Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Haya mambo yakuchokozwa na kutukanwa na baadhi ya members humu halafu mimi nikimjibu nakula BAN sidhani kama imekaa sawa.Haiwezekani mtu anatoka huko anakokujua yeye anaanza kuniporomoshea matusi mazito halafu nimuangalie tu!.

Bado sijafikia kiwango hicho cha Utakatifu,kama ni nginja acha iwe nginja.

Wengine hatujaumbwa kuwa watukanaji,mimi nipo kuwaburudisha na kuwaelimisha hadhira yangu na umma wa watanzania wengi wanaojitambua,sasa anatokea mtu anaanza kukuporomoshea matusi ya nguoni kisa tu alikuja Inbox akaomba jambo fulani ukamnyima,ukimjibu kidogo tu anapelekea na wewe kufungiwa,hii siyo sawa moderators,wengine mnatuonea bila sababu ya msingi.

Kama nyuzi zangu zinakupa kero na huzipendi kwanini usipite ukatazame nyuzi zinazokufurahisha?,Kila mtu hapa anasoma anachoona kwake kina manufaa na anachokipenda,kama unaona hutaki usumbufu una-Block au Una - Ignore unaendelea na mishe zako,waachieni watu wanaotaka kujifunza na kuburudika wasome nyuzi zangu.

Hadhira yangu kwa muda wa siku zisizopungua 5 imeshindwa kupata simulizi nzuri na yenye mafunzo kwasababu tu ya watu fulani wajinga ambao hawataki kuniheshimu na kuanza kuniporomoshea matusi mazito,mimi kuwajibu imekuwa nongwa,hili halikubaliki hata kidogo moderators!.

Kuna muda tunachokozwa na kupandishwa hasira na wajinga kadhaa humu JF,sasa ajabu ni kwamba,mtu anapokutukana mara ya kwanza unamripoti hakuna hatua anayochukuliwa,mara ya pili pia ni vivyo hivyo,akikutukana mara ya tatu uzalendo unakushinda unamjibu,ukisha mjibu tu hapo ndipo Moderators wanakuja kuwaadhibu,wanashindwa kumuadhibu toka awali ulipomripoti wao wanakuja kumuadhibu ulipomjibu ambapo wanawaadhibu wote wanashindwa kumuadhibu mtoa matusi au muanzilishi wa matusi,hili halikubariki na nitaendelea kulipigia kelele.

Nimewahi kutoa mapendekezo kwenye uzi wangu mmoja uko kwenye Jukwaa la COMPLAINTS, APPRECIATION AND ADVICE(TO JF) nikasema tuwekeeni Blocking Button yenye nguvu na siyo hiyo Ignore iliyopo sasa,kwasababu kama nikishaona mtu ananitukana nitampiga Block ili aende akawatukane wazazi wake huko kwasababu wao ndiyo walimfundisha ujinga huo.

Aisee nimesikitishwa sana kupigwa BAN kwakosa ambalo limesabishwa na moja ya wapumbavu hapa JF.Wengine tunakiuka taratibu kwasababu ya kuchokozwa na siyo kwamba taratibu hatuzijui!.


Mimi ni mwema na nitaendelea kuwa mwema ila nikitukanwa lazima nijibu mapigo,kama ni kufungiwa nitafungiwa sana na nipo tayari kwa hilo!.

NIMESHINDWA KUSIMULIA STORI KWA SABABU YA WAJINGA KADHAA HAPA JF,HILI HALIKUBALIKI HATA KIDOGO NA NAUMIA SANA.

Huu ni ujumbe wenu Moderators najua uzi huu mnaupitia.


Ni hayo tu.
Pole mkuu achana nao, tusonge mbele tupe uhondo
 
Baada ya kuona hali inakuwa mbaya,kuna jamaa ambao walikuwa na mizigo yao kwenye ile boti walianza kuvua nguo wakabaki na kaptura pekee kisha wakaanza kupiga kelele ya kwamba wanaume wote tuingie chini tukasaidie kutoa maji kwa nguvu zote kupitia ndoo zilizokuwa huko kwasababu ile mashine iliilemewa.
Ungekufa tu mkuu maana si kwa akili hizo za kukubali kubali kila ujinga
 
True story kama hizi inabidi heading yake iandikwe kwa capital letters kuonesha msisitizo. Huu uzi nilikuwa naupita tu nikijua ni zile nyuzi wanaanzisha vijana wa hovyo, nilivyoingia ndani kusoma episode ya kwanza tu nikakuta ni hatari na nusu.
 
