Nani anayeizima taa ya Jerry Muro mwandishi mahiri wa habari

Hili swala la huyu jamaa nimekuwa kila mara natafakari sipati majibu..
Mpaka sasa sijaamini na sitaamini kama aliomba Rushwa.
Kijana aliyekuwa anaipinga Rushwa na akijua kabisa kuna watu wanamchukia bado akaombe rushwa
La La Tz bwana ni zaidi ya vile tuijuavyo
 
Kuna kauli yake alikuwa anasema "Ikiwaka mulika na ikizima papasa"..huenda kwa sasa bado anapapasa pakuiwashia taa yake iliyopoteza nuru kwenye jamii ya waTz.
 
Hili swala la huyu jamaa nimekuwa kila mara natafakari sipati majibu..
Mpaka sasa sijaamini na sitaamini kama aliomba Rushwa.
Kijana aliyekuwa anaipinga Rushwa na akijua kabisa kuna watu wanamchukia bado akaombe rushwa
La La Tz bwana ni zaidi ya vile tuijuavyo

viongozi wa dini wanapinga machafu na bado baadhi yao kila kukicha wanapata skendo chafu za masuala wanayoyapinga!iinashindikana vipi kwake kufanya analolipinga?.......suala la jerry ni zaidi tulijuavyo ila kiufupi dogo alijiingiza katika upigaji makorongwee na watu wa duniani ndo ilikuwa kampani yake!
 
Of all things Jerry Muro ntamkumbuka kwa kazi kubwa aliyoifanya kuanika uozo, ufisadi, unyang'au waliokuwa wanaufanya askari polisi check point ya Igumbiro- iringa pale. wale watu walikuwa ni kama Miungu watu, manyanyaso, udhalilishaji tuliokuwa tunafanyiwa madereva chek point ile hauelezeki. Mara baada ya tukio lile kuanikwa na Jerry kupitia kipindi cha usiku wa habari TBC1, RPC Mangala alilishughulikia kwa kuwafukuza kazi baadhi ya askari walioonekana "live" wakichukua mlungula (dokezo sabili) hali c mbaya sana hadi leo. Ni mfupa ambao kamanda Advocate Nyombi ulimshinda hadi anaondoka. Big up JERRY!!!!!!!
 
Natamani shauri hili la Jerry limalizike mapema ili arejee kwenye uringo wa habari aendeleze kufichua maovu yatendwayo na watu waliopewa dhamana ya kutumikia wananchi lakini wanafanya ndivyo sivyo! Nadhani ataifahamisha jamii yote yaliyomsibu na kupelekea kuingia matatani dhidi ya vyombo vya dola.
 
JF, tangu jana nimeanza kutafakari upya juu ya report za Jerry Muro na kukumbuka umahiri wake katika kutoa habari bila woga, huyu jamaa ni shujaa kama kina Ndimara Tigambwage and Said Kubenea na wengine wachache. Kuna haja ya JF tena kujadili juu ya nani anataka kuizima taa hii na kwa nini? Afunguliwe Mandela....afunguliwe Jerry Moro![/QUOTE

Mimi nilipofatilia habari ya kesi ya huyu jamaa,kwa kufatilia ushahidi wa wale mashahidi nahisi kuna sehemu alijichanganya akajaribu kuchukua rushwa...maelezo ya mashahidi yapo straight forward...........
 
Alijisahau akadhani yeye ndio yeye. Mpaka ufikia hapo nadhani kuna wengi aliwaliza.
 
subiri kesi iishe ndo ujudge

Ni kweli kaka USIHUKUMU kabla case haijaisha. Tuache Mahakama ifanye kazi yake ila kama kuna ukweli fulani basi amwombe Mungu amsamehe kabla case haijaisha. LAKINI KAMA NI FITINA NA CHUKI BINAFSI HATA KUFIKIA KUMSUMBUA KIASI HICHO, BASI MUNGU ATAMLIPA. Amina
 
Lakini mnafahamu vizuri kosa au kesi yake? Tutafakari vizuri. Huyu kijana nilikuwa namuona tangu awali kuwa ana matatizo makubwa. Hata haya yaliyomkuta. Tafakari.
 
.......Baja,

..............if you come to equity come with clean hands.................asa,mwandishi na pingu wapi na wapi???

taa ameizima mwenyewe,hana wa kumlaumu............

Nadhan taa yake imepunguzwa mwanga......si kuwa imezimwa,mgao ukiisha(kesi yake) atashyn
 
Back
Top Bottom