Namkumbuka rafiki yangu Ali Abdallah Kazua

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
NAMKUMBUKA RAFIKI YANGU ALI ABDALLAH KAZUA

Mwaka wa 2021.
Utasema jana.

Nilikuwa nikikaa na Kazua tunakumbushana mengi sana ya zamani.

Kazua siku moja kanipa kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru.

Mangara Tabu alikuwa President wa Yanga na Ayubu Kiguru alikuwa shabiki mkubwa wa Sunderland.

Ayubu Kiguru alikuwa na ubao wa biashara sokoni Kariakoo.
Wakati wa ujana wake Kazua alikuwa mkoba, yaani "centre half," wa Dundee United.

Leo mimi na sahib yangu Kazua akitutokea simba ghafla tumeliwa.
Miguu hainyanyuki ardhini haitaki inatukatalia sharti tuibembeleze.

Mzee Mangara Tabu alikuwa President wa Yanga na Ayubu Kiguru alikuwa shabiki mkubwa sana wa Sunderland na unaweza kusema ndiyo Haji

Manara wa enzi hizo.
Haji mwanafunzi kwa Ayubu.

Ayubu alikuwa na kipaji cha ajabu.
Mtu wa vibweka lukuki.

Sunderland ikichukua kikombe asubuhi anakujanacho sokoni anakiweka mbele ya ubao wake washabiki wa Sunderland wakija sokoni wanatunza.

Hapo Ayubu kavaa jezi no. 6 ya Hamisi Kilomoni.

Jioni soko likifungwa anahesabu fedha zilizotunzwa anapeleka club Congo na Mchikichi.

Soko zima lile limejaa wanazi wa Yanga basi Ayubu peke yake anapambananao na mwisho wa siku wanasalimu amri wanafunga virago hao wanaondoka.

Siku hiyo Mzee Mangara kenda sokoni kununua mahitaji yake.

Ayubu kumuona Mzee Mangara akamuamkia kisha akamwambia, "Mzee Mangara kanunue hiliki tu basi.

Vingine vyote vilivyobakia njoo uchukue kwangu bure."
Yanga ilikuwa imefungwa na Sunderland.

Mzee Mangara akamshukuru Ayubu kisha akamwambia, "Tutakutana Ilala Stadium."

Ayubu akamjazia vitu Mzee Mangara kwenye jumu lake, Mzee Mangara akimshukuru Ayubu akashika njia kwenda nyumbani kwake ambako hapakuwa mbali na sokoni.

1708961423021.jpeg

Ali Abdallah Kazua
1708961486249.jpeg

Hamisi Kilomoni
1708961590826.png

Soko la Kariakoo 1950/60s​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom