Nani kawakimbiza wafanyabiashara wa nchi jirani kariakoo? TRA au wafanyabiashara wenyewe wa kariakoo kwa ulaghai?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,662
Hapa ndipo waandishi wa habari za uchunguzi wanatakiwa kuingia "chimbo". Wakawasake hao wafanyabiashara wa nchi jirani wawahoji.

Lakini, kinachoonekana wafanyabiashara wa kariakoo ndio wameiua kariakoo yao. TRA hawawezi kuhangaika na aliyelipa Kodi halali, wanashughulika na wakwepa Kodi.

Mfanyabiashara kaja kununua mzigo wa bilioni, mfanyabiashara wa kariakoo anamshawishi amuandikie risiti ya milioni 100 au 200, anaanza safari, TRA hawa hapa, wanamuhoji, anakiri thamani ya mzigo, wanaukamata, mtaji wa bilioni unakufa, unatarajia atarudi tena kariakoo?

Wafanyabiashara wa kariakoo, boriti ni kubwa sana kwenye mboni zenu, anzieni mlipojikwaa. Hao watu wa Congo, Rwanda, Burundi, na kwingine mmewapoteza kwa ulaghai wenu.

Uaminifu zero.
 
Mkuu wewe ndio haujielewi kwa kuwatetea TRA, na kwamfano ulio utoa basi badala ya TRA kukamata mzigo wa mgeni walipaswa wamuwajibishe mfanya biashara kwa kutumia ushahidi wa mgeni.

Hata kwa mfano ulio utoa, bado TRA atakua ndie amewafukuza wafanya biashara wa nje, badala ya kuwaelimisha na kuwalinda.

Kumbuka mfanya biashara wa Kariakoo sio jukumu lake kumuelimisha mgeni, bali ni wajibu wa TRA na serikali kumuelimisha mgeni/mteja ili kumlinda.
 
Asipoelewa hapa nawashauri hamna haja ya kuelekeza tena.
Mtoa mada. Huelewi hilo sakata hata robo.
 
Yes , upo sahihi kwa kiasi, japo TRA ni shida ila watanzania wenyewe sisi kikawaida ni watu wa kupinda pinda ata hiyo kodi nafuu inayoliliwa ikipatikana watu wataangaika kwa nguvu kubwa kukwepa kodi kadhaa
 
Kodi inakokotewa kwenye mtaji na faida uliona wapi haya mambo, chukua kodi kwenye faida na sio mtaji,
 
Tatizo kubwa hapa ni kanuni ya kukokotoa kodi! Kodi inakatwa kwenye gross profit! Hapo hapo TRA anashindwa kukusanya kodi kwa wadau wengine anampa mlipa kodi huyo huyo alipe kodi ya mtu mwingine! Kodi ya storage embu niambie mie sina godown nakodi namlipa mwenye godown tra hamfuati huyo ananisukumia mim nilipe kwa uvivu wake wa kwenda kumdai mwenye godown! VAT 18% nimenunua simu china kama ilivyo nikija kuuza natakiwa niongezee 18% hivi nimeongezea kitu gan au teknolojia gan mpya hapo ili thaman ya simu iongezeke unitoze hyo ziada!
 
Wakati nanunua mtama mwekundu sanga mwalugesha na kupeleka kigali miaka ya 1996 ulikua bado unatoka kamasi, leo uje unifundishe biashara? Elimu zenu za nadharia zinawafanya muwe wajinga msioishi kwa uhalisia,
Mkuu unaweza kua mkongwe na ukafundishwa biashara vizuri tu
 
Asipoelewa hapa nawashauri hamna haja ya kuelekeza tena.
Mtoa mada. Huelewi hilo sakata hata robo.
Usiwe na haraka sana ya kujitangazia ufalme.

Kuna sheria. Yeyote anayevunja sheria ni mharifu.

Huwezi kudai kwamba hujui au hukufundishwa sheria ndiyo maana ukavunja sheria hizo.

SAWA, TRA wanao wajibu wa kuwapa taarifa wateja wao kuhusu mambo wanayoyasimamia; lakini kutofanya hivyo kamwe hakuwezi kuwa ndiyo iwe sababu ya wahalifu kujitetea uhalifu wao.
 
