Namna Bora ya Usawa wa Kijinsia ni ipi?

Sep 20, 2007
69
2
Mimi ni myu ambaye napenda kuona usawa wa kijinsia unakuwepo nchini kwetu. Huwa napata shida kidogo swala la usawa wa kijinsia linavyotekelezwa na sera mbalimbali hapa nchini. Najuavyo mimi nchi inaku wa na usawa wa kijinsia pale ambapo mtu yeyote bila kujali jinsia yake anaweza kupata nafasi au kufanya jambo lolote bila kujali ujinsia wake. Yaani kuna kuwa na uhuru wa kufanya, kuamua, na kupata kile anachokihitaji kutokana na uwezo wake na siyo jinsia yake.

Kwa mtazamo wangu swala hili la ujinsia linaelekea kwakandamiza akina mama na kuwaona kuwa wao ni watu ambao hawana uwezo, hivyo inabidi wabebwe bebwe tu ili kuwa nao katika vyuo, sehemu za kazi na hata katika siasa.

Baada ya kuwajengea uwezo na kuwa motivate kushiriki katika shughuli mbali mbali sasa tunawabeba kila kila kitu. Kwa maoni yangu kufanya hivi hatuwasaidii bali tuna wachimbia kaburi. Vitu kwa wabunge viti maalum vya wabunge kwa maoni yangu vinawalemaza wanawake. Maana sasa badala ya wanawake kuwa active kushiriki siasa za majukwaani, watakaa na kusubiri viti maalum. Tunajenga jamii gani?. Kwa nini vyama vya siasa visikubali kuwa usawa uanzie katika kusimamisha wagombea wa ubunge? Kwa mfano kama chama kinajali usawa, basi kihamasishe wanachama wake wanawake wajitokeze kugombea ubunge katika majimbo halafu wakati wa mchujo wapitishe majina ya wagombea wengi wanawake hata kufikia 50% ya wagombea wawe wanawake na 50% wawe wanaume.

Kwa kufanya hivi kutaleta at least usawa na kuwawezesha akina mama kushiriki siasa kwa kijiamini zaidi. Lakini hivi viti vya bure (maalum) sidhani sana kama vitatuwezesha kufikia lengo letu la usawa wa kijinsia.

Rais Kikwete amefika mahali sasa, eti nafasi ya uteuzi ikitokea kama kuna jina la mwanamkea ana mchagua mwanamke bila kuangalia vigezo vya msingi. Nafikiri kauli kama hizi pia siyo nzuri kutamka hadharani maana zinaonyesha wanaoteuliwa siyo kwamba walikuwa na uwezo bali ni kwa sababu walikuwa wanawake. Hata kama rais alikuwa na nia nzuri ya kuwa promote wanawake lakini asiseme hadharani.

Hali kadhalika hata katika nafasi za elimu ya juu, kushusha kiwango cha kufaulu kwa wasichana hatusaidii sana. Cha msingi ni kuwajengea uwanja sawa wasichana na wanaume katika level ya familia ili mwisho wa siku washindane kwa alama. Sasa wasichana wengi wnabweteka na kutoweka bidii kwa sababu viwango vyao vya kufaulu viko chini. Kufanya hivi tunabagua na kuwadidimiza wavulana. Tusipoangalia hii hali na kuchukua hatua tutajenga jamii ambayo wanawake hawana uwezo na hivyo kutegemea huruma ya kubebwa.
 
Nadhani tatizo ni kuwa kutengeneza level playing field inachukua mda mrefu sana, inabidi ubadili fikra za jamii na existing power stuctures.

So in the mean time unakua unawapa a helping hand kama wamarekani weusi na wanawake marekani chini ya Affirmative Action na Blacks(back people,coloured people,indians and CHINESE!!) nchini South Africa wanapewa upendeleo through Black Economic Empowerment.
 
Last edited:
Back
Top Bottom