JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
Habari wanajamvi?
Niende Moja Kwa Moja kwenye hoja ya msingi.
Kwa muda sasa KATIBA YA JMT imekuwa ikivunjwa na wana Siasa kadiri wanavyo penda bila kujali viapo vyao.
Swali ninalo jiuliza ni kwamba ni nani hasa ni mlizi wa KATIBA yetu?
Binafsi nimeshuhudia Rais Magufuli akivunja KATIBA mara kadhaa Kwa makusudi kabisa wakati aliapa kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Kwa moyo wake wake wote.
Juzi tena nimeshuhudia Rais Samia Suluhu Hassan akivunja Kwa makusudi au Kwa kutokujua, sasa najiuliza mwenye dhamana ya kuilinda, kuihifadhi na kuitetea KATIBA yetu ni nani.
Kitendo Cha Rais Samia kukabidhi mamlaka aliyo pewa na KATIBA yetu Kwa waarabu ni kuvunja KATIBA
Kule kwenye Mkataba wa bandari Kuna kipengele kinasema; ikiwa huko mbeleni, TANZANIA itahitaji kuwekeza Nchi kavu, majini, au angani sharti wao DP world waambiwe kwanza ! Maana yake ni kwamba sehemu ya mamlaka ya Rais tumewakabidhi wao ili wawe wa amuzi wa mwisho wa mambo yetu.
Huko serikalini sioni mtu Wala taasisi wa kukabidhiwa jukumu hili nyeti. Ikiwa Rais ameshindwa , nani ataweza?
Bungee haliwezi kabisa maana ni bendera fuata upepo. Hiki chombo kimejuweka mfukoni mwa Rais.
Tutafakari Kwa pamoja, nani ailinde KATIBA yetu? Vinginevyo Hawa wanasiasa watatuchezea milele.