Namna ya kuangalia kupatwa kwa jua kesho Jumapili asubuhi

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Habari zenu wote,

Hizi ni tovuti pakupata video za maelezo kuhusu kuptwa kwa Jua kesho asubuhi kuanzia alfajiri hadi saa tatu asubuhi pamoja na njia za kuona tukio la kupatwa kwa kutumia vifaa vya kawaida vya kupatika majumbani. T

Tukio ni kesho alfajiri Jumapili tarehe 20 Juni, 2020, mara tu Jua linapochomoza kuanzia saa 12:37 asubuhi. Kiasi kikubwa zaidi cha kufunikwa kwa Jua ni asilimia hamsini 50% ambayo itatokea saa 1:45 na baada ya hapo itaanza kupungua hadi mwisho saa 2:50 asubuhi. Hata kama ukichelewa kidogo saa moja na nusu au saa mbili au hata saa mbili na nusu bado utaweza kuona jinsi Jua lilivyopatwa.

Angalia video upate namna ya kujitayarisha kwa kutumia vifaa vya kawaida nyumbani.

Njia salama ya kutazama jua likipatwa kesho asubuhi (Jumapili, Juni 21, 2020)


Mtaalam: Namna jua litakavyopatwa


Safe ways to watch annular solar eclipse


Kwa maelezo ya kina kuhusu kupatwa kwa Jua hasa kwa wanafunzi na watu wote soma maambatisho ya mwongu uliotolewa mahususi kwa ajili hiyo kwa Kiswahili na kwa Kiingereza:

Hizi ni njia za kufurahisha za kupata taswira ya Jua lililopatwa kwa kutumia chujio na vitu vingine venye matundu unayoweza kupata nyumbani jikoni.

Fun with pinholes yellow background.jpg



Dr Noorali Jiwaji
 

Attachments

  • AfAS_Eclipse2020_Booklet_Kiswahili.pdf
    6.3 MB · Views: 12
  • AfAS_Eclipse2020_Booklet_Eng.pdf
    6 MB · Views: 7
  • AfAS_eclipse2020_poster3.png
    AfAS_eclipse2020_poster3.png
    105.3 KB · Views: 2
  • AfAS_eclipse2020_poster6.png
    AfAS_eclipse2020_poster6.png
    126.3 KB · Views: 2
KUPATWA KWA JUA KUNA UMUHIMU KWA WAABUDUO SANAMU NA MIUNGU KAMA SEMIRAMIS NA MINGINEO KWA MAANA KWAO NI TUKIO LA KISHENZI,LAKINI SIYE TUNAE MWABUDU MUNGU MUUMBAJI WA MBINGU NA NCHI TUTAKUWA TUNAENDELEA NA SHUGHULI ZETU KAMA KAWAIDA ZISIZO NA MSONGO WA AKILI!
 
KUPATWA KWA JUA KUNA UMUHIMU KWA WAABUDUO SANAMU NA MIUNGU KAMA SEMIRAMIS NA MINGINEO KWA MAANA KWAO NI TUKIO LA KISHENZI,LAKINI SIYE TUNAE MWABUDU MUNGU MUUMBAJI WA MBINGU NA NCHI TUTAKUWA TUNAENDELEA NA SHUGHULI ZETU KAMA KAWAIDA ZISIZO NA MSONGO WA AKILI!
Mkuu unaakili za kuazima.
 
Umasikini mzigo. "Kunatusaidia" au unatakiwa kusema "kunanisaidia nini".
Kwani wanaoenda kufanya utalii unawasaidia nini?
Hii ni nature na kwa wengine wasio na stress ni burudani.
Pia usipende kuhusisha ishu yako binafsi na watu wote boss.
Case closed
 
Kupatwa jua kunatusaidia nni ?
Swali limejibiwa vizuri, lakini niongeze kuwa kiSayansi, kwa kuona tukio mwenyewe inakudhihirishia nadharia ulizofundishwa na kuelewa kamilifu jinsi asilia ya Ulimwengu wetu ulivyo badala ya kuelezwa tu au kusoma katika vitabu. Watafiti wakiangalia matukio haya kwa makini na wakipata matokeo tofauti basi hiyo husaidia kuboresha nadharia na kanuni zilizokubalika hadi hapo.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kwa njia ya kutumia ndoo au beseni yenye maji je?
Njia hii hufaa kama Jua liko juu ambayo inafanya maji yanyonye asilimia 95% ya mwanga na kuakisi asilimia ndogo tu 5% inayofika machoni, lakini kwa tukio la asubuhi Jua linakuwa chni sana kwa hivyo maji hayawezi kunyonya mwanga na nishati karibu yote ya mwanga huakisiwa kutoka kwenye sura ya maji na ukiangalia hiyo inaumiza macho. Kwa hiyo njia hii ya kutumia maji kwenye ndoo haifai kuangalia kupatwa kwa Jua saa za asubuhi mapema.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Nikafikiri kesho inayotajwa ni leo tukio limeshapita kumbe ni typing error tu ngoma bado... tunangoja kwa hamu
 
Nashkuru mkuu hatuwezi kupinga hii ni nature,kwa walio na watoto ni vizuri mkiangalia namna bora yakuwaonyesha tukio hili kwa maana elimu ni experince/uzoefu unaotokana na kujifunza kwa kutenda learn by doing, falsafa ya mwalimu nyerere akiiazima kwa mwana falsafa mwamerica aitwaye john deway. Ahsante mkuu
 
Leo hapa Dar upeo una mawingu kwa hiyo tunasubiri Jua lipande, mawingu yatatoweka baada ya muda
 
Back
Top Bottom