SEHEMU YA SITA



Tulichukua pikipiki zikatubeba hadi Kirungu ambapo baada ya kufika kwa kuwa Jentre yeye alikuwa mwenyeji,alitutafutia Guest House ambayo tulipaswa kila chumba kulipa elfu 15.Guest za pale Kirungu karibia zote ni choka mbaya sana,tuliamua kukaa hivyo hivyo kwasababu hakukuwa na namna.

Ilipofika Jioni Jentre alienda kumleta mtu ambaye kwa mujibu wake ndiye aliyepaswa kutupatia kilichokuwa kimetupeleka, baada ya yule mtu kufika akajifanya kutusalimia na kuongea kifaransa akidhani tunakielewa,sielewi kama Jentre hakumwambia sisi ni watanzania au alifanya makusudi ili tumuone anaweza!.

Kamugisha "Sisi hatujui French "

Yeye "Oooh,kumbe nyinyi mko ba Tanzanie eee!"

Kamugisha "Ndiyo"

Yeye "Juu huyu Jentre ameniambia sikujua! nilijua tu anafanya muchezo!"

Aliendelea "Sasa nielezeni ile kitu ambayo nyie mmekuya nayo huku Congo"

Jentre "Anasema mumueleze kile kilichowaleta huku Congo"

Kamugisha "Mimi na ndugu yangu tumekuja kutafuta utajiri,hivyo tulikutana na huyu bwana Jentre akawa ametuambia wewe unaweza kutusaidia,tunaomba utusaidie"

Yeye "Ooh wala msijali,hapa mmefika kwa mwenyewe,mimi wananiintanga makasu,ukisikia Makasu ndiyo mimi hapa kwa Kirungu muzima"

Aliendelea "Je nyie mmekuya na Makuta sababu ili niifanye kazi za kwenu inatakiwa muwe na makuta?"

Jentre "Anasema mmekuja na hela?,kwasababu ili kazi zenu ziende inapaswa muwe na hela?"

Kamugisha "Pesa tunayo"

Yeye "Moto nyonso asengeli kofuta troisi senti senkante mili"

Jentre "Anasema mnapaswa kulipa kila mtu shilingi laki tatu na nusu"

Kamugisha "Hilo halina tatizo tutalipa kwakuwa nina hamu sana hilo jambo lifanikiwe"

Yeye "Musiwe na wasiwasi hilo jambo lenyu ni ndogo sana"

Mimi kiukweli si kuwa na hela zaidi ya nauli na kiasi kidogo nilichokuwa nacho kama dharura,kumbuka niliamua kwenda huko Congo kwasababu ya jamaa ili asije akaona nilikuwa namchora na hata gharama zingine zote yeye ndiye alisema atanilipia,hivyo hata jamaa alipoomba hicho kiasi mimi sikuwa nacho,yeye ndiye aliyelipa hizo hela.

Baada ya kupewa kile kiasi,jamaa alisema hapo Guest tunapaswa kuhama kwasababu mizimu haitokubaliana na sisi kukaa kwenye Guest ambazo huwa zinalaza wazinzi;Hivyo alituambia tutahamia kwenye nyumba ya mdogo wake ambaye kwa muda huo hakuwepo alikuwa amesafiri. Ilipofika Jioni Jentre alirudi na funguo za nyumba za huyo ndugu yake na akawa ametuambia tunapaswa kuhamia huko.Ile nyumba ilikuwa niya nyasi kama kawaida na hakukuwa na godoro bali tulikuta kuna vidude fulani vimesukwa kwa ustadi kwa kutumia mabua vimekuwa kama vijamvi,hivyo ndiyo jamaa alisema yatakuwa magodoro yetu kwa siku tutakazo kuwa hapo.

Jentre "Mtaalamu kaniorodhoshea mahitaji ambayo inapaswa mnunue ili shughuli ianze na shughuli itafanyika nyumbani kwake,si mbali sana na hapa"

Aliendelea "Mahitaji ni kama yafuatavyo"

Jamaa akaanza kuyataja mahitaji moja baada ya nyingine.

1.Ulezi & Ulezi - Hivi vitatumika kutengeneza pombe kidogo ya kwenda nayo porini kwa ajili ya mizimu,siyo ombi ni lazima.

