Namna ambavyo wanawake wamekuwa chanzo Cha upungufu wa nguvu za kiume

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Sep 3, 2022
1,574
3,029
Habari Wana JF ,Napenda kuwatakia heri ya msimu wa pasaka.

Moja Kwa Moja niende kwenye mada

Kumekuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume Kila iitwapo Leo katika Dunia ya sasa.Zipo sababu nyingi zilizochangia tatizo hili ikiwemo kujichua Kwa wanaume pamoja na sababu zingine kadha wa kadha.

Utafiti pia unaonyesha jambo la kustaabisha kuwa wanawake wamekuwa chanzo Cha upungufu wa nguvu za kiume. Wanaweza wakashangazwa lakini ndyo uhalisia wenyewe na wanatakiwa wajirekebishe Kwa kuwa huu ufahamu hawajaupata Kwa bahati Mbaya siku ya Leo.

Zifuatazo ni njia ambazo wanawake wamepelekea kupungua Kwa nguvu za kiume;

1 Namna yao ya uvaaji; Kutokana na maendeleo ya Dunia katika swala la mavazi nguo za wanawake zimefanyiwa ugunduzi mwingi Sana.Wanawake wanavaa nguo zinazochora na kukumbatia maungo Yao kiasi kwamba kIla kitu kina kuwa wazi hata Kwa watu ambao hawakutarajia watakuja kukuona mwili wa mwanamke.

Kibaya zaidi ni kwamba hizo nguo pamoja na kuchora maungo Yao Bado hazisitiri hayo maungo vizuri.Nguo zisizositiri mapaja, maziwa,mgongo.

Hii hali inapelekea Ubongo wa mwanaume kuona na kutafsiri kwamba hivi vitu ni vya kawaida Sana na hata anapoingia kufanya mapenzi na mwenza wake msisimko Unakuwa umepungua ukilinganisha na kama hangewahi kuona haya maungo mara Kwa mara.Kwahivyo kiwango Cha kufanya hayo mapenzi kitapungua(Mwanamke jisitiri hata ukiwa ndani ya nyumba ya mume wako Ili unapokuwa faragha akuone wa tofauti na sio kujiachia tu)

Maungo ambayo yalitakiwa kuonekana watu wakiwa faragha yanaonekana sasa hadharani.Watu wanayazoea kiasi kwamba hata hisia mtu anakosa kwenye mapenzi.

Na ndiyo maana Kuna Jamii kama waislamu zinazokemea wanawake kuvaa nguo zisizo na staha sababu haziishii kuvunja maadili lakini pia zina punguza ufanisi wa tendo la ndoa

2 Wanawake kuwakashifu wanaume wakati wa tendo la ndoa:
Hichi ni kitu ambacho mwanamke anatakiwa kuwa nacho makini Sana la sivyo anaweza akamharibu mwanaume wake kisaiokolojia na kamwe asiwahi kuridhishwa na huyo mwanaume mpaka anaingia kaburini.

Wanawake wanapaswa kutambua kuwa mwanaume anapoingia kufanya mapenzi anatakiwa ajiamini na awe na saikolojia nzuri.Saikolojia na huku kujiamini kunapoharibiwa tegemea kilema Cha maisha Kwa Mumeo.

Sio Kila siku mwanaume atafanya mapenzi Kwa kiwango unachotaka wewe mwanamke.Inapotokea hivi badala ya kumtupia lawama na kumkebehi ilitakiwa uwe ni WA kumtia Moyo.

Wanawake wengi wamekuwa wakifanya makosa makubwa ya kukimbilia kutupa lawama Kwa wanaume wakijua Wanajenga kumbe wanabomoa.

Unapomtupia lawama boyfriend au mume wako unamjengea hofu katika kusex na wewe.Maana Kila anapokuwa anawaza kusex anawaza nisipomfikisha itakuwaje.Fikiria pale mwanafunzi anapokuwa anasemwa vibaya na mwalimu Kila anapokosea kujibu.Huyu mwanafunzi hata kama anajua kitu mwalimu akimuuliza swali atasema hajui.Ni SAWA SAWA na boyfriend au mume wako.

Unaweza kuona unaingia kufanya mapenzi lakini baada ya kumuambia Yale maneno ya lawama akiyakumbuka basi jongoo hapandi kabisa.Wewe ulidhani umeyajenga Kwa kumtupia kebehi na kumlaumu lakini Yale maneno yalimuaharibu zaidi ya ulivyodhani.

Utakazana kumshika na kumchezea kadri uwezavyo asimame lakini hakuna kitu.Hapo utagundua kumbe ulimuadhiri Kwa maneno Yako.Anaweza akadhani ana upungufu wa nguvu za kiume hata akikutana na wanawake wengine lakini kumbe ni saikolojia uliyomjengea.Kwa hivyo wanawake muwe makini Sana na mnachokiongea.

Hakuna mwanamke anayechukua hatua chanya anapogundua mume anafanya chini ya kiwango wengi wanachukua hatua hasi ya kumlaumu na kutukana wakidhani Wanajenga kumbe ndyo wanaendeleza tatizo mara mbili yake.


##############################################################
 
Ugonjwa wa nguvu za kiume haupo ni illusion narudia tena huo ugonjwa haupo ni matatizo tu ya maisha na waganga wa tiba asili wanatumia kupiga pesa ila hilo tatizo halipo.
Mengine ni kuaminishwa tu kwamba Hauna nguvu za kiume ila ukikaa kwenye hali ya Kawaida unakuta nguvu zipo tu
 
Back
Top Bottom