Ni vyema tukakumbuka kuwa Angela Kairuki hii si mara ya kwanza kugombea ubunge. Aligombea 2005 na wakati huo wala hakuwa Vodacom. Sasa mbona kipindi kile hamkuona uhusiano wa Angela na mafisadi akina Rostam..? Hii ni maraya pili amejaribu na amekubalika kachagulika tena kwa kura nyingi sana. Napenda mfahamu taarifa hizi badala ya kumhusisha dada wa Watu na mafisadi. Wagombea waliofadhiliwa na mafisadi kwanza wengi walianguka vibaya sana. Wapo ambao walipewa fedha waende kwenye majimbo kama ya Mzee wetu Mpendwa Samuel Sitta lakini wameanguka ile mbaya.