Nani anaiua CUF je ni CCM, viongozi wenyewe wa CUF au wananchi au muda wake umefika?

Nani aiue CUF wakati ilikufa zamani? Kwani hamkujua kuwa CUF ni Seif na Seif ni CUF? Wanangu, tangu alipogeuzwa nyumba ndogo jeneza lake kisiasa lilishushwa kaburini (ofisi ya makamu wa rais wa Zanzibar).
 
Wenzenu tunaojua siasa tuling'amua zamaaani kuwa CUF imefika ukomo. Wanasiasa huwa wanapenda madaraka si wananchi ambao huwa nyuma yao na wengine kufa kwa ajili yao. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Komandoo alimnyang'anya Maalim Seff haki zake za Waziri Kiongozi mstaafu kisha ukaja muafaka Maalim akarudishiwa haki zake; akapoa. Umekuja huu muafaka na Maalim amepata Umakamo wa Rais; Mungu ampe nini wakati huu ambao ni jioni kwake na bila shaka akitoka hapo atarudi Pemba kupumzika na kula kwa raha hadi siku ambayo Mungu wake atamvuna.Mission accomplished hata CUF ikifa wacha ife malengo ya mwenye Chama yametimizwa. Ninyi wafuasi shauri yenu mtajiju. Madaraka jamani matamu nyie acheni tu.

Nini maana ya chama kufa? fafanua

Mgogoro katika chama ndio kifo?

Mgogoro huu umeandaliwa na kusukwa na wafuatao: CCM, CDM na Maaskofu..

Wote hao wanaogopa CUF jinsi inavyohamasisha wa zanzibar kuwa wamoja..na maslahi yao yanaondoka kila siku

(hizo ni habari za ndani)..nilishasema zamani system haitishwi na cdm bali CUF..
 
UNAPOSEMA KIJUSSA AMEIUA CUF UNAMUONEA, UPUUZI WA KIJUSA NI WA JUZI JUZI TUU WAKATI CUF ISHAANZA KUPOTEZA MVUTO TARATIBU MUDA SANA........

MAALIMU; NAWEZA KUAMINI KWA SABABU
KAMA KIONGOZI MKUBWA ANAYEJALI MASLAHI YA CHAMA ANGEFANYA JITIHADA ZA MAKUSUDI KUNUSURU, HIVYO BASI KUKAA KWAKE KIMYA KWA KUDHANI KUWA LENGO LAKE LA IKURU NDOGO LIMETIMIA LINAZIDI KUPOTEZA CHAMA LAKINI SI CHAMA TU HATA YEYE NAFASI YAKE ITAKUWA FINYU KURUDI HAPO ALIPO LABDA AFANYE SHIBUDA-LISM

MIPANGO THABITI NA HARAKATI ZA CCM KUIINGIZA KATIKA MSETO CUF HUKU WAKIMWELEWA VIZURI NIA YA MAALIMU , NAO HAWAKUHAJIZIKA NI KUMPATIA SUMU INAYOWAUA KUFANIKISHA LENGO.

KUKOSA VIONGOZI HODARI : CUF HAINA KIONGOZI ANAYEWEZA KUFIKIRI AKAFIKIRI KISHA AKASEMA NAWE UKAKUBALI NA KUSEMA KUWA KIONGOZI AMESEMA. UKIMTOA PROFESA WENGI WALIOBAKI NI AKINA KIJUSSA, PROFESSA PEKEE HAWEZI KUONGOZA AKIWA PEKEE ( TEAM WORK INAHITAJIKA)

DHANA YA UDINI : DHAMBI MBAYA ITATAFUNA YEYOTE NA CHOCHOTE AKIBAINIKA. IMEBAINIKA ACHA IWATAFUNEEEE

:lol:WE NI KUNI YA AKIBA, USIICHEKE KUNI YA JIKONI:A S 465:
 
Maalim alikuwa na ajenda yake ya siri siku zote, maslahi ya uzeeni ndiyo ilikiwa vita yake kubwa. Kwa cheo cha uwaziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar alichokuwa nacho kabla, kilimhakikishia maisha ya raha uzeeni kutokana na masurufu yake.
Sasa ilipotokea kupigwa kalamu ndipo akaingia kwenye harakati mpya za kusaka ukubwa kwa njia ya upinzani. Kwa kuwa sasa kafanikiwa kupata alikuwa analipigania binafsi yake ni nini tena kinachomfanya asumbuke zaidi? Pole ni kwa wale wanasiasa makini ambao nia yao ya kuwrpo CUF ilikuwa thabiti na sahihi kama vile bwana Julius Mtatiro aaa siku hizi nasikia wanamwiita Ustaadhi Juma4 Mtatiro.
 
