Nani Mkweli Juu ya Mauaji ya Polisi Ngara?

Kama unaamini UONGO wa huyo RPC basi wewe utaamini kila kitu hapa duniani including akina Vibwetele na
Kamanda Kova: Dr. Ulimboka alitekwa na kichaa kutoka Kenya aliyekwenda kutubu kwa mchungaji Gwajima.
ACP Changoja: Marehemu Mwangosi alipigwa na kitu kizito kilichorushwa na wafuasi wa CDM.

Ni Mjinga tu atakayeaamini taarifa hizi za POLISI.

Halafu watu wengine sijui huwa hamjifunzi, Hizi tume zimekuwa ndiyo KICHAKA cha KUFICHA UONGO NA DHULMA ZA POLISI DHIDI YA RAIA.
 
anayeamini taarifa zinazotolewa na jeshi la polisi kwenye matukio kama haya sijui yuko kundi gani la watu wavivu wa kufikiri !
 
Polisi, watasema hivyo huko ngara. Ukweli ndani ya jeshi lao somo lime eleweka, "usipige risasi hadharani, raia waua polisi, na kuchoma kituo" wana jf amini hiyo ndo lugha sasa wanaongea polisi nchini.
 
hakuna ubishi askari wameuwawa kinyama na askari wameua raia,cha msingi ni kusubiri tume ije ichunguze na kutoa mapendekezo na maoni kuhusiana na jinsi ya kushughulikia matukio ya aina hiyo yasitokee tena.pia katika matukio ya namna hiyo wapo baadhi ya watu wameona tukio zima na wapo tayari kutoa ushahidi.swala la nani anauwezo wa kuwasiliana na marehemu siyo issue,mbona usia wa marehemu unakubalika akisha kufa kama ushahidi sembuse madai ya mtu kutolewa kisu?.kama tunaweza kukubali usiwa wa marehemu kwanini tusikubali mambo mengine?.kama unaushahidi peleka ktk tume iliyoundwa usaidie,kama huwezi kufikisha ujumbe/ushahidi wako basi ukubaliane na majibu ya tume.

Mkuu, nayaheshimu sana mawazo yako kwa kuwa wewe ni gamba na umejitahidi sana kujenga hoja kwa kutumia Masaburi yako. Tume ya Dr. nchimbi?
 
tatizo la viongozi wa nchi hii kutunga uongo kwa kwa manufaa yao police badala ya kuwa walinzi wa raia wamekuwa wauaji wa raia na wakuu wao wanawatetea
 
hatuwezi kuupata ukweli kama kila mtu atakuja na uchunguzi kama wa kwako: Polisi maelezo yao mistari miwili na ya wananchi mengi kama ulivyofanya. Unatoa hoja na mwisho una conlude - polisi ni waongo..! Nadhani tutaupata ukweli pakiwepo na kitu huru cha kuchunguza na kuelezea tukio hili bila ya kuegemea upande wowote.
kuna uzi mwengine hapa mwanzilishi anasema aliepigwa risasi kapigwa wakati yuko njiani kupelekwa kituoni.polisi nao wakati flani ni madhalimu lakini baadhi ya wananchi nao ni wapenda shari.mimi siwezi kuamini hata mmoja mpaka nipate taarifa zilizotafitiwa ki taalam
 
Siku zote polisi ni waongo na wamefuzu katika kutunga na kusema uongo. Na bosi wao ndiye baba wa huo uongo.
Mwananchi akichomoa kisu ndo anapigwa risasi ya kichwa?

Nadhani huko kwenye vyuo vyao vya polisi hawafundishwi mafunzo ya ukakamavu, bali ni siasa za kuilinda ccm kwakuwa wanajua hata wakiua raia hakuna mtu wa kuwachukulia hatua.

Mkuu Mwita Malanya, serikali ya ccm haiwezi kuwachukulia hatua polisi wanaoua raia wema kwa sababu kwa sasa raia hwaitaki ccm na mambo yake yote. Hivyo kwa sasa raia mwema wa Tanzani ni adui wa ccm na kuuwawa kwa raia wema ni jambo la heri kwa ccm.
 
kuna uzi mwengine hapa mwanzilishi anasema aliepigwa risasi kapigwa wakati yuko njiani kupelekwa kituoni.polisi nao wakati flani ni madhalimu lakini baadhi ya wananchi nao ni wapenda shari.mimi siwezi kuamini hata mmoja mpaka nipate taarifa zilizotafitiwa ki taalam

Gamba kubwa wewe! Subiri taarifa ya watalaamu wa Dr. Nchimbi ndipo uamini
 
Kesi ya nyani kula mahindi anapelekewa nyani kuchunguza, unategemea nini. Maelezo ya shuhuda yana kaukweli kidogo ingawa inasemekana kuwa polisi walikuwa wanafuatilia pikipiki ambayo ilikuwa ya wizi. Walipofika eneo la tukio ambapo ni gereji, waliikuta pikipiki hiyo inatengenezwa. Walimfuata fundi aliyekuwa anatengeneza wakamwambia aipeleke ile pikipiki kituoni maana ni ya wizi. Yule fundi aligoma kwani yeye alidai ni ya mteja na ndipo askari alipomkwida na fundi naye akajibu kwa kumkwida askari. Katika hali ya kujitetea inasemekana fundi alimuuma askari shingoni na askari naye alipoona hali ngumu akamuamrisha mwenzake ampige risasi. Basi baada ya hapo ndipo maelezo ya shuhuda wa hapo juu yanakamilisha scene nzima.

Hivi hawa jamaa ndivyo wanavyofundishwa kudeal na watu wanaokataa kutii amri zao huko chuoni wanaposomea mafunzo ya kulinda usalama wa raia na mali zao?? Itabidi tumshauri mgeshi mkuu abadili utaratibu, maana polisi jamii imeshindwa, si tumeona jamii inaua mpaka RPC. Nakumbuka sana enzi za mwalimu, nidhamu ya majeshi yetu ilikuwa juu sana, sijui kwa kuwa walikuwa wanakaa kambini!! siku hizi yaani kila kitu vururu vururu.
 
gamba kubwa wewe! Subiri taarifa ya watalaamu wa dr. Nchimbi ndipo uamini
wewe ndo walewale wakiona kitu chochote kizuri au cha thamani wanasema cha ridhiwani na huwa hawatafiti wala hawaungi mkono utafiti.kuongea kwa emotion au kufanya mambo kwa emotion si sahihi.unaweza ukadhani kitu flani kipo halafu ukafanya maamuzi magumu halafu baada ya muda unagundua kumbe katika uhalisia kitu husika hakikuwepo na kinyume chake.
 
picha za matukio yanayohusina na mauaji yaliyosababishwa askari polisi katika kata ya Mugoma wilayani Ngara PC150203.JPG PC150203.JPG PC150220.JPG
 

Attachments

  • PC160247.JPG
    PC160247.JPG
    287.1 KB · Views: 55
Hi wanajamvi, na pole kwa wananchi wa Ngara kwa msiba huu wa kuuawa kwa RAIA.

Ndg, kwa kipindi cha mwezi mmoja kuna matukio zaidi ya 3 mkoani Kagera (Trh 5 Nov, 19 Nov, 28 Nov), Mawili kati ya hayo wananchi wanne wameuawa ama kwa uzembe au mpango mkakati wa Police. RPC na RC wanatakiwa waeleze polisi wanatoa wapi jeuri ya kutumia siraha mahali ampapo hata maneno achilia mbali kukamata yangeweza kufanya kazi.

Ndani ya wilaya hiyo hiyo ya Ngara, miezi kadhaa iliyopita wananchi kadhaa (wakulima) walichinjwa kama kuku na Wavamizi wa ardhi kutoka Rwanda, DC alihusishwa kwa kuhonjwa na wavamizi hao. Si RC au RPC wala hata waziri wa Ulinzi aliyeweza kutoa taarifa wala kuwajibika kwa jambo hilo. Waziri huyu alifika na kutoa ahadi kibao nzuri za kuchukua hatua kali kwa wahusika wote, sijui kama anakumbuka kwamba ahadi zile bado tunazikumbuka na kwamba hajatoa mrejesho wa utekelezaji wake??. Vitendo vya unyanyasaji wa wananchi vimekithiri, kila mwezi kuna tukio.
Tusisahau Mkuu wa Mkoa aliyepo sasa alipandishwa cheo kutoka Mkuu wa Wilaya kwa kazi eti NZURI ya kuua na kucharaza wananchi Wilayani kwake (wilaya aliyokuwa akiisimamia, Karagwe) na hatimaye CCM kupata ushindi kwa hila za wazi kabisa. Hivyo mauaji yakawa ni ngazi ya kupandia na kupewa fadhila.
 
