Nani anaenyoa watu usiku jamani??

kabla ya kulala soma PSALM 91 kwenye bible. tatizo mnalala bila kusali ndo mana wanga wanawachezea!
 
Mimi huwa siamini mambo haya kabisa ila sasa ni miezi sita walininyoa chini ya kidevu na nywele hazijaota mpaka leo!
 
yapo hayo mambo mie walininyoa ma.... Looo watu wabaya hawa, kuna dada mmoja anakatwaga makucha
 
Hizi story mi huwa nazisikia tu. Na huyo anaewanyoa wenzie sijui na ye yupo anasoma huu uzi!! Mwee!
 
Mara nyingi huwa ni panya jike mwenye mimba hutafuta vitu laini laini kufanyia sehemu ya kuzalia wanawe, wala si kitu cha ajabu na wengi yamewakuta. Mwambie huyo jamaa achunguze atakuta kuna panya chumbani kwake na hizo nywele atakuta zimetengenezwa "kitundu" cha kuzalia. We are not the only intelligent creation.
 
BIBLIA TAKATIFU INASEMA NINI JUU YA UCHAWI?

Biblia inakubali uchawi upo, tusome katika bibilia tupate udhibitisho. “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israel”(Hesabu 23:23)
“basi Balaam alipoona ya kuwa wabariki Israel, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani. Balaam akainua macho yake akawaona Israel wamekaa kabila kabila, roho ya Mungu ikamjia.”(Hesabu 24:1,2)

Kuasi ni kama dhambi ya uchawi. “kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na unyago; kwa kuwa umelikataa neon la BWANA, yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”. (1 samweli 15:23)

“Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu mimi ndimi BWANA.”
(Lawi 19:28),

“msiwaendee wenye pepo wala wachawi; msiwafuate; ili kutiwa unajisi na wao; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu”(Lawi 19:31

“akampitisha mwanawe motoni, akatama bao, akafanya uganga, akashusha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.” (2 wafalme 21:6)
 
Nadhani wanachukuwa sample za DNA ku-check watoto wenu mliowakataa na kuwatelekeza.

By the way kwanini mnasema ni wachawi/shetani na si Malaika mwema kutoka kwa Mola?
 
Aliogopa kuonyesha sehemu nyingine alizonyolewa ila huyu kinyozi aishie hukohuko mtaani kwenu asije akakosea akanifyeka my pencil yangu.
 
Back
Top Bottom