2.Mafuta ya Petroli lita 5 - Haya yatatumika kututoa hapo kwa jamaa hadi huko maporini kwenye mizimu.

3.Mkuki - Huu ni lazima upelekwe kwa mizimu huko porini ili tukubaliwe.

4.Shuka jeusi na Jeupe kwa kila mtu - Haya yatatumika huko porini.

5.Nyembe moja kila mmoja kwajili ya kupigwa Chale.

Alipotupa Orodha ya vile vifaa ilibidi tumpe hela Jentre akaviandae hivyo vitu ili viwe tayari kwa kazi.

Usiku ulipoingia tulienda kutafuta sehemu tukapata chakula kisha tukarudi kulala kwenye tule tujamvi pale chini ya sakafu ya udongo,aisee sitokaa nisahau siku hiyo kwasababu sikupata kabisa usingizi kulikochagizwa na mbu wengi nawa kutosha pia mbavu zilikuwa zinauma sana kulala pale chini,ajabu ni kwamba Kamugisha yeye alikuwa ameuchapa usingizi hadi anakoroma.

Kiukweli nilisema hata kama ni kutafuta lakini kwa hali ile yalikuwa ni mateso makubwa mno.

Namshukuru Mungu kulipambazuka na vile vifaa vikawa vimenunuliwa,sasa kabla ya kuanza lile zoezi yule mtaalamu akawa ametuambia tumpatie elfu kumi kila mmoja pesa Congo ili alale usiku aoteshwe kuhusu mambo yetu kabla hajaanza kutukarabati.Tulimpatia hizo hela na siku hiyo tukalala tena kwa mateso mle ndani na hatimaye kukakucha;Kulipokucha tena jamaa akatuambia alijaribu kufanya zoezi la kuoteshwa usiku lakini hakuona kitu,sasa akasema usiku huo tena inabidi alale tena ili aoteshwe ili kazi iwe rahisi.

Sasa Siku ya Tatu yule Mdogo mtu alikuja kutoka huko alikokuwa ameenda,sasa tulikuwa tunapiga nae stori mbili tatu akawa anatuambia kuna sehemu alikuwa ameenda machimboni kuchimba madini,jamaa alikuwa amechoka sana.

Mimi nilipomuona tu jamaa nikajua atakuwa na maisha magumu mno,sasa nikawa najiuliza!,Kama kweli kaka yake ni Mganga kwanini asimsaidie mdogo wake akawa Tajiri?,Nilijaribu kumshirikisha hilo wazo Kamugisha lakini nikaona analipuuza kwakuwa alikuwa na imani kubwa sana kwa yule mtaalamu.Yule mdogo mtu alijua sisi ni marafiki zake na kaka yake na yeye ndivyo alivyo mwambia.Yule jamaa alilala usiku mmoja tu kesho yake akawa ameondoka kurudi huko machimboni kwake.

Mimi "Kaka mbona kama jamaa inaonyesha amechoka sana?,Kwanini kama jamaa yake ni mganga kweli asimsaidie?"

Kamugisha "Mdogo wangu waganga huwa wanamipaka,unaweza kukuta familia yake inapata taabu ila watu wengine wanasaidiwa vizuri tu,wala hilo lisikushitue mdogo wangu"

Aliendelea "Jamaa inaonekana anajua"


Niliamua kukaa kimya ila kichwani mwangu nilikuwa nina maswali mengi sana.

Sasa baada ya siku tatu jamaa akatuambia alioteshwa mambo yetu na hivyo usiku tulipaswa kwenda kwake ili atuambie alichokuwa ameoteshwa.Kweli,ilipofika usiku tukaelekea nyumbani kwake tukiongozana na Jentre,tulipofika hapo tulimkuta akiwepo yeye na mke wake na wakiwa kwenye nyumba ya nyasi kama kawaida.

Tulikaa sebuleni kama nusu saa kisha tukaanza kusikia huko ndani mtu anaguna kwa vishindo vikubwa kana kwamba amenyigwa na kiazi kooni.


Naendelea.................
 
Nikiwa navuka maji kuingia Congo nikaona nimpige picha mvuvi aliyekuwa akipambana na upepo kupiga kasia akiwa na mtumbwi wake.
 

Attachments

  • IMG-20230405-WA0004.jpg
    IMG-20230405-WA0004.jpg
    174.7 KB · Views: 81
Back
Top Bottom