Nani alimuua Samora Machel?

SIMULIZI ZA MAPAMBANO NCHI MSUMBIJI DHIDI YA WARENO NA PIA WAPIGANAJI WA RENAMO NCHINI MOZAMBIQUE


View: https://m.youtube.com/watch?v=ElHJwY23hk8

Feliciano Juma Moses Mwadusa mzaliwa wa Tanga asimulia mikasa ya RENAMO alipokuwa akitumikia jeshi la serikali ya Frelimo ya Mozambique katika maeneo mbalimbali ya Msumbiji


Miaka ya mwanzo ya 1960 alitoroshwa na mama yake toka Tanga Tanzania hadi Msumbiji.

Huko ndipo baadaye akajiunga na movement ya Frelimo ilipokuwa inaendesha harakati za ukombozi kutoka kwa utawala mkongwe wa Wareno nchini Mozambique.

Kutokana na umri mdogo akapewa jukumu la kukusanya taarifa kiutambuzi za kijeshi na usalamla za maeneo mbalimbali kwa njia ya radio call zilizokuwa zunatumiwa ktk medani za mapambano ya kijeshi.

Katika harakati za jeshi la Msumbiji kurudisha usalama dhidi ya RENAMO ikiyokuwa ikiongozwa na Alfoso Dlakama alitumikia maeneo ya Sofala, Manica, Beira, Cabo Delgado.

Feliciano Juma Moses Mwadusa alipata kujeruhiwa na bomu na ilimchukua muda kuimarika baada ya kupitia mikono ya madaktari kadhaa hadi madaktari wataalamu toka Cuba kuweza kumtibia na kurudi kuweza kutembea kama kawaida.

Feliciano Juma Moses Mwadusa asisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria za kijeshi hata unapostaafu wakati akisimulia wakati wa mahojiano kijijini Tulieni Ngongo Lindi, Tanzania.
 
Maafisa wa usalama wa enzi ya ubaguzi wa rangi wa huko Africa Kusini ndiyo walifanya hayo mauaji mwaka 1986.

Marehemu alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi.

Bwana Machel aliyeuawa pamoja na abiria wengine 30.
Sahihi kabisa
 
Maveterani wa Ukombozi Mozambique wakielezea historia ya Samora Machel


View: https://m.youtube.com/watch?v=CRkgN45HVoM

Wazee hao Marcelino Dos Santos, Marina Pachinuapa, Armando Guebuza na Mariano Matsinhe wanasimulia toka Dar es Salaam walipokutana, kuishi na kuingia msituni pamoja na Samora Machel kutupa kumbukumbu kuhusu shujaa huyu kiongozi wa Mozambique
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom