisoma Marie hapo awali. Katika kitabu cha orodha ya vifaa vya maabara waliugundua kuna karatasi ime chomolewa. Karatasi hiyo ilikuwa ikieleza namna sumu aliyo iba Marie inavyofanya kazi, jinsi ya kuitumia na hatua za kuchukua kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtu aliyetumia sumu hiyo.

Maafisa waliwahoji wataalamu wa afya kuhusu kutokujulikana kwa sababu hiyo ya sumu katika uchunguzi wa kitabibu ulio fanywa awali kwa mwili wa Steve. Wataalamu wa afya walieleza kuwa, yalihitajika maelezo zaidi ili kufikiria kuhusu sumu, ingawa walifanya uchunguzi kwa baadhi ya sumu. Lakini sumu iliyotumika ilihitaji uchunguzi wa hali ya juu kuweza kuigundua, na zaidi mashine iliyohitajika haikuwepo hospitalini hapo kwa sababu ni mashine ya gharama kubwa, takribani dola 150,000. Wataalamu wa afya walijitetea zaidi kuwa, wazo la kuichunguza sumu hiyo ni geni, na hakuna wazo la kununua mashine inayotumika kwa uchunguzi huo. Pia maelezo ya ndugu na maafisa wa polisi hayakuwapa sababu ya kuichunguza sumu hiyo.

Teknolojia inayotumika kuchunguza uwepo wa sumu katika tishu za binadamu inaitwa ‘Mass Spectrometer Gas Chromatography’.

Kwa kuwa Marie aliamua kujiunga na masomo ya udaktari ili aje kuwa daktari bingwa wa patholojia au Pathologist (elimu ya tabia ya magonjwa). Maafisa wa polisi wali amini kuwa Marie anafahamu vema vipimo vilivyokuwa vikifanyika katika hospitali ndogo walipo chunguza mwili wa baba yake. Bila shaka alifahamu ni sumu gani haiwezi kuonekana kwa vipimo hivyo. Kwa kuwa kesi ya kifo cha Steven Robards haikuwa imefungwa, wataalamu wa afya walitunza sehemu za tishu zake katika jokofu maalumu la kuhifadhi viungo na tishu za watu waliokufa kwa utata, kwa faida ya baadaye ikiwa uchunguzi utaendelea. Wapelelezi waliamua kuchukua tishu hizo na kuzipeleka kwenye maabara binafsi huko mjini Pennysylvania. Katika maabara hiyo, tishu hizo zilifanyiwa uchunguzi kwa kutumia teknolojia ya ‘Mass Spectormetry Gas Chromatography’.

Kwa kutumia teknolojia ya Mass Spectrometry Gas Chromatography, tishu za mwili wa binadamu huvunjwavunjwa na kupatikana molekyuli ambazo hufanyiwa upembuzi. Kisha matokeo huonekana katika grafu inayoeleza aina ya kemikali zilizopo kwenye tishu, wingi wa kemikali na muda unaohitajika kwa kemikali kuonekana kwenye tishu tangu iingie mwilini. Katika sampuli ya tishu za Steven Robards, ilionekana kemikali-sumu ambayo Marie alimueleza Stacey kuwa aliiba na kumuwekea baba yake kwenye chakula. Ilikuwa kemikali aina ya ‘Bariamu Acetate’.

Kiasi cha kemikali ya ‘Barium Acetate’ kilichokutwa kwenye tishu za Steven Robards kilikuwa kikubwa sana, mara 28 ya kiasi cha dozi kinachotosha kuua. Taarifa hizo zilimfanya Afisa wa upelelezi – Det. Thomas Boetcher kuendesha gari hadi chuo kikuu cha Texas kumchukua Marie Robards. “Alikuja akiwa na shahuku ya kutaka kujua ujumbe niliokuwa nao, nikamwambia, uko chini ya ulinzi kwa tuhuma za kumuua baba yako mzazi Steven Robards”. Anasimuli Det. Boetcher.

Marie hakujibu kitu, alisimama wima asijue cha kufanya. Hakubisha wala kusumbua mtu yeyote. Alikubali.

Maafisa wa upelelezi walitaka kujua kichocheo kilichopelekea Marie kumuua baba yake. Marie alidai kuwa alitaka kuishi na mama yake ambaye aliachana na baba yake. Lakini mara baada ya baba yake kufariki, mama yeka Marie ambaye alikwisha olewa na mume mwengine alihamia Florida bila kumtaarifu Marie. Jambo hilo lilipelekea Marie kwenda kuishi na babu na bibi yake.

Pamoja na kukiri kosa mbele ya maofisa wa polisi, alipofikishwa mahakamani Marie alikana mashitaka, akidai kuwa hakupanga kumuua baba yake. Marie aliiambia mahakama kuwa hakukusudia kumuua baba yake. Alikubali kuwa aliiba kemikali – sumu kutoka shuleni, na alikiri kuwa alimuwekea baba yake kemikali-sumu ile kwenye chakula, lakini alijitetea kuwa hakupanga kumuua bali kumfanya augue tu. Marie aliongeza kuwa angeweza kuondoka na kwenda kuishi na mama yake baada ya baba yake kuanza kuugua.

Wapelelezi walisema kuwa Marie alikuwa na uwezo mkubwa katika masomo ya sayansi darasani, na kwa sababu hiyo alijua kuwa kemikali-sumu ile inaweza kusababisha kifo. Na zaidi alitumia dozi kubwa, mara 28 ya kiasi cha dozi kinachotosha kusabaisha kifo. Wapelelezi waliongeza kuwa, Marie alisimama pembeni akimungalia baba yake anavyokata roho, bila kuchukua hatua yoyote.

Sababu ya kukiri mbele ya Maofisa wa upelelezi, sababu ya kumueleza rafiki yake na kumuomba kutunza siri, sababu ya kukiri kuiba kemikali - sumu shuleni, na sababu ya ushahidi wa kimaabara zilitosha kumtia hatiani. Mei 9, 1995 mahakama ilihitaji nusu saa tu kumkuta Marie Robards na hatia. Marie alihukumiwa kifungo cha miaka 27.

Dr. Marc A. Krouse, mtaalamu wa uchunguzi wa kimahakama eneo la maabara (Forensic Lab. Scientist) alimuita Marie Robards, muuaji mjanja.

Ali hukumiwa Mwaka huo, lakini Ina semekana ali achiwa Mwaka 2003 na ali ishi maisha mapya kwa utambulisho mwingine.
download (18).jpeg
download (19).jpeg
 
View attachment 2897935View attachment 2897936
Dah kweli binadamu wabaya ,mdada kamuua mdingi wake
 
Back
Top Bottom