William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Mkuu swali kwamba ana watoto wangapi na umri wake una relevance gani kwa kazi yake ya Unaibu Waziri? La maana hapa la kufahamu ni elimu yake. Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge mheshimiwa huyu ni Mwanasheria, ni Wakili wa Mahakama Kuu, na kabla ya uteuzi wake alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.
Ukiachilia mbali michango yake mingi Bungeni inayohusu utetezi wa haki na maslahi ya wafanyakazi (malipo ya pensheni ya wafanyakazi wa Tazara, waalimu waliosimamishwa Chuo cha Ustawi wa Jamii, wafanyakazi wazalendo wa migodini wanaolipwa kipato tofauti na wageni kule Barick) mheshimiwa huyu aliongoza debate ya maoni ya wadau kuhusu muswada wa sheria ya Katiba kule Dodoma....pale ndipo alipo display skills za hali ya juu,kwa ku accomodate mawazo ya pande zote pasipo ushabiki.
Mpaka anateuliwa nafasi ya naibu Waziri wa Katiba na Sheria, alikuwa ni Katibu Mkuu wa Tanzania Women Parliamentarian Group (TWPG) inayojumuisha wabunge wanawake kutoka vyama vyote, pia alikuwa Mmoja wa wawakilishi wa Bunge la Tanzania katika Interparliamentarian Union (IPU) ambapo alichaguliwa na taasisi hiyo kuwa Mjumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu.
- CV nzito nilidhani ni ya Rais mpya wa Ufaransa maana zinafanana fanana eti, saafi sana Waziri anakuwa kwenye kiwango cha elimu yake, sasa muacheni dada yetu afanye kazi ya taifa.
William.