Wenzenu tunaojua siasa tuling'amua zamaaani kuwa CUF imefika ukomo. Wanasiasa huwa wanapenda madaraka si wananchi ambao huwa nyuma yao na wengine kufa kwa ajili yao. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Komandoo alimnyang'anya Maalim Seff haki zake za Waziri Kiongozi mstaafu kisha ukaja muafaka Maalim akarudishiwa haki zake; akapoa. Umekuja huu muafaka na Maalim amepata Umakamo wa Rais; Mungu ampe nini wakati huu ambao ni jioni kwake na bila shaka akitoka hapo atarudi Pemba kupumzika na kula kwa raha hadi siku ambayo Mungu wake atamvuna.Mission accomplished hata CUF ikifa wacha ife malengo ya mwenye Chama yametimizwa. Ninyi wafuasi shauri yenu mtajiju. Madaraka jamani matamu nyie acheni tu.

Big up Mkuu Kimbunga.Great analysis
 
Nini maana ya chama kufa? fafanua

Mgogoro katika chama ndio kifo?

Mgogoro huu umeandaliwa na kusukwa na wafuatao: CCM, CDM na Maaskofu..

Wote hao wanaogopa CUF jinsi inavyohamasisha wa zanzibar kuwa wamoja..na maslahi yao yanaondoka kila siku

(hizo ni habari za ndani)..nilishasema zamani system haitishwi na cdm bali CUF..

Mkuu jiondoe hilo shuka usoni.Ina maana maaskofu ndio walimtuma Ismail Jussa aropoke CUF walishindwa Uzini kwa sababu ya Ukristo na Ubara? Huyu ndio mchawi namba moja wa CUF
 
Mkuu huhitaji miwani ya lens kujua kwamba CUF iko ICU. Kwa maana yako CCM ni Maali Seff, CDM ni Hamad Rashid na Maaskofu ni Mtatiro na Jussa? Au sijakuelewa mkuu?
 
Maalim alikuwa na ajenda yake ya siri siku zote, maslahi ya uzeeni ndiyo ilikiwa vita yake kubwa. Kwa cheo cha uwaziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar alichokuwa nacho kabla, kilimhakikishia maisha ya raha uzeeni kutokana na masurufu yake.
Sasa ilipotokea kupigwa kalamu ndipo akaingia kwenye harakati mpya za kusaka ukubwa kwa njia ya upinzani. Kwa kuwa sasa kafanikiwa kupata alikuwa analipigania binafsi yake ni nini tena kinachomfanya asumbuke zaidi? Pole ni kwa wale wanasiasa makini ambao nia yao ya kuwrpo CUF ilikuwa thabiti na sahihi kama vile bwana Julius Mtatiro aaa siku hizi nasikia wanamwiita Ustaadhi Juma4 Mtatiro.
Haswaaaaaa MKuu! Leo mtu anatembea na eskoti, anavalishwa na SMZ na bila shaka ana uhakika wa 80% ya incumbent VP unataka apiganie CUF ili iweje? Nyinyi hamumtakii mema Maalim mnataka amalize uzee wake kwa shida ati kisa CUF iwe imara ilhali yeye ni dhooflihal?
 
Maalim Seif kwa tamaa ya madaraka na ndio maana akakubali haraka haraka matoke ya uchaguzi uliopita ili tu apate umakam wa rais feki, sasa ndio wanavuna walichopanda.
Hivi wale waliokufa january 27 kwa kumpigania Maalim wakifufuka leo hii itakuwaje? Siasa bwana ni kamchezo kazuri hasa ukiwa hufungwi na kachama kokote ama mtu. Siku huyo mtu atakapogeuka baada ya kutimiza matakwa yake unaweza kujinyonga.
 
