Nane nane mwaka 2015: Matembezi ya hisani ya wana JF kuchangia wagonjwa Ocean Road

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398


Jamii-Media-798x350.jpg


Wakuu,

Kama mnakumbuka mwaka jana mwezi wa nane wana JF zaidi ya 20 tuliwakilisha wana JF wenye moyo waliochanga fedha na misaada mingine kwa ajili ya wagonjwa wa Kansa katika hospitali ya Ocean Road.


Usiku wa jana nilipitiwa na wazo la kuwashirikisha wana JF kwamba sikukuu ya nane nane ya mwaka huu 2015, tufanye matembezi ya hisani kwa ajili ya kuwachangia wenzetu waliolazwa pale Ocean Road.

Utaratibu wa kuchangia utakuwa ni kama ifuatavyo;

Nitauomba uongozi wa JF uchapiche fulana za kutosha ambapo kila fulana itauzwa si chini ya 30,000 kila moja na kama mtu ana uwezo anaweza kuchangia mahitaji ambayo nitayataja yenye thamani ya kiasi hicho cha 30,000 au atachangia zaidi kulingana na uwezo wake kifedha.

Fedha zitakazopatikana zitatumika kununulia mahitaji ya wagonjwa kamatulivyofanya mwaka jana, ila lilitolewa pendekezo siku ile tulipotoa misaada kwamba kila bahasha atakayopewa mgonjwa yenye mahitaji tuliyowanunulia iambatanishwe na kiasi cha shilingi 10,000, kwa ajili ya kuwasaidia kununua mahitaji mengine.

Wazo hilo lilikuwa ni zuri na ningependa mwaka huu tufanye hivyo.
Siku hiyo ya nane nane tukutane maeneo ya Sayansi Kijitonyama ndio tuanze matembezi ya kuelekea Ocean Road, ambapo tukifika tutawasilisha misaada yetu.

Naamini kwamba siyo wote watakaochangia watajitokeza siku hiyo katika kushiriki kwenye hafla hiyo, kwa sababu wengine wanaweza kuwa wametingwa na shughuli zao za kila sikuna bila kuwasahau wale ndugu zangu wa mikoani.

Nawaomba sana tena sana tushirikiane katika jambo hili maana kutoa ni moyo na si utajiri. Wenzetu wanahitaji misaada kutokana ha hali zao, na wote hapa hakuna anayejua kwamba kesho ataamka akiwa katika hali gani kwani mitindo ya maisha tunayoishi pamoja na vyakula tunavyokula vyote hivyo vinatuweka katika hatariya kupata ugonjwa huo wa kansa.

Ndugu zangu ambao tumekuwa tukishirikiana katika ile mikutaniko ya Get Together Party nawaombeni tuungane katika jambo hili. Najua kabisa hamtatuangusha kwani mara nyingi tumekuwa pamoja na hapa nitawataja wachache kwa msisitizo:

TAREHE: 11/06/2015

UPDATE.........

Wakuu,

Narejea bandiko langu kuhusu matembezi ya hisani ya kwenda Ocean Road siku ya sikukuu ya nane nane mwaka huu ili kutoa misaada.
Kuna maoni yalitolewa kuhusu kubadili muelekeo na kuelekeza misaada ya mwaka huu katika hospitali ya Muhimbili nazaidi ward ya watoto wanaoumwa kansa.

Bahati nzuri nilikutana na Mike Mushi hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu jambo hilo. Mike alinihakikishia kuhusu uongozi wa JF kushiriki katika kufanikisha zoezi hilo kama tulivyofanya mwaka jana.
Sasa basi katika maongezi yangu na Mike alinipa jukumu la kwenda Muhimbili kuonana na uongozi ili kupewa utaratibu wa namna ya kufikisha misaada hiyo na aina ya misaada inayokubalika.

Nilifika pale na kukutana na muwakilishi kitengo cha ustawi wa jamii ambacho ndicho kinachohusika na mambo ya social responsibility ambapo alinipa maelekezo kuhusuana ya misaada inayokubalika pale Muhimbili.


Tofauti na misaada tuliyopeleka Ocean Road, muhimbili hawapokei misaada ya aina ile,wao wanashauri kwamba ni vyema tukaangazia mahitaji ya dawa kuliko vitu vidogo vidogo ambavyo haviwapi wagonjwa nafuu.
Kwa kuwa nilisema kwamba lengo letu ni kuwatembelea watoto wenye matatizo ya kansa,lakini aliniambia kwamba wale watoto wanapata misaada mingi sana, hivyo akashauri tuangalie ward ya watoto wenye matatizo mbalimbali hususan wale wenye kesi za kuungua na moto ambao ni wengi sana na mahitaji yao ni mengi na na wamesahaulika kwa muda sasa.

