Nani anafaa kuwa rais wa Tanzania 2015?

SLAA, please tusilinganishe mamba na mjusi. Mamba tani 1.5 uzito mjusi hata robo kilo hafiki jamani.
 
Kwa kuona kichwa cha habari hapo juu mawazo ya wengi huenda yaka kimbilia katika mchakato wa uchaguzi mkuu ujao.
Nimetafakari juu ya matukio mawili niliyo pata kuyafahamu ;
(1) Rais Kenyatta kulipua meli iliyo kamatwa na shehena ya madawa ya kulevya
(2)Rais Kenyatta kuteketeza kwa moto shehena kubwa iliyo kamatwa ya pembe haramu za ndovu

Kiukweli ninadra sana barabarani Africa kushudia uthubutu huu, hii ni kwa vile tu viongozi wengi wa nchi, huwa na maslahi ya moja kwa moja na biashara hizo.

Lakini kama watatokea viongozi wengi zaidi wasio na tamaa (walio rizika) wenye utayari wakulinda maslahi ya wananchi wao, nasema Africa itakua namba moja duniani kwa mafanikio.

Tuweni makini sana jamani katika kuchagua viongozi makini, tuangalieni mbali nasio mbele.

Ahsanteni kwa kuusoma na kuuelewa uzi huu
 
Leo nipo safarini nasafiri kwa usafiri wa bus , nategemea kusafiri umbali wa zaidi ya km . 900 , mpaka saa hizi tumesha maliza km.600.

Ndani ya bus tulilopanda mjadala uliopo ni wa uraisi , nani anafaa kuiongoza tanzania ya leo . Sijawa mchangiaji lakini mawazo ya wengi humu yanasema raisi akiwa lowasa au dr. Slaa si mbaya wanadai kwa sababu wote ni watu wa kuchukua maamuzi magumu. Naona wengi wanaponda Pinda kwamba hafai kuwa raisi kama tatizo la albino tu ameshindwa ataweza uraisi. Membe na wengine hawazungumziwi kabisa sijui kwa nini wadau .

Watu humu wanasema Lowasa si mwizi wa Richmond na yeye kasema ikifika muda atasema ukweli juu ya richmond na kumbainisha nani mwizi. Watu wanajua mambo humu ndani ya bus utadhani walikuwepo.
 
Leo nipo safarini nasafiri kwa usafiri wa bus , nategemea kusafiri umbali wa zaidi ya km . 900 , mpaka saa hizi tumesha maliza km.600.

Ndani ya bus tulilopanda mjadala uliopo ni wa uraisi , nani anafaa kuiongoza tanzania ya leo . Sijawa mchangiaji lakini mawazo ya wengi humu yanasema raisi akiwa lowasa au dr. Slaa si mbaya wanadai kwa sababu wote ni watu wa kuchukua maamuzi magumu. Naona wengi wanaponda Pinda kwamba hafai kuwa raisi kama tatizo la albino tu ameshindwa ataweza uraisi. Membe na wengine hawazungumziwi kabisa sijui kwa nini wadau .

Watu humu wanasema Lowasa si mwizi wa Richmond na yeye kasema ikifika muda atasema ukweli juu ya richmond na kumbainisha nani mwizi. Watu wanajua mambo humu ndani ya bus utadhani walikuwepo.

Lowassa anatutosha sana kiukweli..
 
nimekuwa navutiwa sana aina ya uwajibikaji binafsi wa Kinana, amekuwa na mtu asiyependa kujikweza katika kutimiza majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kushiriki shughuli za wananchi moja kwa moja, kama mnavyojua kuna viongozi ambao huwa wanaigiza kuonekana ni watendaji ilhali hawawezi, pia viongozi wengine wameonekana kuchemka kwa staili yake ya ufanyaji kazi za wananchi, kutokana na kulemewa na vitambi na wengine kujifanya watanashati. kwa staili yake hii ya utendaji inanishawishi kumuona anafaa kuwa raisi ajaye, ingawa simfahumu vizuri katika mambo mengine yanayosumbua nchi yetu, ikiwemo maadili, umri wake nk.
Z
 
ndugu zangu watanzania rais atayetufaa ni mtu aliyebobea kwenye uchumi tatizo ni kuwa hakuna rais duniani ambaye ataingia madarakani zama hizi akawa muadilifu kutoka vyama vyote.kwa nini?kila mmoja atataka kwanza kujitajirisha yeye ,mkewe na familia yake.pili kuwaridhisha marafiki zake ama kwa vyeo au mambo mengine.lakini la msingi apatikane mchumi ambaye angalau ataweza kuboresha pesa yetu,miundo mbinu nk ingawa naye atakuwa mwizi.mchumi atazingatia fani yake ambayo pamoja na wizi wake atasaidia kukuza uchumi na kuuboresha hivyo angalau mwananchi ataweza kuboresha maisha yake.
 
Kuna kila dalili kuwa Katibu mkuu wa CCM Abrahaman Kinana huenda akawa miongoni mwa wanaCCM watakaochukua form za kutaka kugombea urais kupitia CCM mwaka huu 2015.
Mpaka sasa Kinana hajatangaza kutaka kugombea au kutogombea urais.

Habari hizi zinakuja wakati tayari Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara Mwigulu Nchemba amekwisha tangaza kutaka kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka huu na yupo kwenye kampeni kubwa kufanikisha hilo na tayari (Kinana amempiga marufuku kufanya ziara zozote za kichama toka aanze harakati hizo)

Inasemekana Kinana huenda ameficha kuonesha nia yake ya kutaka kugombea urais mapema ili apate mwanya mzuri wa kujijenga miongoni mwa wanaCCM akitumia kofia ya ukatibu mkuu bila vipingamizi na pia kuepusha kuadhibiwa na Chama kwa kuvunja kanuni za CCM.
Mbinu kama hii aliitumia vizuri sana John Malecella wakati anataka kugombea urais kupitia CCM 2005 wakati huo akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara.

Sababu kuu zinazoweza kupelekea Kinana kushawishika kutaka kugombea urais ni:
1/Nafasi ya juu ya Kiuongozi na kiuendaji ndani ya CCM inayompa kuaminiwa na wanaCCM wengi.(Kumbuka rais mwanaCCM pia anapata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa CCM).

2/Vita kubwa ya Makundi hasimu ya Urais ndani ya CCM inayohatarisha uhai wa CCM kwa sasa, hivyo inampa Mwanya Kinana kuweza kuteuliwa ili kulinda uhai wa chama kwa kuwa hana kundi na amekuwa akipambana kulinda uhai wa ndani ya CCM.

3/Ziara nyingi na ndefu za CCM anazozifanya sasa zimekuwa zikimjenga zaidi Kinana binafsi kuliko wagombea wengine wa urais ndani ya CCM. Amekuwa akikosoa utendaji mbovu wa serikali na watendaji wa CCM kana kwamba yeye sio Miongoni mwao. (Awali watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri waliwahi kulalamika kitendo cha Kinana na msafara wake kuwaweka majukwaani na kuwadhalilisha mbele ya wananchi kwa utendaji mbovu)

4/Uzoefu wa kampeni za urais za wagombea wa CCM dhidi ya Upinzani(Kinana alikuwa meneja wa Kampeni za Urais za CCM mwaka 1995, 2000, 2005, 2010. Yaani wakati wa Mkapa na Kikwete) na CCM ikaibuka kidedea. Hivyo kupambana na UKAWA ingehitaji mtu kama yeye.

5/Kitendawili kigumu ilichonacho CCM kwa sasa kuhusu nani wakugombea urais na wakati huo huo Rais Kikwete alishawaambia wanaCCM kuwa wote waliojitokeza kutaka kugombea wote hawafai, hivyo waibuliwe wengine ambao CCM inaweza akawaamini. Kinana hajawahi kutangaza kugombea urais lakini ni MwanaCCM halisi, mzoefu na Kiongozi wa juu sana wa CCM kwa sasa.
 
Back
Top Bottom