Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Nani kateua mhuni kampeni za CCM?
Na Anthony Mayunga
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba ametetea chama chake, kwamba hakihusiki na tukio la kufukuzwa kwa waandishi wa habari, wiki tatu zilizopita mjini Bukoba.
Alisema, CCM ni chama makini, hakiwezi kufukuza waandiushi wa habari.
Makamba alikuwa akijibu tuhuma kwamba chama chake kilishiriki katika kufukuza waandishi wawili wa habari wa magazeti ya Mwananchi na The Citizen.
Katika kutetea chama chake, Makamba alisema, Ili uamuzi wa chama chake uwe wa chama, ni lazima ufikiwe na Kamati Kuu (CC), Halamashauri KUU ya Taifa (CCM-NEC), au aufanye katibu mkuu. Vikao hivi havikufanyika kokote na mimi katibu mkuu sijaagiza mtu awafukuze waandishi.
Aliongeza, Fuatilia vizuri habari yako, ni lazima utagundua kuwa yupo mhuni amekosana nao akawafukuza.
Makamba hataki kumtaja huyo anayemwita mhuni ambaye ameongozana na mgombea wa chama cgake. Wala hataki kujadili hatua ambazo chama makini kitamchukulia mhuni anayetajwa kufukuza waandishi wa habari.
Aidha, Makamba hataki kueleza ulimwengu, kwa nini chama chake kimeteua mhuni na kumwingiza katika msafara wa mgombea urais.
Hataki kujadili kwa nini yeye na chama chake wameshindwa kumwondoa mhuni huyo. Hataki kueleza kwa nini chama kinachoelekea Ikulu kimebeba wahuni.
Ni kwa sababu, alichokisema Makamba sicho anachokiamini. Makamba anajua kuwa uhuni si sifa nzuri. Anayeitwa mhuni hafai kukaa na watu makini; hawezi kuruhusiwa kufanya kazi zao wala hawezi kuwasemea.
Kama afisa wa habari wa mgombea wa urais ni mhuni, habari zinazotoka zitawezaje kuaminika? Je, nani anaweza kuziamini? Kwa vigezo vipi?
Ni muhimu hili likafahamika. Kama mhuni yupo katika msafara wa mgombea urais, tena ambaye yuko madarakani, wahuni wengine wangapi wamejazana Ikulu? Akibahatika kushinda uchaguzi, atauynda serikali gani na iliyolenga kundi gani?
Je, mgombea ambaye amekusanya wahuni katika timu yake ya kampeni, atawezaje kuaminisha wananchi, kwamba serikali atakayounda haitajaa wahuni?
Kauli ya Makamba ni tata kwa ujumla wake na ina tafsiri nyingi kwa watu; maana haiwezewkani chama makini kinachoongoza serikali kuchukuwa mhuni na kumlipa fedha ili kuratibu waandishi wa habari.
Mtu aliyemtaja Makamba kwamba ni mhuni bado anaendelea na kazi yake. Anaendelea kufukuza waandishi. Amekabidhiwa fuko la fedha ambazo zimechangwa na wanachama.
Bila shaka Makamba anajua maana ya mhuni; ni kapera, mseja, mpora wake za watu, asiye na makzi maalum, mwizi, kibaka, mvunjaji wa sheria, mnyanganyi, mchopozi na ambaye anaishi kihuni.
Kutokana na hali hiyo, Makamba anataka kuwaambia wanachama wake, kwamba amekosa watu makini wa kufanya kazi ya kuratibu vyombo vya habari. Ndiyo sababu amelazimika kuchukua mhuni kufanya kazi hiyo.
Vinginevyo, Makamba anataka kutuambia kuwa CCM yote imejaa manyani wanaoweza kuruka pamoja .
Chanzo: Mwanahalisi, toleo la sasa.