Lilikuwani wazo zuri na walinipa mahitaji machache ambayo yanahitajika japo wakatimwingine yanabadilika badilika na wasingeweza kunipa orodha ndefu, lakini hatahivyo walishauri kwamba yapo mahitaji ya vipimo na dawa ambazo mara nyingi niza kununua moja kwa moja kwenye maduka na unaweza kukuta wazazi hawana uwezokifedha au wengine inaweza kutokea wamepewa ruhusa lakini wanakwama nauli.


Sasa walipendekeza kwamba pamoja na misaada ya dawa tutakazonunua, ni vyematukatenga kiasi cha fedha kikakabidhiwa kwenye kitengo cha ustawi wa jamii kwadharura za aina hiyo ambapo kama zikinunuliwa dawa au mahitaji mengine basirisiti itatumwa kwetu kwa uthibitisho na mwisho watatupa mchanganuo wa matumizi ili kujenga imani na sisi tuliotoa misaada.

Kama hilo litakuwa gumu kwa namna moja au nyingine, basi hilo fungu linawezalikakabidhiwa kwa uongozi wa JF na pale watakapokuwa na mahitaji ya kifedhawatawasiliana na uongozi na watatumiwa fedha wa tigo pesa kisha watatuma risitikwa uthibitisho mpaka pale kile kiasi cha fedha kilichotengwa kitakapokwisha nahapo uongozi wa JF utaweka mrejesho kwa wadau waliochangia.

Lakini hata hivyo uamuzi ni wetu, vile tutakavyoona inafaa.
Mahitaji ya jumla wanayohitaji ni kama ifuatavyo, na kama kuna daktari wa Muhimbili humuJukwaani anaweza kutupa muongozo zaidi kuhusiana na mapendekezo ya dawa na vifaa tulivyoshauriwa kuvinunua.

ØBandages medium size
Ø
Sliverex Cream
Ø
Gentamicin
Ø
Paracetamol Supposifories 250mg

Kuhusu namna ya kupata ruhusu ya kutembelea hospitali hiyo inabidi iandikwe barua na uongozi wa JF na iwe addressed kwa Mkurugenzi Mkuu kisha ipelekwa kwa mkono auposta.

Wale wa Mikoani tupo pamoja, namba mshiriki nasi kama mlivyofanya mwaka jana, wadau wa Arusha Wing, Rock City Mwanza Wing, Iringa Wing, Nje ya Nchi Wing na kwingineko naomb sana tena sana mshiriki nasi ili kufanikisha hafla hii.

Baadaye uongozi wa JF utaweka namba za kutuma misaada na majina ya watakaochanga yatawekwa hapa kama kawaida yetu.

lara 1, AshaDii, Elli, everlenk, TANMO, Power to the People, Neylu, miss chagga, Zion Daughter, Asnam, sister, Fixed Point, cacico, gfsonwin, Madame B, Madame S, Fixed Point, Mentor, Dark City, NANDERA, sosoliso, Ruttashobolwa, Husninyo, Kaizer, amu, tinna cute, lin, jouneGwalu, Nameless, monaco, ladyfurahia, zumbemkuu, MwanajamiiOne, MANI, BPM, kabanga, Pleasure, CYBERTEQ, figganigga, mwaJ, Mwita Maranya,
 
hivi vijamaa mbona vinaonekana vimechoka sana???? inabidi kabla ya matembezi mle mshibeshibe kidogo
Jamii-Media-798x350.jpg
 
Mtambuzi nipo hapa unaniona na mikono yote iko juu na miguu kuunga mkono hoja! Hio picha imenikumbusha mbali sana sana hahahahaa mpwa wangu MANI njoo huku tunahitaji mchango wako. MANI wewe ndio uliacha camera ikanifanya niwe mweusi kama mkaa! Dah hahahahahaaaaaaa memories, nitachnaga na nitashiriki kwa kila hatua na kwa kila jambo njooni hapa akina everlenk .
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtambuzi kwanza ninakupongeza kwa kuzidi kuonyesha njia.. Na ninapenda nikushukuru sana kwa kunishirikisha kwenye tendo hili ambalo vitabu vyote vitakatifu vya dini zetu zinatuhimiza kufanya kama sehemu kutenda wema kwa jirani zetu..

Kwa hili tuko pamoja sana Mkuu.. Kwangu mie nitatoa ushirikiano kwa asilimia 100.. Tutawasiliana mkuu kwa simu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom