Nani alimtangaza Majaliwa kuwa shujaa wa ajali ya ndege Bukoba?

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wadau wenye akili kubwa tulimjua shujaa wa ajali ya ndege iliyoua abiria 19 kuwa ni abiria aiitwaye Victor na mfanyakazi wa ndege walioshirikiana kuufungua mlango wa ndege kwa ndani na huyo Bw.Victor ndiye aliyesimama mlangoni kuwavusha abiria kuingia kwenye mtumbwi. Pia huyo huyo Bw. Victor ndiye aliyemtuma majaliwa kuangalia begi lake.

Je, ni nani aliyemtangaza kijana Majaliwa kuwa shujaa na kwa vigezo gani?
 
Wadau WENYE AKILI KUBWA tulimjua SHUJAA wa Ajali ya NDEGE iliyoua ABIRIA 19 kuwa ni ABIRIA aiitwaye VICTOR na Mfanyakazi wa Ndege Walioshirikiana Kuufungua Mlango wa Ndege kwa Ndani na huyo Bw.VICTOR ndiye aliyesimama Mlangoni kuwavusha Abiria kuingia kwenye Mtumbwi.Pia huyo huyo Be.VICTOR ndiye aliyemtuma Majaliwa kuangalia Begi lake .
Je ni nani ALIYEMTANGAZA Kijana MAJALIWA kuwa SHUJAA na kwa VIGEZO gani?
Ripoti ya Wataalamu Ina mapungufu;
1. Huyo Victor kama yeye na mhudumu ndiyo waliofungua mlango, ilikuwaje watu 19 washindwe kutoka hadi wafariki? Lazima wali struggle ndipo Majaliwa akasaidia kwa nje

2. Baada ya kufungua milango anasema watu wakapanda mtumbwi. Je huo mtumbwi ulikuwa hapo ukisubiri ndege ya Precision ianguke?

3. Ripoti hajawahoji manusura wengine wa ajali
 
Naye alikuwepo eneo la tukio mwanzoni kabisa kwahiyo kashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwaokea abiria
Haina haja ya kumsakama tatizo letu watz tunaumia kwanini awe Majaliwa... jambo dogo hili tunalikomalia wakati kuna mambo mengi tu yanayotusumbua sisi watz kwa ujumla
 
Mpaka sasa serikali ndio mshindi Majaliwa alitengenezwa akajadiliwa na report imemrudisha tena Majaliwa tutamjadili upya. Na issue ya msingi itapotezewa ambayo ni Uzembe wa Serikali.

Hii report walikosea sana kurejesha mjadala wa Majaliwa vitu vya msingi vitaacha jadiliwa tutamjadiili Majaliwa
 
Naye alikuwepo eneo la tukio mwanzoni kabisa kwahiyo kashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwaokea abiria
Haina haja ya kumsakama tatizo letu watz tunaumia kwanini awe Majaliwa... jambo dogo hili tunalikomalia wakati kuna mambo mengi tu yanayotusumbua sisi watz kwa ujumla
Hao walioandaa hii report wameichukulia hii issue personal.
 
Ripoti ya Wataalamu Ina mapungufu;
1. Huyo Victor kama yeye na mhudumu ndiyo waliofungua mlango, ilikuwaje watu 19 washindwe kutoka hadi wafariki? Lazima wali struggle ndipo Majaliwa akasaidia kwa nje

2. Baada ya kufungua milango anasema watu wakapanda mtumbwi. Je huo mtumbwi ulikuwa hapo ukiaubiri ndege ya Precision ianguke?

3. Ripoti hajawahoji manusura wengine wa ajali
Ushujaa wa Majaliwa haukuja kwasababu alipeleka mtumbwi, kama ingekuwa hivyo basi wavuvi wote pale walikuwa mashujaa.

Kinachoitwa ushujaa wa majaliwa kilikuja kutokana na madai ya huyo majaliwa kwamba aliufungua mlango wa ndege kwa kuupiga na kasia na mambo mengine mengi aliyoyaeleza kama kumpungia Rubani mkono wa kwaheri.

Victor anayedai kufungua mlango wa ndege kwa kusaidiana na mhudumu na kuendelee kuushikilia ili watu watoke alieleza wazi kabisa kwamba waliotoka kwenye ndege walipanda kwenye mabawa ya ndege mapaka mitumbwi ya wavuvi ilipokuja.[

Wadau wenye akili kubwa tulimjua shujaa wa ajali ya ndege iliyoua abiria 19 kuwa ni abiria aiitwaye Victor na mfanyakazi wa ndege walioshirikiana kuufungua mlango wa ndege kwa ndani na huyo Bw.Victor ndiye aliyesimama mlangoni kuwavusha abiria kuingia kwenye mtumbwi. Pia huyo huyo Bw. Victor ndiye aliyemtuma majaliwa kuangalia begi lake.

Je, ni nani aliyemtangaza kijana Majaliwa kuwa shujaa na kwa vigezo gani?
Majaliwa

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni hizo million 10 sijui 7 ndo zinawatoa watu roho hivi?

Em mwacheni kijana wa watu , Khaa Awe shujaa, asiwe shujaa haijalishi kama hajawaokoa ni bahati tu imemuangukia.

Hebu tuendelee na mishe zetu jamani.
aina ya watu mnaomkubali Majaliwa ndio ambao mnapendwa sana na wanasiasa,mnapendwa sana na manabii wa uongo na ni wafuasi wazuri wa chama tawala.Ni aina ya watu ambao ni rahisi sana kuwalaghai huwa hamjui kuhoji kwa kina.
 
Back
Top Bottom