Jicho la Tai
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 1,449
- 574
nani anaweza kutuambia Namna ya kumjua mpenzi wako kama amekusaliti phisicaly
Unataka ujue ili iweje, umwache au uishi na maumivu?
Ndio mpenzi wako wa kwanza? Kama haumuamini si umuache!!!
Kama humwamini wakaa naye wa nini?
Mijitu mingne badala ya kuleta point inaanza
kuleta siasa. km huna hoja kaka kimya.
Kwani wewe ulikua unataka tukujibu vipi? haya chukua jibu aliokupa snowhite
HUNIJUI,
Pressure za nini unataka? Kwani huoni raha ya kuwa katika hayo mahusiano? Maana unaweza jivuruga sana ikitokea ni kweli ama ni uongo hizo hisia zako. Uking'ang'ana kutaka kujua kama anakusaliti ama lah, itafika wakati utamvaa! na ikitokea sio kweli utaweka dosari kubwa katika mahusiano yenu... Na ikitokea kuwa ni kweli umeshajua ni hatua gani unataka kuchukua?? Utamuacha/Utalaumu/Utamuadhibu ama una mpango wa kufanya nini? Hayo yote ni msingi kwa wewe kutaka kujua...
Hata hivyo dalili hutofautiana kwa mwanamke kama ilivyo kwa mwanaume... (Huu ndio muono wangu);
Kwa baadhi ya wanaume
- Mapenzi huongezeka kwa mke.
- Anaweza kuwa na amani, furaha, kupita kiwango cha siku zote bila sababu zozote ambazo zipo wazi kwako kuwa imemfanya kuwa hivo.
- Kutokuwa huru na simu yake kama awali (hii ni baadhi sana)
- Hasira zisizo za msingi (kuchukia mambo madogo lawama kibao!)
- Saa ingine hata tendo la ndoa kuongezeka ndani ya nyumba kuliko kawaida.
Kwa baadhi ya wanawake
- Kuongezeka dharau kwa mpenzi wake na kutojali kwa yale alikua akijali awali.
- Ghafla kuanza kujali muonekano wake kupita kiwango cha siku zote, anataka ahakikishe she is looking good kila mara.
- Yupo busy na simu yake, mwanamke mara nyingi kama ana mtu wake wa karibu ambae anawasiliana nae mara kwa mara simu haikai mbali. Kama ulikuwa ukipiga simu kumpata shuguli tokana na kuitelekeza, siku hizi ni kila ukimpigia yupo karibu na simu yake.
- Kutokukufuatilia wala kujali nini unafanya, urudi saa 9 usiku, ule ama usile haijalishi mradi unatimiza wajibu wako (take note hii hata yule ambae hatoki na kachoka tabia zako pia hufanya hivi)
Anakua na mdomo mrefu ka chuchungenani anaweza kutuambia Namna ya kumjua mpenzi wako kama amekusaliti phisicaly
nani anaweza kutuambia Namna ya kumjua mpenzi wako kama amekusaliti phisicaly
Physically? Ni ngumu kutambua ila akishanogewa huko nje, ndiyo utamtambua kirahisi tu kwa maneno na matendo yake!
Penzi kikohozi...lazima abugi stepu siyo...?