Nani anaelekeza madereva Mwendo Kasi kupakia abiria kupitia milango iliyoangalia barabarani (Kibaha to Kimara)? Hadi abiria wagongwe?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimeona jambo lisilo la kawaida katika eneo la Temboni, gari la mwendo Kasi linapakia abiria kupitia milango inayotazama katikati ya barabara. Kibaya Zaidi wakati wanapakia Kuna gari zinapita kwa Kasi huku abiria nao wakikimbia Kwa Kasi Jambo ambalo kiusalama siyo SAHIHI. Wakati haya yanafanyika askari usalama barabarani yupo anaangalia, najiuliza haya ni maelekezo ya nani? Hiki kitendo kingekuwa hakina baraka za menejimenti naamini trafic angemwajibisha dreva lakini ukiona dreva asemeshi yapo maelekezo.

Ila niombe tu Kwa usalama wa abiria huyu aliyetoa haya maelekezo anapaswa kujitafakari kama fedha inazidi thamani ya uhai wa binadamu. Lakini pia ajiulize Hii ndiyo mwendokasi tuliyoitangazia Dunia? Kwamba katika ulimwengu huu gari za serikali zinapakia abiria bila kuzingatia usalama? Kibaya Zaidi muundo wa gari unakinzana na hiki tunachofanya, abiria anayepandia Upande wa kulia analazimika kushikwa mkono na kuvutwa na abiria aliyepo ndani ya gari. Let assume anayemvuta amemwachia akaangukia kichwa au Kuna gari inapita ikamkanyaga? Tutakwenda mahakamani na trafic case kwa sababu serikali umeshindwa kujali usalama wa watu wake?

Kamanda wa usalama barabarani nikushauri ukague utendaji wa magari ya mwendokasi, chukua maoni ya abiria kuhusu matendo yasiyo ya kiusalama juu Yao, fanya analysis nenda Kwa huyo aliyelekeza abiria wapakiwe kupitia mlango wa kulia eneo la kibaha to Kimara mwambie anatishia usalama wa kazi Yako. Lakini pia wape Uhuru trafic kusimamia mabasi ya mwendokasi. Mwisho fanyia mabadiliko parking ya daladala na mabasi ya mwendokasi mbezi Luis kupunguza mrundikano wa abiria kituoni kwani yawezekana wanaolazimisha madreva kuvunja sheria ni abiria wakilazimisha kuwahi kazini Baada ya kukatiwa tiketi na magari yenyewe yakiwa hakuna.

Wito Kwa serikali; huu mradi wa mabasi ya mwendo Kasi umewashinda mliowapa dhamana, mabasi mabovu, hakuna usalama na yanapungua kila siku kwa kukosa matengenezo. Nadhani Hadi waziri mkuu akatembelee mabasi haya ndipo hatua zitachukuliwa ,vinginevyo mkuu wa mkoa na timu yake sidhani kama wanaelewa changamoto za mabasi haya na may be wamekatazwa hata kusimamia utendaji wake, lakini pia yawezekana hata polisi wamekatazwa kukagua usalama wa vyombo vya moto vya shirikia letu pendwa.......
 
Ule mlango ulivyo mrefu mtu anapandaje pale?
Kwanza huyo abiria katokea wapi hadi apandie upande wa Deree
 
Hukuweza kupata hata ka picha?, haya mambo yanahitaji kufanyiwa kazi turipoti sehemu husika.
 
Watu wa huko Dar Wana uwoga wa ajabu sana Sijui akili zinadumazwa na Nini: kama wao wanaweza kupanda mwendokasi Kwa mlango wa kulia wakivutwa mkono unadhani watu wa mikoani watafanyaje?

Wasomi wengi tumefauli history kwakujibu tulitokana na nyani na Sasa tupo kwenye practical exercise ya unyani


Mwendokasi shikilia hapohapo nyani waelewane
 
Back
Top Bottom