Mkuu jiondoe hilo shuka usoni.Ina maana maaskofu ndio walimtuma Ismail Jussa aropoke CUF walishindwa Uzini kwa sababu ya Ukristo na Ubara? Huyu ndio mchawi namba moja wa CUF
mkuu huyo topical achana naye...ni moja kati ya watu ambao chuki yao dhidi ya ukristo sanasana ukatoliki haielezeki kwa maneno...bila kuingiza issue za maaskofu na mou maruhani yake hayawezi kutulia...!
 
Mkuu huhitaji miwani ya lens kujua kwamba CUF iko ICU. Kwa maana yako CCM ni Maali Seff, CDM ni Hamad Rashid na Maaskofu ni Mtatiro na Jussa? Au sijakuelewa mkuu?

Haya mambo si rahisi hivyo..

Hamad Rashid amehongwa na CCM na Agent wa maaskofu (Pinda) kuivuruga CUF ili umoja wa wazanzibar upungue maana kadri siku zinavyokwenda CUF wanazidi kuwaunganisha wazanzibar kitu ambacho ni hasara kwa ccm...na interest za church..

Chadema wametumika kuwarubuni wafuasi wa chini kuasi CUF, na hiyo inafanyika through watu maalum kuna mkono mrefu, kubwa zaidi chadema wanashirikiana na CCM kuimaliza CUF, as ata stake chadema na CCM wana ajenda moja kuhusu zanziba -kupunguza nguvu za wazenj

Ni swala la wazanzibar kuwa makini na huu mchezo unaoendelea..wakiteleza ndio hivyo tena zanzibar inarudi kwenye migogoro CCM na CDM wakifurahi kwani malengo yao na wakubwa zao.(???) yametimia..

ni swala la kusubiri nakuona kama watafanikiwa..
 
mkuu huyo topical achana naye...ni moja kati ya watu ambao chuki yao dhidi ya ukristo sanasana ukatoliki haielezeki kwa maneno...bila kuingiza issue za maaskofu na mou maruhani yake hayawezi kutulia...!

Hivi ukweli ni chuki mkuu?

MoU ni uwizi ni uwongo? najua wewe udini unakusumbua hutaki kusikia mabaya ya kanisa lako
 
Hahhaha, DUA YA KUKU HAIMPATI MWEWE. Hivo munafikiri CUF inakufa?. Hiyo ni ndoto. CUF iko imara kabisa hawa wanaotoka CUF ni makada wa CCM ndani ya CUF. Inabidi wajitoe maana wameshtukiwa hawana mpango. CCM walijaribu sana kukiharibu chama hata Mh. Kikwete akathubutu kutamka hadharani kuwa watakiuwa chama kwa bahati tukaingia kwenyez serikali ya umoja wa kitaifa ambao wapinzani wakubwa ndani ya CUF walikuwa ni hao hao waliojitoa. Na hata CCM wenyewe hawakuamini kama CUF watakubaliana baina ya Amani Karume na Maalim Seif kukaa chini kwa manufaa ya taifa lao. Sasa inabidi hao waliopinga, wajiuzulu maana "mission impossible"..
Sasa tutaona viongozi wapya wadogo wanajitokeza kusimami chama chao. Wananchi wengi hawafahamu kama hata hawa chipukizi wana haki ya kuwa viongozi. Tuna mikakati ya kuwawezesha vijana kushika hatamu za uongozi wa juu katika chama. HAKI SAWA KWA WOTE.
 
Mkuu Maalim Seff alikuwa na bifu na Komandoo, alipokuja binamu yake
akamrejeshea marupurupu ya uwazir kiongozi mstaafu na JK akaja akasema
aingizwe kwenye SUK basi jamaa akanyamaa. Huku akijua kwamba hawezi ten kuukwaa Urais wa Zenj akaamua yaishe. Nadhani ulimsikia akisema mwenyewe siku ile matokeo yanatangazwa. Mkuu hutaki kuamini kwamba CUF ilizaliwa na sasa inakufa? Hebu naomba uniambie Maalim alipoitwa na Mwalimu pale Butiama waliongea nini? Ukiniambia hilo basi nitaamini kuwa Maalim si CCM.
 
Back
Top Bottom