Nani ni mtanzania wa kawaida?

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Ndugu wadau kwa muda mrefu viongozi wetu wmekuwa wakitumia neno "Mtanzania wa kawaida" kila walalamikiapo jambo lolote la hovyo linapotokea hapa Tanzania Mifano: Mfumuko wa bei wanaseama anayeathirika ni mtanzania wa kawaida, ongezeko la bei ya umeme muathirika ni mtanzania wa kawaida, mgomo wa madactari muathirika ni mtanzania wa kawaida.

Mtanzania wa kawaida ni yupi na asiye wakawaida ni yupi? Nini kinawatofautisha? Kwanini hawa viongozi wetu wanajitoa katika kundi la watanzania wa kawaida?
 
Yeyote ambaye anakubaliana nao bila ya kufikiria madhara yake. Akipewa kanga, T-Shirt na soda amefuraaaaaaaahi. Ukiwa unauliza uliza basi wewe si mtanzania ila utaitwa mhamiaji toka burundi au kenya au hata uarabuni. Usinitaje kuwa nimekuambia.
 
Mtanzania wa kawaida kwa uelewa wangu ni mtanzania ambaye anaishi katika maisha ya umaskini, asiyekuwa na sauti,aliyekosa mtetezi, ni mtanzania ambaye huathirika haraka pale mabadiliko yanapotokea hasa ya kisiasa, kiuchumi.
 
'Mtanzania wa kawaida' is a commonplace phrase referring to grassroot people who invariably fail to make ends meet. It is unofficial translation of an English phrase 'an average citizen'. So anyone who lives very common life as opposed to wealthy elite's luxurious lives has this phrase reserved for them.
 
Mtanzania wa kawaida kwa uelewa wangu ni mtanzania ambaye anaishi katika maisha ya umaskini, asiyekuwa na sauti,aliyekosa mtetezi, ni mtanzania ambaye huathirika haraka pale mabadiliko yanapotokea hasa ya kisiasa, kiuchumi.

Asante kaka !
 
Back
Top Bottom