Bila shaka wewe ni mwajiriwa wa serikali, kodi yako si sawa na wafanya biashara ndio maana unaona ni sahihi

Ingekuwa kodi ni hiyo tu 18% sawa ila imagine ulipe hiyo 18% bado ya leseni ulipe, jiji, bado ya mapato kubwa mhalisia bro
 
Usiwe na haraka sana ya kujitangazia ufalme.

Kuna sheria. Yeyote anayevunja sheria ni mharifu.

Huwezi kudai kwamba hujui au hukufundishwa sheria ndiyo maana ukavunja sheria hizo.

SAWA..., TRA wanao wajibu wa kuwapa taarifa wateja wao kuhusu mambo wanayoyasimamia; lakini kutofanya hivyo kamwe hakuwezi kuwa ndiyo iwe sababu ya wahalifu kujitetea uhalifu wao.
Hizo ni sheria kandamizi ndo maana wanasema wamechoka na inatosha. Msiwalazimishe kufungua maduka.
Afterall hata wakikusanya zinaenda kuliwa tuu.
 
Mkuu wewe ndio haujielewi kwa kuwatetea TRA, na kwamfano ulio utoa basi badala ya TRA kukamata mzigo wa mgeni walipaswa wamuwajibishe mfanya biashara kwa kutumia ushahidi wa mgeni.
Hata kwa mfano ulio utoa, bado TRA atakua ndie amewafukuza wafanya biashara wa nje, badala ya kuwaelimisha na kuwalinda.
Kumbuka mfanya biashara wa Kariakoo sio jukumu lake kumuelimisha mgeni, bali ni wajibu wa TRA na serikali kumuelimisha mgeni/mteja ili kumlinda.
Umeandika utumbo wa kuku Bora ungekaa kimya tu
 
Hizo ni sheria kandamizi ndo maana wanasema wamechoka na inatosha. Msiwalazimishe kufungua maduka.
Afterall hata wakikusanya zinaenda kuliwa tuu.
Hilo ni jambo tofauti na linalojadiliwa hapa.

Kama ni sheria kandamizi, shughulika na hilo zibadilishwe.

Si jukumu la TRA au Waziri kuzibadili hizo sheria moja kwa moja. Kuna taratibu zinazojulikana katika kufanya kazi hiyo.
 
Kuksta mzizi wa fitina ,serikali ingechukua sample ya hao wafanyabiashara wanao sema wamekadiriwa kodi kubwa na commission an independent reputable audit firm eg PWC/KPMG/E&Y/Delloite kupitia hizo disputed assessment na baada ya hapo kuchukua hatua stahiki.
 
Kikokotoo cha kodi ni kibovu mno wakuu, tusidanganyane kodi za nchi hii + tozo lukuki hazilipiki.... TRA na wenyewe wanakadria kwa kukomoa ili uwape rushwa. Eeh bhana eeh juzi nikaenda pale TRA Kimara kusajili kibiashara changu kimoja, nikadanganya mtaji wangu 300000 na faida kwa siku nikaweka kama 5000 hivi, frem nikasema 50000 kwa mwezi. Jamaa amekokotoa mahesabu ananiambia milion 1.5 kodi, alooooh jamaa nikamweleza mbona hii miyeyusho, jamaa akaniuliza mimejipangaje, daah ikabidi nimtoe 70000 jamaa akafanya manyanga, kodi akaweka 250000.

Yani hapo ukimzingua kumpa rushwa anakuwekea makadrio si ya nchi hii, na mwaka kesho ita_double, imagine hapo nimedanganya ningesema ukweli hapo si ni hatari.

Ukiagiza gari Japan, ikifika bandarini wakati mwingine kuitoa inakugharimu tozo kuzidi gharama ya kununua na kusafrisha, hiyo ni kuua uchumi, watendaji wenyewe wanajichotea hela na kuiacha nchi inajifia, chawa kazi yao ni kuimba na kusifu tu.

Ukiwa mfanya biashara kwenye hii nchi ni full stress.
 
Back
Top Bottom