Inasikitisha kwamba askari wetu wameuawa kikatili. natoa pole kwa familia zao. Lakini ukweli pia ni kwamba maaskari wengi wanaokuwa mipakani hasa Mugoma, Kabanga, Murusagamba na Rusumo wanjifanya Miungu watu. Hiingii akilini askari aliyefundishwa jinsi ya kumkamata raia hata kama ana silaha kumuua raia kwa sababu ya kisu tu ! Kitendo kilichofanywa na wananchi nina uhakika hakikusababishwa na kitendo cha kisu bali ni mrundikano wa vitimbwi amabvyo wananchi wamefanyiwa kwa muda mrefu bila kupata utatuzi. Vitendo vya polisi havifai na watapata matatizo wasipo jirekebisha.
 
Serikali hii haiwezi kuwa upande wa Raia. Je gereji hupelekwa kitu kizima au kibovu?

hapo ndipo tunapo hoji uwezo wa kufikiri wa baadhi ya tuliowakabidhi dhamana ya kutulinda,hivi kitu ni kizima kiende garage kikafanye nini?halafu hata siku moja ndani ya nchi hii sijawahi kusikia kuwa lilikua ni kosa la polisi rather kila siku wao ni wasafi,wao ndio wanaochokozwa,hivi ni kweli?au wanatuona watanzania ni wajinga wa highest level kabisa na wanaweza kutupumbaza watakavyo sio?
 
Huyu RPC ni kiboko, amejuaje hayo ya kutoleana visu na kupigana risasi wakati wahusika wote wawili wamefariki?
Au yeye ni kigagula na anaweza kuwasiliana na marehemu? mwaka huu tu unakwisha huku tukiendelea kushuhudia killa aina ya sinema kutoka policcm.
Kweli ni kiboko hawa policcm! Kwenye gazeti la Mwananchi j2 walisema walipompigia RPC ili kuthibitisha alisema yupo njiani kuelekea kwenye tukio akipewa habari kamili ataufahamisha umma nini kilitokea. Sasa hapa ndiyo napata shaka kwamba eti ameambiwa kuwa marehemu fundi alikataa kupeleka pkpk kituoni na akawatolea policcm kisu! Kweli jamani, polisi 2 wenye bunduki watishiwe kwa kisu( au panga)? tehetehe! IGP nafahamu umahiri wako lakini kwa ushemeji wako na JK UMEKUWA DHAIFU SANA!
 
kuna uzi mwengine hapa mwanzilishi anasema aliepigwa risasi kapigwa wakati yuko njiani kupelekwa kituoni.polisi nao wakati flani ni madhalimu lakini baadhi ya wananchi nao ni wapenda shari.mimi siwezi kuamini hata mmoja mpaka nipate taarifa zilizotafitiwa ki taalam

Taarifa zipi ambazo utazipata katika nchi hii zilizotafitiwa kitaalam ndugu? Ya Ulimboka, Ally Zona(Moro) Mwangosi, Taarifa zake unazo? na umeziamini? je kama uziamini unategemea taarifa za kitaalam zitoke wapi.
 
Polisi hawajipendi kabisa. Ingetakiwa sasa wao ndio wadai uchungunzi huru wa kimahakama kwa mujibu wa sheria. Hii itawasaidia kurejesha nidhamu ndani ya jeshi lakini pia kuaminiwa na wananchi. Kwa vitendo na kauli wanazotoa kila bahada ya mauaji tata haisaidii mustakabali wa taifa letu na serikali. Kwa maono ya karibu karibu serikali na jeshi la Polisi wanaweza kufikiria wanashinda, lakini hii inatupeleka papaya Kama taifa. Huku mitaani ni wazi kabisa watu hawaliamini tena jeshi la Polisi na mbaya zaidi inaenda hata kwa kesi zinazofikishwa mahakamani. Hii ni moja ya sababu ya wananchi kuchukua sheria mkononi. Bahati mbaya hatua hii pia uungwa mkono na Polisi kwa namna Fulani! Polisi daini kutumika kwa sheria ya uchunguzi wa Vifo vyenye utata kujisafisha na kuimarisha amani ya taifa na utaifa wetu.
 
Back
Top Bottom